Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

KUTOKA KUKIITA CHUO CHA KATA BAADA YA UDOM KUKAZA MPAKA NAFASI YA PILI MMEBADILI MAADA TENA WATU NYIE MNGEJUA TULIVOTESEKA UDOM MSINGANDIKA HAYA MLIYOANDIKA
 
Shule ya IFM ndugu isikie tu hivyo hivyo. Ukiingia pale shile ikichanganya utaomba japo upige karai zako tu za kutosha usidakwe. Ile shule ukitoka pale huwa hata hakuna haja ya kuajiriwa
Kile chuo kimenitesa sana mkuu siwezi kukisahau daima japo now nipo sehemu nawashukuru sana kwa kifupi wapo vizuri.
 
Nina kila sababu ya kuheshimu wazo lako na sina data za kutosha kukupinga maana sijafanya utafiti huo, ila pengne nisaidie kidogo katika hili

1. Asilimia 85 ya walimu wanaofundisha UDOM ni wahitimu wa UDSM

2. Wakaguzi wa mitihani wanayofanya wanafunzi wa UDOM kutoka nje ni kutoka UDSM

3. Wasimamizi wa Chuo kwa maana ya uongozi wa chuo 95% ni wahitimu wa UDSM

Swali kwanini wahitimu hawa kutoka Chuo bora ambao ndio college mate wenzio ndo mazao yawe ovyo? Je tafsiri yake na wewe huduma unayotoa huko ni mbovu?

Ningeshawishika kukubali kama tu ungeonesha wahtim ndiyo wabovu pamoja na kutoka GPA ndogo lakini tuhuma yako ni walimu hawa kutoa GPA kubwa.
 
UDOM ikifanya vizuri inaonekana wanabebwa, ikifanya vibaya, wanaonekana wajinga, hamuoni mnakosa hoja jamani?

Binafsi hii inanipa ishara kuwa UDOM inafanya vizuri sana ndio maana baadhi ya vyuo vilivyodhani kuwa vitakuwa bora siku zote vinashangaa Nn kuchukia kuona kuna chuo kinakuja kwa kasi na hakika, hata miaka 5 haitapia, UDOM itakuwa ya 1 Tanzania na hata top 10 za Africa.
 
Kile chuo kimenitesa sana mkuu siwezi kukisahau daima japo now nipo sehemu nawashukuru sana kwa kifupi wapo vizuri.
Pale hakuna anaekubembeleza kuja chuo, kufanya presentation wala chochote. Wewe fanya ufyokolo wako ukitegemea kuna make up test uone utavyorudi kwenu
 
Wanapataje kazi kama sio competent? Na ni mwajiri gani huyo anataka watu ambao sio competent?
 
Nilipoona andiko la mtoa mada hapo juu imenilazimu nitafute kitabu cha orodha ya Graduate mwaka 2016 ambapo mimi ni miongoni mwa nilie-graduate mwaka huo nimetumia nusu saa kuangalia wenye FIRST CLASS kwa mwaka huo, lakini nikajikuta nacheka hadi kufikia kuidharau sana elimu ya Tanzania, kwamba kweli mtu anayejinasibisha kuwa na PTS 12 mara sijui ngapi huko anaweza akasema kama alichokisema na kibaya zaidi wachangiaji nao bila kufanya utafiti kabla hawajachangia pengine kujilizisha Kwa kile ambacho mtoa mada amekisema wameamua kuchangia uongo wa mtoto mada.

Jamani kama tunajinathibisha kuwa wasomi ni vizuri pia tukachangia vitu ambavyo tuna uhakika navyo kwa kufanya utafiti ama kujilizisha hapo tutakuwa tunaendana na sifa jadidi ya sisi kuuvaa uhusika wa usomi wetu.
 
Pale hakuna anaekubembeleza kuja chuo, kufanya presentation wala chochote. Wewe fanya ufyokolo wako ukitegemea kuna make up test uone utavyorudi kwenu
Tena ukimbie test ukitegemea utafanya special siku matokeo yakitoka unaona incomplete inaninginia
 
Tena ukimbie test ukitegemea utafanya special siku matokeo yakitoka unaona incomplete inaninginia
Wajomba wa pale hawanaga time na mtu, nyie mfeli hata darasa zima wao wanasonga tu. Hakuna cha kuuliza imekuwaje wala nini. Prof Mjema kama bado upo IFM, heshima kwako
 
Nathan Jr, No research no right to speak. Wewe ni msomi unajua hilo. Weka hapa data zako, au za mamlaka husika za jinsi UDOM ilivyo chini kielimu, kuanzia ufaulu kila mwaka, incompetency ya product hao wakiwa kazini (walioshindwa na kfukuzwa), halafu Fanya comparison na vyuo ulivyitaja.

Kwa wachangiaji wengine kumbukeni critical thinking ndio tool ya hoja.
 
Nilivyokuwa UDOM kipindi hicho nilikuwa na rafiki yangu mmoja raia wa Gabon alikuwa anasomea masuala ya fedha pale chuoni yule jamaa kitu kimojawapo ambacho alikuwa anatushangaa Watanzania ni kuwa watu tusiopenda kufanya utafiti kwa kila kitu tunachotaka kukisema ama kwa kukifanya, kwa maana kwamba kabla hatujachangia tujisumbue kidogo kwa kufanya utafiti ili kile unachochangia kiwe ni kile ambacho ni sahihi. Mimi niseme tu kwamba najivunia kusoma UDOM
 
Mkuu umenikumbusha Chuo cha Teophil Kisanji, kwa staili hii vyuo vya private vitapiga hela balaa.
Mkuu kama watu wamefaulu na kupata maGPA ya ajabu basi haina haja ya kupinga, kama vipi tubadilishe mfumo wa mitihani ya vyuo vikuu.
 
Wajomba wa pale hawanaga time na mtu, nyie mfeli hata darasa zima wao wanasonga tu. Hakuna cha kuuliza imekuwaje wala nini. Prof Mjema kama bado upo IFM, heshima kwako
Waliosoma IFM wakitoka pale wameiva, sikisifii ila ukweli ni huo tu wanakwambia wanatoa competent students
 
Back
Top Bottom