Ni sahihi kubana matumizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni sahihi kubana matumizi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 26, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na kilio na wito wa kutaka serikali "ibane matumizi". Siku za karibuni kumekuwa na mwitikio wa kubana matumizi ikiwemo kwa Rais kupunguza anaoambatana nao na mambo ya posho n.k Nimekaa na kufikiria hivi ni kweli kwamba tatizo letu ni kuwa tunatumia sana? au tunatumia vibaya? Ni kipi basi sahihi kufuatwa?

  a. Kubana matumizi (kupunguza matumizi ili "kuokoa fedha")na kutumia vizuri kidogo kilichopo
  b. Kuongeza matumizi na kutumia vizuri kile kingi kilichopo
  c. Kupunguza matumizi bila kujali tunatumiaje kidogo kilichopo
  d. Kuongeza matumizi bila kujali tunatumiaje hicho tunachoongeza
  e. Tutumie tu bila kujali alimradi vipo vya kutumia
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Utabana matumizi kivipi kama hujui matumizi yako? Unajua mshahara wa rais? Per diem zake je? Cost ya safari zake? Inakuwaje kuna bajeti mbili? Serikali inafuata ipi?
  Kama vitu basic havijulikani (ni siri kubwa) ni wazi kuwa hatuwezi kubana matumizi.
   
 3. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mafisadi na wahujumu uchumi washtakiwe kwanza na kurejesha pesa zote walizoiba then option yako 'a' itumike mkuu
   
 4. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa kawaida by using Monetary & fiscal policy! Increase in gvt expenditure to certain level under proper control will enhance investment as financial institution reduces interest rate but if and only if it adopt crowding-in tactic in turn increase in imployment opportunities with slight rise in general price level in short run due to increase in purchasing power of individuls! Now the govnt will increase more revenue due to increase in personal incomes and change in taxable income as well as tax base! Mkuu u a right with option "b"!

  But 4 Jk gvt it's all about UJUHA, nothing else!
   
 5. T

  Tom JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  b inafaa. Vema kubana matumizi mabaya ya pesa na rasilimali zingine lakini hapo hapo tumia hiyo pesa ama rasilimali kwa uwingi wake katika uzalishaji wa mali yenye kuuzika na kuongeza pato la nchi ama tumia kwa uwingi wake katika kuondoa majanga ya njaa, maradhi, elimu, nk.

  Namba moja ni kuongeza matumizi katika uzalishaji wakati huo huo unaondoa matumizi yasiyo ya lazima - naamini wabunge wanaweza tembelea pikipiki huko kwenye majimbo yao, mawaziri/wabunge wawapo kwenye vikao Dodoma mabasi yatawafaa zaidi pia sioni kwa nini wasitumie gari yeyote chini ya cc 2000 kwenda ofisini. Hostel zingefaa sana kwa viongozi wetu kuliko gharama za mahotelini ama kwa nini watibiwe nje ya nchi - after all wote tutakufa tu hivyo bora tukatumia mali vizuri sasa ili watoto wetu baadaye wawe na utajiri, nchi safi, maisha safi na marefu nk. Ukweli ni kua kwa umasikini wetu tulionao kwa sasa hatuwezi mudu anasa ya VX, kutibu watu Ulaya/India nk la sivyo tunakua tunaongeza ufisadi tu na kuendekeza umasikini. Ni rahisi sana kwa fisadi ama mtu yeyote binafsi kudai kua JK atibiwe kwa gharama yeyote ile popote pale, ama kua maisha ya mtu hayana bei hivyo watu wapekekwe na serikali kutibiwa nje.
   
 6. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kati ya alternatives ulizoweka mimi nadhanni A ni sahihi zaidi kwakuwa tunatumia sana kidogo kilichopo na tena tunatumia vibaya. Tukipunguza posho zisizo na kichwa wala miguu, tukiondoa magari ya kifahari yaliyotapakaa kila kona, tukidhibiti matumizi pia ya magari ya serekali (nakumbuka wakati fulani kilihitajika kibali kuendesha gari la serekali baada ya saa 12 jioni) na matumizi mengineyo na mwisho tukaangalia upya vipaombele vyetu kwa hakika tutaona mabadiliko!
   
 7. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kinachotakiwa katika nchi yetu ni kitu kimoja tu change of attitude kwa sababu mtazamo wetu kinchi haueleweki kwa hiyo tukiweza kubadili mind set yetu tutajua kutumia kwa kadri ya uwezo tulionao
   
 8. W

  We know next JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mzee Mwanakijiji,

  Nadhani ni sahihi kabisa kulijadili. Mimi nadahani kinachotakiwa kufuatwa ni suala la matumizi ya Magari ya Serikali, ambapo utaona ktk Wizara moja mathalani, utakuta kuna magari ya bei ya juu (VX, GX) karibu kila idara, na wakuu wa idara hizo ndio wanazitumia. Nadhani cha kufanya sasa ni.

  1. Kutafuta mabasi ya TATA kutoka India, ili yaweze kuwa yanawachukua wafanyakazi wa serikali ktk vituo fulani fulani na kuwapeleka maofisini, kama vilie inavyofanyika kwa baadhi ya idara za serikali na BOT.

  2. Magari hayo yote yauzwe na yabakie kama matatu ktk pool, kwa ajili ya matumizi ya kiofisi,

  3. Wakuu wa idara au hat awafanyakazi wengine, wakopeshwe magari ili kama wanataka kuyaendesha basi gharama ziwe zao.

  Nadhani kwa kufanya hivyi, tutashangaa kiasi cha matumizi kitakavyo pungua kwa nchi nzima.
   
 9. mulambakao

  mulambakao Member

  #9
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very right! Tambua uwepo wa CAG mthibiti mkuu na mkaguzi mkuu wa serikali kwanza, heshimu repoti zake kwa kuzifanyia kazi, hilo hata yeye mwenyewe ameshindwa sasa anawajibika kwa magamba badala wananchi! kisha tutambue mapato yetu kwa uwazi (siyo misaada) milingano ikieleweka tutabana matumizi, Mkapa aliyaelewa hayo akafanya mambo ingawaje aliharibikiwa mbeleni na yule mama wa kichaga akajirudisha kwa kasi kuwa First lady.

  Hapo tutapata maendeleo
   
 10. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  fikiri hii, kuacha kutumia fedha uliyo nayo bila kuboresha uzalishaji wako je hii ni kubana matumizi au ni kubana uzalishaji.
  kwetu tatizo si matumizi tu bali hata uzalishaji na usimamizi wa rasilimali na mgawanyo wake.
   
 11. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala siyo kubana matumizi tu bali kutumia kilichopo vizuri na wote tunufaike na rasilimali za nchi,haiingii akilini mtu mmoja kumiliki nyumba kumi na bado anaendelea kuiba utadhani atazikwa nazo.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Binafsi naamini tunahitaji not less than 50 Billion US Dollars Budget.. hii bajeti ya Dola bilioni 11 sijui 12.. kwenye taifa la watu milioni 45 ni kidogo sana kuleta impact kwenye maendeleo. Hivyo hoja yangu ni tuongeze matumizi.. which will bring the question - tunatumia vipi zaidi bila kuzalisha zaidi? Na utazalisha vipi zaidi bila kuwekeza zaidi?
   
 13. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Kabla hatujafika huko inabidi kwanza tujenge discipline ya kutunza na kutumia vyema tulicho nacho pamoja na kuishi maisha kulingana na uwezo. Bila ya nidhamu hii hata tuwe na bajeti ya $100Billion haitatusaidia kamwe!

  Ukitazama bajeti yetu sasa hivi hata matumizi ya kawaida yanategemea mikopo/misaada...tunataka kuishi kama matajiri wakati uwezo hatuna!
   
 14. A

  Ame JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  k
  <br>
  <br>
  Kuongeza matumizi na kutumia vizuri kile kingi kilichopo! Nchi yenye migodi saba ya gold; watu zaidi ya 40M; ardhi nzuri yenye kufaa kilimo; bahari; maziwa makuu ya Africa; Milima mirefu; Mbuga nyingi za wanyama; mawe mengi katika mikoa zaidi ya mitatu yenye kufaa kujenga; mchanga mzuri wa kujengea; wasomi wakutosha mpaka wanakosa kazi inakuwaje na kidogo kilichopo? Wa nipe mimi nchi na marupu rupu yote waone kama tutabana matumizi! Yes Daudi hakukubali ku risk kumuua Goliati bila kuambiwa akifanya hivyo atapewa nini; mimi vile vile tuwekeane mkataba kwamba niwaonyeshe tunavyoweza kustarehe kwanza kwa hivi vingi tulivyonavyo alafu baada ya hapo 2% ya kila kipato nitakacho kiinovate inakwenda kwenye personal account yangu; wao wabaki na vyeo vyao kama walivyo! tuendelee kuwaita waheshimiwa sisi wengine tuwe wafanyakazi lakini yenye malipo baada ya out put; waone kama tuta bana matumizi!
   
 15. A

  Ame JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mzee budget hiyo unataka cash tu ama umewa thamanisha na kila mtu aliye hai? Itatoka wapi wakati production ni -ve? Watu wanafanya kazi bila maarifa. Mi sihitaji pesa nyingi hivyo katika cash ila kama mchumi kila kichwa/mtu mke ama mume above 18 below 70 years (chenye uwezo wa kufanya kazi) ni mtaji tosha wa mimi kuwaonyesha watanzania how we can live in plenty with all the Natural resources we have!
   
 16. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tatizo la bajeti yetu ni tumia kadili unavyokusanya, hapa nina maana unategemea makusanyo ya kila mwezi ili utumie. Sasa hapa tatizo linakuja katika ukusanyaji wa mapato yenyewe ili kufikia lengo lililowekwa. Kuna nchi moja wanapopanga bajeti ya mwaka, pesa tayari zinakuwepo cash, kwa hiyo wao wanapanga matumizi, na wanazokusanya ni kwa ajili ya mwaka unaofuata, ili waje kuzipangia matumizi wakiwa tayari wameshazikusanya.
   
 17. P

  Paul S.S Verified User

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nadhani ili uwekeze ili uzalishe zaidi kisha tupate zaidi na tutumie zaidi inabidi hiki kidogo kilichopo kibanwe kwa shughuli zingine kama posho na burudani ili zipatikane za kuwekeza zaidi ili uzalishaji upande ili tupate zaidi kisha tutatumia zaidi.

  Kwa sasa kilio kilichopo ni kuwa gov inatakiwa ijibane kwenye matumizi yasiyo na lazima na kuelekeza nguvu nyingi kwenye kuwekeza, ni ukweli ulio wazi tunahita kutumia zaidi kulinganisha na ilivyo sasa lakini kupanga ni kuchagua.

  Kupanga ni kuchagua kwa maana ya kwamba tuchague kutumia ilimradi tunavyo vichache vilivyopo au tuwe na strategies katika matumizi yetu kwa kuamua kujinyima mengine na kutumia zaidi ktk uwekezaji ili tuzalishe zaidi.

  Wanaopigia swala hili kelele wanamaana kuwa serikali ijibane upande mmoja na itumie zaidi upande mwingine
   
 18. A

  Ame JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu tukiangalia budget tunaipnga ki uhasibu zaidi kuliko kiuchumi; kuna tofauti kati ya economic analysis na financial analysis kwenye budgetting; sijawahi sikia hata siku moja kwenye bunge letu watu wakijadili idadi ya wakulima waliopo na watafanaya nini kwa mwaka huo; idadi ya wasomi waliopo na watafanya nini kwa mwaka huo; ukubwa wa mashamba yaliyopo na yatatumiwaje kwa mwaka huo; ukubwa wa misitu uliopo na utatumiwaje kwa mwaka huo; tunaangalia tu huko hazina kuna cash kiasi gani huku tukijua uchumi wetu siyo comercialised bali bado uko ki peasant zaidi. Tuiga iga sana vitu hivi badala ya kuwa realistic; wenzetu mataifa yaliyoendelea kila kitu chao kina price index sisi ukiuliza tu bei ya unit ya kitu zaidi ya products za china; na kenya etc hakuna mwenye jibu sahihi sasa huoni kuwa kuna biashara kubwa ya exchange of goods and services zinafanyika bila media of exchange money kuhusishwa? TRA ndiyo hapo wengi wao wanapo kula kona na huwezi kuwa kamata kwa lolote maana vipimo tunafanya kwa macho zaidi kuliko SI Units maana bidhaa haziko processed. Sasa vipi ufanye budgetting ya cash tu bila kuangalia hali halisi? Tunahitaji watu kuwa more creative na tuache kufuata vitu ambavyo viko so imposed na havionyeshi uhalisia kwenye ground!
   
 19. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kubana matumizi kunatakiwa kuwe kwa vitendo,kama ni kuuza mashangingi,kupunguza posho,kupunguza safari za nje na kupunguza pia baraza la mawaziri na safari zisizo na lazima
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Sielewi haswa lengo la mada hii kwa sababu yaonyesha wewe mwenyewe una mashaka na hili neno "Kubana Matumizi" lakini ukweli unabakia kwamba serikali yeyote duniani inatakiwa kubana matumizi na ushindani mkubwa upo ktk sehemu zipi ambazo tunatakiwa kubana matumizi hayo.

  Na hata sisi wananchi ktk maisha yetu tunatakiwa kubana matumizi ilimradi kiuchumi inatambulika kwamba FAIDA huongezeka kutokana na kupungua kwa matumizi, isipokuwa swala kubwa la kuumiza vichwa ni matumizi yapi muhimu ya yapi sio muhimu ktk kuboresha biashara na maisha ya wananchi kwani vitu hivi vinakwenda sambasamba..

  Kibiashara:-
  Tofauti kubwa ipo ktk kupunguza matumizi ya kibiashara ikiwa ni pamoja na yale ya huduma kwa mrengo ambao unaamini kwamba biashara inapofanikiwa zaidi na utajiri kuongezeka automatically maisha na huduma za mhusika huboreka pia. The more you earn, more money to spend. Kwa hiyo sii vizuri kutumia mtaji katika kuboresha maisha yako kwanza isipokuwa mtaji ndio mbegu inayoweza kuleta mavuno ya maisha bora kwa maana kwamba mavuno bora ndiyo hutuwezesha kupanua matumizi. Na kama wewe ni mfanyabiashara (MTU) unatakiwa kutazama matumizi ambayo hayana umuhimu na hivyo kuzua udadisi mkubwa baina ya watu wawili. Mwingine anaweza kuhitaji gari ktk kuendesha biashara na mwingine akasema sina ulazima wa kuwa na gari kuendesha biashara hiyo hiyo. Hapa ndipo tunapoweza kupima ni matumizi yapi yabanwe ikiwa sote tunashughulika ktk biashara moja (Partnership) bila kuathiri malengo ya mavuno bora.

  Kisiasa:-
  I
  le dhana yenye malengo ya kuvuna mazao bora (quality)za zaidi (quantity) ili kuboresha maisha ya wananchi inasimama pale pale isipokuwa watu hutofautiana ktk matumizi yapi hafifu na yapi muhimu bila kupoteza lengo la kuvuna kilicho bora. Ndio unakuta wenzetu wakibishana ktk misingi ya matumizi yasiyokuwa muhimu dhidi ya yale muhimu bila kuathiri malengo..Ni ubishi unaohusu matumizi ktk kuwezesha biahsra hiyo kukua na sii nje kama sisi Wadanganyika tunavyotazama vitu hivi...

  Kwa bahati mbaya sana wanasiasa wetu hubishana ktk matumizi yao wenyewe, hubishana ktk biashara ambazo haziongezi pato wala mfuko wa Taifa kwa kutazama faida ipi itapatikana na kwa kiasi gani itaboresha maisha ya wananchi. Hoja nyingi hazihusiani kabisa na kibiashara bali politics kwa kwenda mbele bila kutazama malengo ya kuingia biashara hiyo. Na ndio maana unaona tunabishana kuhusu Posho, kuhusu safari za JK na viongozi wenza, kuhusu mishahara na posho zao, mashangingi, mafuta, nyumba, kuhusu viti vya wabunge walioteuliwa, kuongeza majimbo ya kura, na mengine mengi ambayo kibishara au niseme kiuchumi hayana uhusiano kabisa isipokuwa ni matumizi ambayo yangetokana na mavuno ila sisi tunayaweka mbele ktk mtaji na matumizi yake kama Mzaire anayenunua suti na kuendesha gari kubwa huku akilala chini na kuomba hela za mafuta, au muuza unga anayerudi mjini na kutumia hadi mtaji ili mradi apatwe kuimbwa na twanga pepeta..

  Nchi yetu hakika tunatazama karibu sana, pengine upeo wa wasomi na wanasiasa wetu ni mdogo sana kibiashara kiasi kwamba wanashindwa kuunganisha siasa zao na Uchumi. Na kama ingekuwa ni amri yangu mimi leo hii kila Mbunge angelazimika kuchukua economics japo kidogo kuelewa Principles maanake bado wabunge wengi wana Ulimbukeni na umaskini wa kiasili (Auafrika) wa kuvaa vizuri, gari kubwa wakati huna biashara kabisa isipokuwa kubangaiza na kutembea na bakuli la kuomba misaada..hawana biashara yoyote bungeni zaidi ya kuwa bunge ndio mtaji wa waisha yao wao. Ukiwaondoa bungeni watalalamika kwa nafsi zao na sii kupoteza uwakilishi na makusudio wa yale waliotaka kuyafanya ili kuboresha uchumi wa majimbo yao.


  Kibaya zaidi tunabishana ktk mambo ambayo yako wazi kabisa kuwa ni matumizi mabaya na hayapo ktk uzalishaji zaidi ya kujistarehesha sisi wenyewe hali kiuchumi hakuna kinachoongezeka. Ikiwa rais amefikia kusema swala la umeme ni kazi ya Mungu, unategemea vipi mtu huyo kuelewa umuhimu wa Umeme na maji ktk kukuza uchumi?. Na watu kama hawa huchanganya aya za Mwenyezi Mungu na kushindwa kutofautisha mamlaka ya Mwenyezi Mungu na ibada za mwanadamu, hivyo kufanya kufuru ya maamuzi yao binafsi kwa kisingizio cha Uwezo wa Mungu.

  Sisi waislaam tunasema hivi, Riziki hutolewa na Mungu kwa misingi kwamba Mwenyezi Mungu ndiye alopanda miti yote, akaweka mito, maziwa na mabonde yote na ndiye aliiwezesha nchi kuwa na maliasili na rasilimali zote zote hizi ni riziki za mwenyezi Mungu. Nguvu za umeme zinaweza kutokana na riziki alotupa Mwenyezi mungu iwe Upepo, maji, jua na kadhalika na hatuwezi kufikiria nje ya vitu alotupa yeye muweza, lakini unapopokea hizi riziki ni jukumu lako kufanya maamuzi yanayo kuwezesha kupata maisha bora ambayo ni ibada ya mwanadamu.

  Lakini unapokosa imani ktk maamuzi yako mwenyewe kujenga Dam kwa kutumia riziki ambayo mwenyezi Mungu kakupa (mito yenye maporomoko) ukashindwa kuifanyia ukarabati, ukashindwa kutazama jinsi ya kuboresha njia za mito hiyo kulingana na uzalishaji wa umeme zaidi badala yake akaanzisha kilimo kwanza pembenizoni mwa mito hiyo bila kujali maji yatapungua kwa kiasi gani wala huna mpango mwingine (plan B) kama maji yatapungua utawezesha nguvu zipi nyingine kuzaliwa umeme isipokuwa unafanya tu ili mradi ni siasa za kupendezeshana.

  Itakuwaje kiongozi mzima tena muumini wa kiislaam ufikie kumlalalimia Mungu maanake majibu ya JK kusema kweli kule BBC ilikuwa kana kwamba if you have a question in regards to electricity, well ask God! Hii ni kufuru kubwa na atanisamehe JK lakini kusema kweli alikwenda kinyume cha maadili ya dini na hata uongozi bora.


  Kwa hiyo mkuu wangu kubana matumizi kwa mtazamo wa Kitanzania hakika huwezi ku achieve kitu chochote isipokuwa ni Ufisadi kwa kwenda mbele maanake watu wanataka wabunge wasiendeshe mashangingi na posho zao zipungue ili fedha hizo zikajenge shule bora zaidi wakati hatuna walimu wa kutosha. Tukajenge Hospital wakati madawa feki yanatoka India na China au tunapambana na malaria kwa kugawa vyandarua hali nchi nzima (85% sasa hivi imefikia 90) ipo gizani na unajua mbu wanavyoshambulia kukiwa na kiza.
  Kwa hiyo malengo yetu kiuchumi ni kuuana zaidi, tunawezesha vifo zaidi ya kuboresha maisha ya wananchi. Yote haya yametokana na nchi kukosa dira...
   
Loading...