Kuna jambo nilisilo lielewa hasa ninapokutana na tambo kama hizi: "Tumejenga barabara...tumejenga shule...tumejenga hospitali...tumejenga vyuo vikuu nk nk" Ninajiuliza je hayo siyo majukumu ya kila serikali duniani? Kama ujenzi wa barabara katika nchi ni hisani? Je! Majukumu ya serikali ni yepi? Je, kodi inayokusanywa na serikali hiyo kazi yake ni nini? Au ni kufisidi kodi hizo?
Na iwapo ujenzi wa miundo-mbinu, hospitali,shule na vyuo sio jukumu la serikali, ni kwa nini basi kila nchi inakuwa na bunge la bajeti? Bunge hili kwa kila nchi hupanga bajeti za maendeleo na matumizi ya kawaida kwa taifa husika.
Imefika mahali unamsikia Waziri Mkuu akijinanga kwamba sisi tumejenga barabara ndefu na nyingi kuliko Burundi. Je, Burundi wana raslimali kiasi gani ni nyingi kuliko za Tanzania? Basi, ni bora Waziri Mkuu angeilinganisha serikali yake kiutendaji na zile za Botswana na Mauritius.
Serikali zote duniani hujenga miundombinu bora, hospitali na shule ili ziweze kuwa na jamii inayosonga mbele kimaendeleo.
Nawasihi wahusika wasijitokeze mbele ya watanzania na kutoa tambo kama hizo..vinginevyo watazomewa..watapopolewa mawe na kukimbiwa. Tambo kama hizo unaweza kuzisema kwa hadhira ya kukodishwa na kubebwa kwenye malori na kwenye coaster toka mji hadi mji mwingine ilkujaza watu mkutanoni.
Tatizo kubwa ni rushwa, eleza rushwa, chukua hatua kuikabili. Hapo utasikilizwa. Kwa sasa, hakuna mwananchi anayepata huduma yoyote pasipo rushwa. Imekuwa kawaida katika jamii huko vijijini na hata mijini, wanandugu wanachangishana fedha kwa ajili ya kutoa rushwa wanapokuwa wanadai haki ya mmoja wa ndugu yao akiwa anamashauri polisi, mahakamani, akitaka huduma hospitali, katika vituo vya afya, akitaka huduma kwa watendaji wa vijiji ama mitaa.
Rushwa ikianzia Ikulu usitarajie kuwa kuna mahali patakosa rushwa.Biblia inasema mfalme akiasi na kulaaniwa hadi taifa lake na watu wake huingia kwenye matatizo ya yanayotokana na laana hiyo. Aliweza kuishi bila laana hiyo, mwl. Nyerere, aliweza W/Mkuu. Moringe Sokoine. Waliweza kwa kuwa hawakupata madaraka kwa rushwa na ufisadi. CCM ya leo haina jipya, wameshika dola kwa rushwa, wanaishi kwa ufisadi kuanzia mabalozi wao wa nyumba kumi hadi wenyeviti wa jumuiya za chama; makatibu, wakuu wa wilaya, mikoa, wabunge, mawaziri, hadi huko ikulu.