Ni soni kuu Rais kwenda Kagera kwa mbwembwe muda huu

Nadhani mkuu in bora ukaanzisha thread inayojitegemea ya "Kwanini serikali inasuasua kuamisha makao makuu ya wilaya ya Bukoba Vijijini kwenda Rubale kama ilivyokubaliwa"
wazo zuri,ntalifanyia kazi!
acha nikusanye data!
 
nadhana hapa washauri wake hawakutumia hekima kumshauri.

Ilipaswa wamshauri Aende wakati ule wa Maafa ulipotokea.

Lakini kwenda sasa haileti Maana sana ni kama anaenda kwenye ziara za kiserikali tu.
Mkuu anao washauri katika kila sekta lakini yeye ndiye anayewashauri hao Washauri.
 
Tazama unafiki wa wanakagera leo, utawaona na miguo yao ya kijani, tena watakuwa wanamshangilia kama sio wao, ngoja tuone, mwafrika hana dhamana
Mkuu usichanganye mambo! Mikutano ya kiccm ni ya ajabu sana. Unaweza kukuta mkutano Morogoro lakini waliopo na kushangilia sana ni wa Dodoma walio wezeshwa kufika huko.
 
Ni soni kuu. Ni soni kwa wote waliohusika na wanaohusika kufanikisha ziara ya Rais Magufuli mkoani Kagera. Haileti ladha,muda huu,Rais kutua Kagera kwa mbwembwe.

Lilipotokea tetemeko kule Kagera,wanaKagera walichangiwa. Kubwa zaidi,waathirika wa tetemeko walihitaji faraja. Faraja juu ya misiba iliyowakuta na mateso yaliyowakabili.

WanaKagera,kwa sauti na vitendo,vyao na vya wengine,walimhitaji Rais Magufuli. Walimhitaji kiongozi wao mkuu wa nchi akawaone na kuwafariji. Wakamsubiri bila kiburi na kwa hamu muhimu. Rais hakwenda. WanaKagera wakashangaa na kusinyaa.

Hainogi kuona au kusikia kuwa Rais anakwenda Kagera muda huu na kupanga kuhutubia kwa mbwembwe. Kisiasa,Rais hata-gain chochote!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Hayo ndio matamanio na maombi yako kuwa Rais asi gain chochote kisiasa
 
Kwa hili jambo kama tungekuwa wakweli asili mia 99 ingekubaliana na mada hii. Kwani ni ukweli kuwa safari ya mkuu Kagera kwa sasa ama wakati mwingine wowote ni - siyo plus.
 
Ni soni kuu. Ni soni kwa wote waliohusika na wanaohusika kufanikisha ziara ya Rais Magufuli mkoani Kagera. Haileti ladha,muda huu,Rais kutua Kagera kwa mbwembwe.

Lilipotokea tetemeko kule Kagera,wanaKagera walichangiwa. Kubwa zaidi,waathirika wa tetemeko walihitaji faraja. Faraja juu ya misiba iliyowakuta na mateso yaliyowakabili.

WanaKagera,kwa sauti na vitendo,vyao na vya wengine,walimhitaji Rais Magufuli. Walimhitaji kiongozi wao mkuu wa nchi akawaone na kuwafariji. Wakamsubiri bila kiburi na kwa hamu muhimu. Rais hakwenda. WanaKagera wakashangaa na kusinyaa.

Hainogi kuona au kusikia kuwa Rais anakwenda Kagera muda huu na kupanga kuhutubia kwa mbwembwe. Kisiasa,Rais hata-gain chochote!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mbaya zaidi aliwaambia tetemeko halikuletwa na Serikali wala ccm, fanyeni kazi msitegemee kujengewa nyumba na serikali
 
nadhana hapa washauri wake hawakutumia hekima kumshauri.

Ilipaswa wamshauri Aende wakati ule wa Maafa ulipotokea.

Lakini kwenda sasa haileti Maana sana ni kama anaenda kwenye ziara za kiserikali tu.
Ziara zote za rais huwa ni za kiserikali
 
Mkuu usichanganye mambo! Mikutano ya kiccm ni ya ajabu sana. Unaweza kukuta mkutano Morogoro lakini waliopo na kushangilia sana ni wa Dodoma walio wezeshwa kufika huko.

WEWE CHAKAZA MPUUI SANA. WEWE JUZI ULIHAMAISHA MH RAIS AENDE BUKOBA BAADA YA KUTOKA CHATO..SASA LEO UNAGEUKA NAKUSEMA UJINGA HAPA. NADHANI MH RAI AFANYE ANAYOONA YANAFAA KWANI KAZI YA WENGI NIKUTAKA NCHI ISIENDE MBELE.NDIYO NYIE MLISHANGILIA MCC KUONDOA MISAADA NA BAADA YA KUONDOA MNAKEJELI TENA
 
Kwa hiyo kama urais ni taasisi wewe sasa unataka tufanyaje? Kila mtu anajua hivyo, nini kipya sasa?
Akili zingine bwana ni shida, Rais unampangia mda wa kwenda Kagera, Urais ni Taasisi nasiyo JPM, kutokana na udumavu wa akili yako unadhani urais ni JPM, Viongozi wakuu wa kitaifa walishakwenda nakuwafariji ndugu zetu wa kagera na sasa mkuu mwenyewe kapata mda na amekwenda. Sijui kwanini unasema amekwenda na mbwembwe, nadhani ni udumavu wa akili yako jambo ambalo hatuna uwezo wakukusaidia labda kukuombea kwa Mola.

Yah right!!

Taasisi iliahirisha safari ya Zambia kwa ajili ya tetemeko. Taasisi ilishafika Bukoba .... hii ziara haina uhusiano wowote na tetemeko. Ni ziara ya kikazi tu!!
 
WEWE CHAKAZA MPUUI SANA. WEWE JUZI ULIHAMAISHA MH RAIS AENDE BUKOBA BAADA YA KUTOKA CHATO..SASA LEO UNAGEUKA NAKUSEMA UJINGA HAPA. NADHANI MH RAI AFANYE ANAYOONA YANAFAA KWANI KAZI YA WENGI NIKUTAKA NCHI ISIENDE MBELE.NDIYO NYIE MLISHANGILIA MCC KUONDOA MISAADA NA BAADA YA KUONDOA MNAKEJELI TENA
Hongera sana mkuu Kimla kwa kuvunja rekodi ya dunia kwa kuwa mwanadamu wa kwanza kunitukana mwaka 2017, nakupongeza sana. Hata hivyo rekodi hiyo umeivunja kwa vigezo vya kijinga sana. Jifunze kusoma katikati ya mistari ujue kilikuwa kinajibiwa kitu gani. Haikuwa kufika kwake Kagera kwani hiyo ni haki yake Raia namba moja kuwa popote pale. Hoja ni mbwembwe za tukio hilo huku mashati ya kijani yakimeremeta bila aibu.
Next time ukitaka kuvunja rekodi kama hii jipange na upangike kweli ili usije ukanyang'anywa medali yako bure!
 
Akili zingine bwana ni shida, Rais unampangia mda wa kwenda Kagera, Urais ni Taasisi nasiyo JPM, kutokana na udumavu wa akili yako unadhani urais ni JPM, Viongozi wakuu wa kitaifa walishakwenda nakuwafariji ndugu zetu wa kagera na sasa mkuu mwenyewe kapata mda na amekwenda. Sijui kwanini unasema amekwenda na mbwembwe, nadhani ni udumavu wa akili yako jambo ambalo hatuna uwezo wakukusaidia labda kukuombea kwa Mola.

Hebu twambie wewe mwenye akili nyingi ,sababu ya Raisi kukatisha ziara kipindi kile lilipotokea tetemeko sababu ipi ilimfanya akatize safari ?

mwenye akili nyingi...tunaomba majibu..
 
Back
Top Bottom