Wadau,
Miaka ya karibuni serikali imeanza tena kupeleka wanafunzi wa kidato cha sita kupata mafunzo ya kijeshi, kama ilivyokuwa enzi za mwalimu. Hoja yangu ni kuwa kwanza ni nini kilichofanya huu mfumo usitishwe hapo awali ili sasa hivi urudishwe?
Nini faida yake ukilinganisha na gharama zinazotumika kutoa mafunzo hayo? Kama ni kujenga uzalendo kama wengi wanavyodai mbona hatuuoni huo uzalendo kwa viongozi wetu wengi waliotutangulia amabao wengi wao walipitia kwenye huo mfumo? Kwa sababu sio wote wanapata hayo mafunzo ina maana ambao hawajapata nafasi hawatakuwa wazalendo? Vipi wale wanaoenda kusoma certificate baada ya form four wakiajiriwa watakuwa sio wazalendo?
Juzi rais amesema vijana wanachapa kazi na sio mafisadi Je hao vijana walipitia jeshini? Kulipa gharama za kumpeleka jeshini mwanafunzi na baadae kushindwa kumlipia mkopo wa chuo kipi kilihitajika kuwa cha muhimu elimu au ukakamavu?
Hela zile zingepelekwa kwenye fungu la vijana kujiajiri serikali haioni ingekuwa na maana kubwa kuliko hayo mafunzo.
Je, serikali haioni itahatarisha usalama wa raia kuwapa watu mafunzo, mpaka kutumia bunduki alafu baada ya hapo hakuna ajira, hawaoni vijana wataingia kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani maana wana ujuzi?
Ombi langu ni serikali iangalie vipaumbele vyake upya haiwezekana mabilioni yapelekwe kwenye vitu visivyo na ulazima kama daraja la Kigamboni na mwenge wakati kuna vijana wamemaliza chuo wanahitaji tu mtaji waweze kujiajiri na kuleta maendeleo kwa taifa.