Ni sawa kununua gari ya TZS 15 Million huku ukiwa unaishi nyumba ya kupanga chumba na sebule?

Mwanzoni nilkuwa natamani sana niwe na kwangu na kweli nikafanikisha, nikawa nmehamia " lakini badae nikaja kupga garama za usafiri nilizokuwa natumia kwa mwezi , nilijikuta natumia pesa nyingi sana kutokana na umbali nipokuwa naishi .. Yaani nilkuja kujikuta hela nayotumia kwenye usafiri kwa mwezi mmoja ,inaweza kulipa kodi ya miezi 6 Kama nikiwa kwenye upangaji " na ukizingatia huko nilpokuwa nmejenga hamna miundo mbinu kama maji,,hospital, umeme .... Nikasema yote ya nini haya saivi npo zangu kwenye upangaji na maisha yamekuwa rahisi zaidi tofauti na nilpokuwa kwangu....
Watu wengi Huwa hawajiulizi hii hesabu
 
Kwa maoni yangu Mimi, kuishi kwa kupanga Nyumba ndiyo kunaweza kutuacha salama. Miji yetu imejengwa shaghala baghala kwasababu kila mmoja kwa kisenti vyake vichache anataka kujenga.

Matokeo yake vijumba ni vibaya, vimekaa kihatarishi kwa usalama na Afya za wakazi. Hakuna mpangilio bora nk.

Tungeachia kwenye uwezo wajenge Nyumba standard, wengine wawe wapangaji au wanunuaji wa Nyumba zilizokwisha jengwa.
 
Acha uoga wa maisha wewe, kila mtu ana namna yake yakucheza hili game..
 
Kwa maoni yangu Mimi, kuishi kwa kupanga Nyumba ndiyo kunaweza kutuacha salama. Miji yetu imejengwa shaghala baghala kwasababu kila mmoja kwa kisenti vyake vichache anataka kujenga.

Matokeo yake vijumba ni vibaya, vimekaa kihatarishi kwa usalama na Afya za wakazi. Hakuna mpangilio bora nk.

Tungeachia kwenye uwezo wajenge Nyumba standard, wengine wawe wapangaji au wanunuaji wa Nyumba zilizokwisha jengwa.
Serikali ingeweka utaratibu Mzuri nadhani jukumu la kujenga nyumba lingeachwa kwa taasisi chache Na wengine wawe wapangaji.Miji yetu ipo hovyo kwa vile kila mtu anajenga tena kiholela.

Sema kinachofanya watu kukimbilia kuwa Na vibanda vyao ni kipato kisichotabirika Na Kodi ambazo hazijadhibitiwa au hazijawekewa utaratibu.Kila mtu anakuja Na Kodi yake anayotaka kutoza
 
Ujenzi wa DSM sio wa hela hiyo na sio wa siku moja pia inategemea wap unataka kujenga mana sehemu nyingine hata hyo 15M bado hujapata uwanja.
 
gari ni asset nyumba ni liability kama hutaki kataa kwa mazoea ila sababu hizi zikusaidie kuelewa
  • gharama za ujenzi
  • gharama za kodi ya ardhi
  • gharama za kodi ya majengo
  • gharama ya uchakavu
  • gharama za uendesheji wa maisha tegemea familia kuongezeka hasa ndugu kwa kuwa kwa kulala na kula kupo ukilinganisha kipindi unaishi vyumba viwili hivyo bills za maji, umeme, vingamuzi, uchakavu wa thamani za ndani n.k
  • gharama ya kukamilisha nyumba inayolipiwa kodi 300,000 inahitaji si chini ya million 90 ambayo ni sawa na kuishi miezi 300 sawa na miaka 25.
gari inaweza kukusaidia kuongeza kipato kama utajipanga vizuri mfano unaweza kufanya kazi halafu ukatafuta kazi nyingine part time.
unakopesheka kirahisi
inajenga heshima
inatengeneza goodwill
inaongeza ajira kwa parking na waosha magari
inachangia pato la taifa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa unalipa zaidi kodi kadri unavyo nunua mafuta

iga uone
 
Kama ulimsaidia kutafuta au ulimpa hizo hela sawa, otherwise sidhani kama unayo haki ya kumpangia mtu matumizi yake hata anunue upuuzi...
 
Ukiwa na akili za Congo Dandies - la sape unaweza kuwa na gari huku unaishi kama panya buku

6617872-9982726.jpg
 
Kwaiyo kwa akili yako kununua kiwanja kujenga ndio ujanja wale wezi wahindi kule mjini wengi wamepanga unajuwa wana kiasi gani mwisho wako wa kufikiria ndio mwazo wa wengine kuwaza !!!
Unapo kwamia wengine ndipo wanapo anzia!!!
 
Back
Top Bottom