Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Walimu wote Wana kasumba ya kufanana aisee high marks hutolewa kwa wachache kwa kujuana. So wengi hutoa b plain na makarai kwa wingi walah
Taratibu za kuappeal zipo au hazipo? Na je utaratibu ukoje? Mimi nina experience ya tofauti sana katika hili. Labda kama mwanafunzi mwenyewe awe hafahamu taratibu hii
 
Tuzingatie na ukubwa wa chuo na idadi ya wanafunzi inaowadahili kila mwaka kujiunga na course husika pia
 
kumbe wewe u
Ukihudhuria maafari Yao vyuo Tajwa hapo juu
UDSM, IFM, SUA, MZUMBE Si rahisi kusikia wanatangaza wanafunzi wenye first class wengi, utakuta wanne au watano hawazid kumi mara nyingi. Lakini ukienda UDOM utakuta first class wapo 70. Sababu nini? UDSM na IFM hawana walimu competent kama UDOM au?
Kumbe wewe umehudhuria mahafali na sio masomo? Ulizia kwanza selection za masomo wanaanza first class wachaguliwa kwenda Chuo gani? UDOM hawapo labda Education kama Chang'ombe (DUCE)
Kuna maajabu yalitokea eti form 4 wakaenda UDOM badala ya TTC kama sio Mh Ndalichako na Rais wetu tulishaharibikiwa na mfumo wa elimu
 
Unaongea tu bila facts zozote, ukweli ni kwamba kumekuwa na MYTH kuhusu ubora wa Chuo Kikuu cha Dodoma, kwanza walianza na myth ya kwamba kwanini chuo kikubwa kama kile kikajengwe jangwani, baadae wakaja na kile chuo hakina walimu, mara kinadahili wanafunzi wasio na sifa, leo hii baada ya miaka 10 product za UDOM zmeanza kukubalika mtaani mmeanza kukipiga majungu kwamba kinatoa GPA za upendeleo.

But in real sense hakuna aliyefanya thorough investigations kupata ukweli wa haya yote. Pia wanaosoma pale ni wenzetu ambao tumesoma nao na wengi wao pengine walikuwa wanatuzidi uwezo darasani. Mimi nina mfano wa faculty moja hapo UDOM kuna mwaka walidahiliwa wanafunzi waliopata division 1 & 2 tu, lakini ni mmoja tu ndo alimaliza na first class wengine wote waliambulia GPA za kuokoteza, sasa sijajua hizo GPA first class za kumwaga wewe umezitoa wapi hizo data.
 
Kibongo u-appeal nani ana huo mda kazi zinazokuwaga fair ni zile za kwa external tu the rest vile vile.
Mkuu taratibu zipo na zinashughulikiwa. Nadhani issue ni uelewa wa taratibu hizi
 
Huyu aliyewaambukiza watoto wa kizazi hiki ugonjwa wa GPA na kuhusudu majina ya vyuo kaharibu sana maana ya elimu ya juu. Ukivikuta huko vimekaa vichwani hamna kitu, vilivyopo kazini tija hakuna vinatambiana GPA na vyuo vilivyosoma, kama haka hapa hata neno MAHAFALI hakawezi kuandika ila kana ujuzi wa kupima ubora wa elimu inayotolewa na taasisi za elimu ya juu.

Kengine kamekuja juzi ofisini kwa ajili ya mchakato fulani kwenye vyeti vyake (kahitimu ka St. nini sijui huko maana vyuo vingi siku hizi) na ki CV chake kimeandikwa lugha isiyofahamika (inafanana na Kiingereza). Hiyo barua ndio balaa!! Makaratasi yake yameandikwa ana GPA ya 4.1. Katika story eti kananiuliza bro GPA (yangu) inasoma lakini!? Nikacheka then nikaiba muda wangu mwenyewe nikakafanyia counselling ya kina kidogo.
 
Bongo tunahusudu GPA kuliko utendaji kazi na ubunifu

Issue sio uelewa hyo inajulikana wahadhiri huteteana sana nikikumbuka jinsi mdada alivyopata disco kisa mambo ya ngono wakamtetea mhadhiri
Mkuu taratibu zipo na zinashughulikiwa. Nadhani issue ni uelewa wa taratibu hizi
 
cariha, Believe me ninapokwambia utaratibu upo. Appeals haziishii idarani wala Colleges taratibu zipo. Hayo mambo labda useme yalikuwepo zamani but now haki inatendeka hasa baada ya kujua nguvu ya media.
 
Samahani kusema hivi mleta mada ni mshabiki wa elimu zwazwa, haijawahi kutokea UDOM kukawa na 1st class zaidi ya 10 kwa kitivo kimoja sasa hizo sabini ulikaa na chuo kuzipitisha?

Halafu kumbuka Udom ni chuo cha taifa kitakachosomwa na vizazi kwa vizazi hapo mbeleni hivi kwanini usijonee fahari kama Mtanzania uwepo wa chuo kama hicho

Fikra za kimasikini ni kutojali vya kwenu
 
Back
Top Bottom