Ni Serikali au CCM ndio inayonuka DAMU?

Ni Serikali au CCM ndio inayonuka DAMU?

Joined
Dec 11, 2010
Posts
3,321
Reaction score
6,331
Wakuu.

Mwaka jana rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa anahutubia wajumbe wa kamati kuu ya CCM alikionya chama chake kuacha kutumia Polisi na vyombo vingine vya usalama kukabiliana na nguvu ya CHADEMA. Raisi alipotoa kauli hiyo tayari wanachama kadhaa wa CHADEMA walikuwa washauwawa kwenye harakati za chama chao katika maeneo kadhaa ikiwemo Arusha, Mwanza, Morogoro, na Tabora.

Mauwaji haya yanatafsirika kama mauwaji yaliyofanywa nje ya ridhaa na mamlaka ya mahakama yaani "Extra Judicial Killings". (Extra Judicial Killings can be defined as deliberately killing not authorized by a previous judgement pronounced by a regularly constituted court affording all the judicial guarantees which are recognized as indispensable by civilized peoples".

Kwa bahati mbaya rais alipo kuwa anatoa agizo la CCM kutokutegemea Polisi kwa wajumbe wa CCM, tayari CHADEMA walisha muandikia barua ya kumuomba aunde tume huru ya kimahakama itakayo ongozwa na majaji ili kuchunguza vifo vyenye utata vilivyo tokea kwenye maeneo kadhaa hapa nchini ikiwemo kwenye mkutano yao, kwa bahati mbaya tarifa za ndani nilizo kuwa nazo ambazo hata viongozi kadhaa wa CHADEMA walisha wahi kulalamika hadharani ni kwamba rais hakuwahi kuwajibu barua yao iliyokuwa na hitaji hilo la msingi kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu.

Mauwaji ya watanzania wenzetu yametokea huku sheria zikikataza mtu yoyote kuondosha uhai wa mtu mwingine au kupanga kuondosha kwa sababu yoyote ile iwayo. Na kama ikitokea mtu yoyote kusababisha kifo cha mtu mwingine basi mtu huyo moja kwa moja anakuwa na kesi ya mauwaji. "Any person who with malice aforethought, causes the death of another person by an unlawful act or mission is guilty of the murder".
Kuna baadhi ya viongozi wa CCM wamehusika kwa namna moja au nyingine kutoa matamko au vitisho au hata kuhusika na mawauwaji ya raia au wanachama wa vyama vingine, mfano kiongozi wa CCM kule Arumeru ilidhibitika kuwa alishiriki kumuuwa kiongozi wa CHADEMA (Msafiri Mbwambo) kwa kumkata shingo kwa msumeno wa kukatia mbao lakini baada ya kukamatwa baadae akatorokoa kwenye eneo la mahakama akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wenye silaha na mpaka sasa hakuna hatua au dalili ya kukamatwa kwake. Inasemekana uliachwa upenyo wa yeye kutoroka mbele ya Polisi kwa hila ili kukiepusha chama chake na tope la uchafu wa mauwaji.

Lakini pia kuna kauli ambazo zinaweza kutafsirika kama mission, ambazo zimesha wahi kutolewa kwenye hadhara na viongozi kadhaa wa CCM na baadae mauwaji yakatokea tena katika eneo hilohilo lakini hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye alisha wahi kuhojiwa kwa kauli zake kutokana na mauwaji yaliyotokea. Mfano siku moja kabla ya kulipuliwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA pale uwanja wa AICC ambapo watu 3 waliuwawa kwa mabomu na risasi, kiongozi wa CCM (Mwingulu Nchemba) alishatoa kauli inayo tafsirika kama kauli iliyo sababisha mauwaji kwa kusema "...WATAKAO CHAGUA UPINZANI WATAKUFA..." na kesho yake wakafa watu 3 kwenye kuhitimisha kampeni za chama pinzani (CHADEMA).

Kwenye kitabu cha kituo cha sheria na haki za binadamu cha 2012 "HUMAN RIGHT REPORT 2012" UK 21 wameorodhesha matukio yaliyosababisha mauwaji nje ya mamlaka ya mahakama, na mauwaji haya unaweza kutafsiri kuwa yanaifanya serikali ya CCM inuke damu au serikali yenye viongozi wanao tembea huku matone ya damu yanamwagika kwenye viganja vya mikono yao.

Kwa mwaka 2012 kuanzia Januari hadi Disemba orodha ya watu waliouwawa kwa kuonyesha Mwezi, Mahali na Mhusika ni kama ifuatavyo:

JINA
MWEZI
MAHALI
MSABABISHI
1. JACKSON BHOKE
JAN
NYAMONGO
POLISI
2. MGOYO MGOYO
JAN
MUSOMA RURAL
POLISI
3. MIPAWA SAMWELI
FEB
MUSOMA RURAL
SUNGUSUNGU
4. TUNGURA WANSIMBA
FEB
NYAMONGO
MINE SECURITY OFFICER
5. THEODAT NGONYANI
FEB
BOMBAMBILI
POLISI
6. MOHAMEDI SAID
FEB
BOMBAMBILI
POLISI
7. ALLY SAID
FEB
BOMBAMBILI
POLISI
8. HASAN MGALU
MACHI
URAMBO
POLISI
9. SAIDI MSABAHA
MACHI
MBEYA
POLISI
10. SANYIWA NDAHYA
MACHI
MORO
TPDF
11. NG’EREBENDE NCHAMBI
MACHI
ULANGA MORO
TPDF
12. KASHINJE MSHESHIWA
MACHI
ULANGA MORO
TPDF
13. KULWA LUHENDE
MACHI
ULANGA MORO
TPDF
14. LUTALA NDAHYA
MACHI
ULANGA MORO
TPDF
15. SELEMANI MSHAWEJI
MACHI
ULANGA MORO
TPDF
16. JOSEPH CHACHA
MAY
NYAMONGO
MINE SECURITY OFFICER
17. DANIEL NSIMBA
MAY
NYAMONGO
MINE SECURITY OFFICER
18. MGOSI MAGIGE CHACHA
JUNE
NYAMONGO
MINE SECURITY OFFICER
19. JUMA JAMSON
JUNE
SERENGETI
TANAPA SCOUTS
20. KUMTANGE JUSARIO
JUNE
ARUSHA
MWIBA SECURITY GUARD
21. ALLY ZONA
JULY
MOROGORO
POLISI
22. DAUDI MWANGOSI
SEPT
NYOLOLO- IRINGA
POLISI
23. PAUL SAVYA
OCT
NYAMONGO
POLISI
24. RODGERS MWITA
OCT
NYAMONGO
POLISI

KWA ORODHA HII NI SERIKALI AU CCM NDIO INAYONUKA DAMU?
 
Mohammedi Mtoi.

Poleni sana kwa kutatishwa tamaa na harakati za Chadema.

Twende zetu Lushoto tukale matunda huku tukijadili ammbo muhimu ya kitaifa.

Hicho chama kwanza waachie wenyewe, kitakuumiza kichwa tu.

Tuna vitu vingi vya kuongea kaka. Tenga muda twende Lushoto...
 
Ni CCM ambayo inaiongoza serikali ambayo ina hivyo vyombo vya dola.
 
Wakuu.

Mwaka jana rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alipokuwa anahutubia wajumbe wa kamati kuu ya CCM alikionya chama chake kuacha kutumia Polisi na vyombo vingine vya usalama kukabiliana na nguvu ya CHADEMA. Raisi alipotoa kauli hiyo tayari wanachama kadhaa wa CHADEMA wakiwa washauwawa kwenye harakati za chama chao katika maeneo kadhaa ikiwemo Arusha, Mwanza, Morogoro, na Tabora.

Mauwaji haya yanatafsirika kama mauwaji yaliyofanywa nje ya ridhaa na mamlaka ya mahakama yaani "Extra Judicial Killings". (Extra Judicial Killings can be defined as deliberately killing not authorized by a previous judgement pronounced by a regularly constituted court affording all the judicial guarantees which are recognized as indispensable by civilized peoples".

Kwa bahati mbaya rais alipo kuwa anatoa agizo la CCM kutokutegemea Polisi kwa wajumbe wa CCM, tayari CHADEMA walisha muandikia barua ya kumuomba aunde tume huru ya kimahakama itakayo ongozwa na majaji ili kuchunguza vifo vyenye utata vilivyo tokea kwenye maeneo kadhaa hapa nchini ikiwemo kwenye mkutano yao, kwa bahati mbaya tarifa za ndani nilizo kuwa nazo ambazo hata viongozi kadhaa wa CHADEMA walisha wahi kulalamika hadharani ni kwamba rais hakuwa wahi kuwajibu barua yao iliyokuwa na hitaji hilo la msingi kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu.

Mauwaji ya watanzania wenzetu yametokea huku sheria zikikataza mtu yoyote kuondosha uhai wa mtu mwingine au kupanga kuondosha kwa sababu yoyote ile iwayo. Na kama ikitokea mtu yoyote kusababisha kifo cha mtu mwingine basi mtu huyo moja kwa moja anakuwa na kesi ya mauwaji. "Any person who, who with malice aforethought, causes the death of another person by an unlawful act or mission is guilty of the murder".
Kuna baadhi ya viongozi wa CCM wamehusika kwa namna moja au nyingine kutoa matamko au vitisho au hata kuhusika na mawauwaji ya raia au wanachama wa vyama vingine, mfano kiongozi wa CCM kule Arumeru ilidhibitika kuwa alishiriki kumuuwa kiongozi wa CHADEMA (Msafiri Mbwambo) kwa kumkata shingo kwa msumeno wa kukatia mbao lakini baada ya kukamatwa baadae akatorokoa kwenye eneo la mahakama akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wenye silaha na mpaka sasa hakuna hatua au dalili ya kukamatwa kwake. Inasemekana uliachwa upenyo wa yeye kutoroka mbele ya Polisi kwa hila ili kukiepusha chama chake na tope la uchafu wa mauwaji.

Lakini pia kuna kauli ambazo zinaweza kutafsirika kama mission, ambazo zimesha wahi kutolewa kwenye hadhara na viongozi kadhaa wa CCM na baadae mauwaji yakatokea tena katika eneo hilohilo lakini hakuna kiongozi yoyote wa CCM ambaye alisha wahi kuhojiwa kwa kauli zake kutokana na mauwaji yaliyotokea. Mfano siku moja kabla ya kulipuliwa bomu kwenye mkutano wa CHADEMA pale uwanja wa AICC ambapo watu 3 waliuwawa kwa mabomu na risasi, kiongozi wa CCM (Mwingulu Nchemba) alishatoa kauli inayo tafsirika kama kauli iliyo sababisha mauwaji kwa kusema "...WATAKAO CHAGUA UPINZANI WATAKUFA..." na kesho yake wakafa watu 3 kwenye kuhitimisha kampeni za chama pinzani (CHADEMA).

Kwenye kitabu cha kituo cha sheria na haki za binadamu cha 2012 "HUMAN RIGHT REPORT 2012" UK 21 wameorodhesha matukio yaliyosababisha mauwaji nje ya mamlaka ya mahakama, na mauwaji haya unaweza kutafsiri kuwa yanaifanya serikali ya CCM inuke damu au serikali yenye viongozi wanao tembea huku matone ya damu yanamwagika kwenye viganja vya mikono yao.

Kwa mwaka 2012 kuanzia Januari hadi Disemba orodha ya watu waliouwawa kwa kuonyesha Mwezi, Mahali na Mhusika ni kama ifuatavyo:

JINAMWEZIMAHALIMSABABISHI
1. JACKSON BHOKEJANNYAMONGOPOLISI
2. MGOYO MGOYOJANMUSOMA RURALPOLISI
3. MIPAWA SAMWELIFEBMUSOMA RURALSUNGUSUNGU
4. TUNGURA WANSIMBAFEBNYAMONGOMINE SECURITY OFFICER
5. THEODAT NGONYANIFEBBOMBAMBILIPOLISI
6. MOHAMEDI SAIDFEBBOMBAMBILIPOLISI
7. ALLY SAIDFEBBOMBAMBILIPOLISI
8. HASAN MGALUMACHIURAMBOPOLISI
9. SAIDI MSABAHAMACHIMBEYAPOLISI
10. SANYIWA NDAHYAMACHIMOROTPDF
11. NG'EREBENDE NCHAMBIMACHIULANGA MOROTPDF
12. KASHINJE MSHESHIWAMACHIULANGA MOROTPDF
13. KULWA LUHENDEMACHIULANGA MOROTPDF
14. LUTALA NDAHYAMACHIULANGA MOROTPDF
15. SELEMANI MSHAWEJIMACHIULANGA MOROTPDF
16. JOSEPH CHACHAMAYNYAMONGOMINE SECURITY OFFICER
17. DANIEL NSIMBAMAYNYAMONGOMINE SECURITY OFFICER
18. MGOSI MAGIGE CHACHAJUNENYAMONGOMINE SECURITY OFFICER
19. JUMA JAMSONJUNESERENGETITANAPA SCOUTS
20. KUMTANGE JUSARIOJUNEARUSHAMWIBA SECURITY GUARD
21. ALLY ZONAJULYMOROGOROPOLISI
22. DAUDI MWANGOSISEPTNYOLOLO- IRINGAPOLISI
23. PAUL SAVYAOCTNYAMONGOPOLISI
24. RODGERS MWITAOCTNYAMONGOPOLISI

KWA ORODHA HII NI SERIKALI AU CCM NDIO INAYONUKA DAMU?
Mtoi wewe kichwa chako sijui kimejaa maji vitu unavyoongea ni vya kibavicha zaidi sijui utaacha lini uongo mmehangai na zitto weeeeee kawashinda .

kama wewe ni mtenda haki twambie chacha wangwe mlimfanya nini baada ya hapo grace mbowe naye vipi.
 
Ni CCM ambayo inaiongoza serikali ambayo ina hivyo vyombo vya dola.
ndo tuseme askari wa NYPD akikurarua risasi,kinalaumiwa chama cha democrat?.

Mijitanzania inajifanyaga mijuaji sana,mda wote kuongea ugoro,action zero.
 
chadema ndiyo wananuka damu bana yale mauaji ya kule arusha mliyouwa watu si mchezo.
 
mohamed mtoi tangu usukumwe nje ya mlango wa makao makuu chadema bado hauko sawa kile chama kinawenyewe na bado watakuja wakupe tofari la utosi kama mwigamba.
 
Mohammedi Mtoi.

Poleni sana kwa kutatishwa tamaa na harakati za Chadema.

Twende zetu Lushoto tukale matunda huku tukijadili ammbo muhimu ya kitaifa.

Hicho chama kwanza waachie wenyewe, kitakuumiza kichwa tu.

Tuna vitu vingi vya kuongea kaka. Tenga muda twende Lushoto...

mkuu kijana alivamia rambo la majia bila kujua kina chake sasa anajuta na hajui pakutokea kwa sasa kijana huyu ni mtu wa kutumwa tu hana thamani tena tumpe pole.
 
Maccm yanapanga serikali inatekeleza!
 
Inatia uchungu sana,,,,kuna wengine wanachangia mambo ya hovyo hovyo kwasababu hayawahusu kwakuwa wao wapo salama na ndugu zao wapo salama pia lakini hawajui kesho au kesho kutwa,,,,inauma sana,,,

kamwe hatutakuwa waoga hata siku moja ,,maana uwoga ni dhambi kubwa sana...
 
chadema wameua watu wengi halafu leo mtoi hata aibu hana anaongea vituko bila hata kujistukia anachokifanya.
 
Inatia uchungu sana,,,,kuna wengine wanachangia mambo ya hovyo hovyo kwasababu hayawahusu kwakuwa wao wapo salama na ndugu zao wapo salama pia lakini hawajui kesho au kesho kutwa,,,,inauma sana,,,

kamwe hatutakuwa waoga hata siku moja ,,maana uwoga ni dhambi kubwa sana...
Mwambie mtoi atwambie chama chake kilimfanya nini wangwe.
 
Asante kamanda kwa ujenzi wa hija hii,

Rais alishawaonya wanachama wake kutotumia vyombo vya dola, hii inamaanisha kuwa ccm hutumia vyombo vya dola kukabiliana na upinzani,

ccm na serikali wananuka damu
 
Chacha wangwe mlimpeleka wapi?

mohamed mtoi tangu usukumwe nje ya mlango wa makao makuu chadema bado hauko sawa kile chama kinawenyewe na bado watakuja wakupe tofari la utosi kama mwigamba.

chadema ndiyo wananuka damu bana yale mauaji ya kule arusha mliyouwa watu si mchezo.
Mtoi wewe kichwa chako sijui kimejaa maji vitu unavyoongea ni vya kibavicha zaidi sijui utaacha lini uongo mmehangai na zitto weeeeee kawashinda .

kama wewe ni mtenda haki twambie chacha wangwe mlimfanya nini baada ya hapo grace mbowe naye vipi.
Mohammedi Mtoi.

Poleni sana kwa kutatishwa tamaa na harakati za Chadema.

Twende zetu Lushoto tukale matunda huku tukijadili ammbo muhimu ya kitaifa.

Hicho chama kwanza waachie wenyewe, kitakuumiza kichwa tu.

Tuna vitu vingi vya kuongea kaka. Tenga muda twende Lushoto...
Kazi ya kumchafua zitto imewashinda mmehamia kuichafua serikali kazi mnayo.
vijana wa buku 7 embu oneni damu hiyo ya binadamu wenzetu ilivyofanywa kwa maagizo ya chama chenu cha CCM, hembu kila mmoja hapo alipo atulie kwa dakika moja tu kutafakari juu ya familia za hao marehemu ama kwamba wawe ni ndugu jamaa au rafiki, na mjitazame na hizo buku 7 mnazochukua, tafakari!!!!!!
 
Back
Top Bottom