trachomatis
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 3,758
- 736
Kwamba alikuwa daktari wa binadamu,na pili alipata kumtibia Malkia Elizabeth kwa kigezo kuwa ndiye Daktari mwenye kiwango cha juu kwa kipindi hicho,na kuongezea hapo kwa sharti kwamba ahasiwe?
Habari ni hii,
Kwanza, hakuwahi kuwa daktari wa Malkia wa Uingereza japo alikuwa daktari mzuri sana huko Uningereza. Pili, uraisi wa maisha alipewa na waMalawi wenyewe mwaka 1970. Tatu, jamaa kumbe hakua hasi (dunye) hata kidogo, alikuwa anakula kisirisiri na hata kuzaa watoto...
Mnamo mwaka 1951, wakati Hastings an-practice udaktari huko Uingereza alizaa na receptionist wake ambaye pia alikuwa ni mke wa rafiki yake (inaonekana alisababisha mpaka waka-divorce), huyo mama alikuwa anaitwa Mrs. Marene French, Kamuzu alikataa katakata mtoto na mama!
Na hivi juzi juzi tena ameibuka jamaa anayedai kuwa ni mtoto wake, huyu jamaa alifanya DNA testing na ikaonekana kuwa ni kweli Hastings Kamuzu Banda ni mzazi wake lakini ndugu za banda ambao ndio wanamiliki utajiri aliouacha wamegoma kukubali...
Huyu jamaa (mtoto wake) jina lake ni Jumani Johansson au Jim Jumani Immanuel Masauko Kamuzu Banda ana uraia wa Sweden anakoishi na baba wa kufikia lakini pia ana passport ya Malawi....
Nielimisheni pia kuhusu sababu ya hii notion kuenea kwamba alihasiwa.Ilikuwa ni kumtafutia umaarufu,au kuondoa mashaka kwa wanaomzunguka kutokana na masuala fulani ya kibinafsi?
Kuna taarifa vilevile kuwa Kamuzu Banda aliyetoka Malawi miaka ile ya awali siye yule aliyerudi kuja kutawala Malawi wakati wa uhuru. Inaonekana waingereza walibwatapeli wa Malawi. Ushahidi wa hilo unatokana na kwamba Kamuzu hana ndugu wa kikweli
je hayo mambo yalifanyika lini? Sababu banda ana mtoto nafikiri anaishi Afrika Kusini. Au alihasiwa baada ya kuwa na mtoto?.