magari ya Serikali twayaona sana usiku kwenye magesti ya huku Sinza.
Na hawakomi coz kila kukicha yanapigwa power window na vikolokolo vengine vya kuuzika maeneo ya Kariakoo Gerezani...
ila kwenye hizo picha nimeona wananchi wengi sana hapo! hivi hao wananchi sio serikali??
whatever we can say, sioni ubaya wowote ule......maana magari haya wanayatumia mpaka kwenye shughuli za ajabu, wanaendea mashambani kwao weekend n.k
kwa kifupi kama tumeishashindwa huko nyuma hatuwezi leo...labda kesho
imetoka hiyo
......acheni uvivu wa kufikiri....
huyu mama hana uwezo wa kuamrisha gari ya kwendea msibani,
waulizeni watu wa Protocol na wasemaji wa ofisi ya Waziri mkuu
kwanini 'itifaki' imemruhusu kutumia gari hiyo.
Kila siku mnayaona magari ya STK nk yakisubiri watoto shule mwajionea sawa tu..
Accountability mtihani ee?
UK!! we are Tanzanian for God sake!
Wakati mwingine kuiga mazuri si jambo baya.
Katika hili la matumizi ya magari ya serikali haswa kwa viongozi waandamizi (ukitoa rais, makamu wa rais, spika, waziri mkuu na jaji mkuu) wa serikali kama mawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi wa idara na wakala za serikali, wakuu wa mashirika yanayotegemea ruzuku kutoka serikali kuu n.k., kuna haja ya kuiga mfumo wa serikali ya Uingereza.
Ambapo kuna mfumo was
ministerial car pool; kiongozi wa wizara (waziri,naibu waziri, mkurugenzi, katibu mkuu) anapewa gari ya ofisi
kama yupo London tu, na tena kama amebeba makabrasha muhimu
classified documents/papers ambayo anaenda kufanyia kazi ofisini. Kama si hivyo, basi kiongozi huyo anapaswa aombe gari kutoka kwenye
pool au atumie usafiri wa umma.
Sasa kwanini na sisi katika kuandaa katiba ya wananchi, tusifikiri namna gani ya kupunguza matumizi mabaya ya gari za serikali kwa kuiga mfumo huo?! Mfumo huo utawafanya viongozi hao wawe na nidhamu na magari hayo; tuna mifano katika vyuo vya umma, ambapo kuna mfumo wa
car pool; ukitaka kutumia gari kwa shughuli ambazo haziko mahusiano ya moja kwa moja na ofisi, basi kodi gari kutoja kwenye
pool. Ingawa mfumo huu waweza kuwa na mapungufu, lakini mimi naona faida nyingi kuliko hasara.
Viongozi wa waandamizi wa wizara kama hawana jambo la maana la kiofisi, basi hasitumie gari la ofisi; atumie gari lake binafsi, si anaenda kazini?! Pia matumizi ya gari la ofisi kama ana jambo la maana la kiofisi yawe yana mipaka na mahala. Kwa mfano, kama makao yetu makuu ya nchi ni Dar es Salaam, basi iwe ni kwa Dar tu; akienda nje ya Dar kiongozi akodi gari kutoka kwenye
pool. Hili pia litaondoa kabisa utaratibu wa viongozi waandamizi wa serikali kutumia magari ya serikali kwenda kufanya kampeni za kisiasa kwenye majimbo yao na mahal apengine.