Ni Paka kweli au jini?

Boflo

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
4,384
4,409
Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani
 
Sali tu nakila kitu kitakua shwari...ukiendekeza tu hizo imani utasumbuka sana,muombe mungu atakusaidia.
 
imani potofu hzo! Mwamin mungu wako hakutakuwa na cha kukutisha ktk hii dunia. Sali sana ndg yng.
 
akilia tena mwambie hapo ni dirishani, apitie mlangoni aingie ndani akae kwenye sofa badala ya kupigwa na baridi nje ya dirisha!!

Kama akiendelea kulia mwambie aendelee kukuimbia tenzi za rohoni wakati ww unaupiga usingizi!!!!
 
wakuu kuweni serious haya mambo yapo sana kwenye jamii yetu...jambo zuri ni kusali tu tena kwa imani..
 
Ni kiumbe cha mwenyezi mungu tu huyo..usipate hofu yuko katika 'heat' anatafuta mwenza ndio sababu ya makelele hayo...si unajua wao hawahongi kukidhi haja?
 
akilia tena mwambie hapo ni dirishani, apitie mlangoni aingie ndani akae kwenye sofa badala ya kupigwa na baridi nje ya dirisha!!

Kama akiendelea kulia mwambie aendelee kukuimbia tenzi za rohoni wakati ww unaupiga usingizi!!!!

safi sana!!
 
Huyo ni paka wa kawaida tu hawezi kukudhuru kimwili - utakapolikubali hilo madhara ya kisaikolojia yatakwisha na utalala kwa amani.
 
akilia tena mwambie hapo ni dirishani, apitie mlangoni aingie ndani akae kwenye sofa badala ya kupigwa na baridi nje ya dirisha!!

Kama akiendelea kulia mwambie aendelee kukuimbia tenzi za rohoni wakati ww unaupiga usingizi!!!!

na jee baada ya kusema hivyo,akiingia ndani na akaa kwenye sofa,si utatetemeka?
 
Atakuwa paka jike yupo kwenye heat na hana paka dume wa kumshuhulikia. Tfuta paka dume ikifika mida hiyo mtoe nnje. watamalizana then hutamsikia tena akipiga myau miau dirishani kwako.

Akirudi tena baada ya kushughulikiwa na dume basi sali sana na umwagie dirisha lako maji ya baraka au chumvi yanapatikana kanisani.
 
sali na soma neno kisha acha hiyo bible wazi iweke mkabala na dirisha.kama jini atatoweka asipotoweka huyo ni paka pori tu wa kawaida amenusa harufu ya kitoweo ulichohifadhi ndani mwako
 
yupo kweye hot period, anatafuta bwana!!. we akilia mnyatie umtoe balu, hata rudi tena hapo atajua ni hatari.
 
Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani

Nimaeneo gani mkuu? Kama huna muda mrefu check na darali wako atakuwa alikuwa anajua. Mie nakushauri komaa, maana hata mie nina jamaa yangu ilikuwa inamtokea hivo baada ya kuulizia akaambiwa vimbwanga hivyo vinafanywa na mwenye nyumba lengo ni kuwa ukimbie ili apate kupangisha mtu mwingine, kwahiyo ilikuwa ndio mtindo wa mwenye nyumba wake jamaa alikomaa mpaka akamaliza kodi yake kisha akahama hiyo nyumba
 
Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani

Huyu ni paka tu wala si jini. Vyovyote itakavyokuwa, wewe kitakachokusaidia ni kusali tu kwani unaweza kulikimbia jiji? Sala zako ndo zitalitupilia mbali
 
issue ndogo,weka birika la umeme chumbani kwako,ikifika time yake,chemsha maji ya kutosha,andaa mazingira,ukimuona tu,wewe usizungumze kitu,kimya kimya mwagia maji ya moto.kama ni jini jibu utalipata hapo hapo,kama ni mchawi its the same ,na kama ni paka wa ukweli utajua tu.
kusali ni moja ya tiba za mauzauza,ila je unao usafi wa kutosha kukemea haya mapepo.kwangu nilikuwa na hilo tatizo,manati tu ilitosha kutoa solution.
Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani
 
Wadau leo ni siku ya 3 mfululizo kila inapofika mida kama tisa ya usiku, katika dirisha ninalolala huwa anakuja paka na kuanza kulia kwa milio ya ajabu sana, sauti huwa anaibadilisha badilisha, inakuwa kama ya mtu mzima mara kama ya mtoto na ya ajabu,.

Kuna jamaa 1 nimemuuliza akaniambia huyo si paka ni jini...wadau eti kuna ukweli wowote? Na nichukue hatua gani

Siyo jini huyo ni binadamu alivaa umbo la paka, kawaida ulozi hufanyika kuanzia saa sita hadi saa tisa usiku, ukisikia paka analia dirishani kwako jua kuwa alijaribu kuingia chumbani tangu saa sita akashindwa, hivyo anaishia kutoa sauti ya vitisho.

Dawa yake ni kumzomea, mwambie achukue ufagio afangie uwanja, ukiamka asubuhi usikute uchafu.
 
Back
Top Bottom