Ni pesa, lakini zinaitwa kwa majina mengi...

Ni pesa, lakini zinaitwa kwa majina mengi...

Kijana Style

Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
37
Reaction score
10
Pesa ni pesa lakini hizi pesa zina majina mengi,kwa mfano ukijaribu kuzitaja kwa jina lake [Pesa] katika mambo mengine ambayo ni muhimu kijamii kama vile kufunga ndoa huwezi kuwaambia wazazi wa bibi harusi ntawapa PESA munipe binti yenu,hiyo haitakuwa lugha ya kiheshima, kwahivyo hapo ndipo hizo pesa zikaitwa MAHARI.
Hebu sasa tuangalie ni majina gani hizi pesa zinaitwa katika mambo mbalimbali;
kama tulivyoandika hapo juu

Katika kuowa mke -
MAHARI

Ukifanya kazi unalipwa -
MSHAHARA

Ukimkopesha mtu unaziita -
DENI

Mtu akistaafu kazi kwa uzee -
PENSHENI

Kwa serikali kila mtu analipa -
KODI {tax}

Mahakamani unalipishwa -
FAINI

Ukimpatia Ofisa ili akusaidie -
HONGO

Unaposaidia Wanavijiji -
MCHANGO

Unapoomba kutoka Banki -
MKOPO

Siku njema kwenu wote,
Kijana Style.
icon6.png
 
Kanisani zinaitwa sadaka.
Shuleni zinaitwa ada
 
kwenye ujenzi nk zaitwa gharama,baa zaitwa bili,kadhalika tanesco, vyuo vikuu zaitwa boom,vibaruan ujira,rushwa halali zaitwa takrima
 
kwenye burudani unatoa KIINGILIO.
Lakini fanya ufanyavyo, hayo yote ni MALIPO.
 
Pesa ni pesa lakini hizi pesa zina majina mengi,kwa mfano ukijaribu kuzitaja kwa jina lake [Pesa] katika mambo mengine ambayo ni muhimu kijamii kama vile kufunga ndoa huwezi kuwaambia wazazi wa bibi harusi ntawapa PESA munipe binti yenu,hiyo haitakuwa lugha ya kiheshima, kwahivyo hapo ndipo hizo pesa zikaitwa MAHARI.
Hebu sasa tuangalie ni majina gani hizi pesa zinaitwa katika mambo mbalimbali;
kama tulivyoandika hapo juu

Katika kuowa mke -
MAHARI

Ukifanya kazi unalipwa -
MSHAHARA

Ukimkopesha mtu unaziita -
DENI

Mtu akistaafu kazi kwa uzee -
PENSHENI

Kwa serikali kila mtu analipa -
KODI {tax}

Mahakamani unalipishwa -
FAINI

Ukimpatia Ofisa ili akusaidie -
HONGO

Unaposaidia Wanavijiji -
MCHANGO

Unapoomba kutoka Banki -
MKOPO

Siku njema kwenu wote,
Kijana Style.
icon6.png

Nimeipenda hii hahahaaa imetulia mkubwa
 
Kwenye vikao vya wale wanaotaka kuheshimiwa kwa lazima wakati mambo yao ni hovyo - POSHO

Kwenye mipango inaitwa - BAJETI

Kwenye makusanyo ya serikali - MADUHULI

Kwenye biashara - USHURU

Kuanzisha biashara - MTAJI

Kwenye hisa inaitwa - GAWIO

Ukienda NHC mwisho wa mwezi - PANGO

Taarifa rasmi ya uchumba - POSA

Ila sijui ni wakati gani inaitwa PESA na wakati gani inaitwa FEDHA na wakati gani inaitwa HELA
 
Ktk biashara ya ujanja tunaita "CHA JUU"
 
Kwa matumizi ya chenge billion-vijisenti
 
Back
Top Bottom