Ni nini tofauti kati ya kuona, kutazama na kuangalia?

Mmeme

JF-Expert Member
Nov 25, 2017
700
299
Kiswahili kina ugumu wake. Nashindwa kutofautisha kati ya "Ona", "tazama" na "angalia".

Je, ni wakati gani natakiwa nitumie neno lipi katika matumizi sahihi ya kiswahili?

Naomba kujua matumizi yake sahihi.
 
Tazama- kuangalia kitu Kwa umakini(chunguza) zaidi Ili kupata taarifa za ziada. Mfano mgonjwa, bidhaa unayotaka kununua sokoni,

Ona- kuangalia Kwa kutozingatia zaidi na bila umakini wowote. Mfano watu na vitu vyoote vilivyo mbele ya macho Yako.

Angalia - kutazama Kwa vipindi, Kuna wakati utatilia umakini na wakati mwingine unapuuza. Mfano mpira wa miguu, sinema, movie n.k
 
Tazama- kuangalia kitu Kwa umakini(chunguza) zaidi Ili kupata taarifa za ziada. Mfano mgonjwa, bidhaa unayotaka kununua sokoni,

Ona- kuangalia Kwa kutozingatia zaidi na bila umakini wowote. Mfano watu na vitu vyoote vilivyo mbele ya macho Yako.

Angalia - kutazama Kwa vipindi, Kuna wakati utatilia umakini na wakati mwingine unapuuza. Mgmfano mpira wa miguu, sinema, movie n.k
Ninaposikia sauti ya ndege angani na kuthibitisha kuwa ndege ile inapita.

Je, japo nakuwa natazama, naona au naamgalia ndege?
 
1. kuona-See.
2. tazama-Look at.
3.Angalia-watching.
Sometimes maana ya kiswahili unaipata vizuri ukitafsiri kutoka katika kiingereza kuja katuka kiswahili
 
1. kuona-See.
2. tazama-Look at.
3.Angalia-watching.
Sometimes maana ya kiswahili unaipata vizuri ukitafsiri kutoka katika kiingereza kuja katuka kiswahili
Nimekuelewa vizuri, asante sana. Lugha ya kukopa imeeleza vizuri sana.
 
Back
Top Bottom