Ni Tanzania pekee Bunge husimama na Serikali na kuwaacha Wananchi

chotera

JF-Expert Member
May 19, 2016
6,305
15,034
Kwa maneno ya Naibu Spika Tulia Ackson na Ndugai inaonesha Bunge halina meno na ni chombo kisichoweza kuisimamia serikali.

Kwa tafsiri rahisi ndio maana hua kazi kubwa ya wabunge ni kupiga makofi na kusema ndioooooooo na kusema naunga hoja mkono asilimia mia moja na kazi yao nyingine ni kupitisha kila kitu kinachopelekwa na serikali.

Bunge liko pale kuisaidia serikali na sio kama muhimili huru wa kuisimamia serikali, naona kabisa tuendako giza nene kuliko kawaida.

Hiyo pia inaweza kua sababu ya nchi kutokupiga hatua kimaendeleo lakini pia ukuaji wa demokrasia kudumaa na uwepo wa sheria nyingi za ajabu kwa mfano sheria ya vyombo vya habari, sheria ya vyama vya siasa

Kiujumla kuna tatizo kubwa kwa Bunge la namna hii kamwe hatuwezi kupata sheria nzuri kama nchi.
 
Back
Top Bottom