Jinsia zote mbili zina matatizo na matamanio yasiyo na mipaka. Hakuna kinachomridhisha mwanadamu na akaganda nacho mwanzo wa uhai wake hata mwisho. Binadamu ni mtu wa adventures bila kujali ubaya na uzuri wake. Ila kwa kuwa tuna akili na dhamira, mambo mengine tunayaonea haya, na wakati mwingine tunayafanya kwa uficho ili walimwengu wasitubaini.
Sijui kama kuna mtu ambaye yuko kwenye mapenzi kapata chaguo lake kwa asilimia mia kama alivyotaka iwe. Hakuna. Hapo ndio mwanzo wa matatizo. Kupewa mahitaji yote ya kibinadamu sio tiketi ya kumpenda mtu. Mwanamke anahitaji ulinzi. Sio ulinzi kama wa Ultimate security. Ulinzi wa kihisia, kimali, kimwili, n.k. Ulinzi wa kiroho atatoa Mungu. Mwanaume mmoja kutimiza yote hayo ni ngumu sana. Wapo ambao watakosa baadhi ya mambo fulani na watatulia kwa kuwa hawana jinsi. Wapo wanaotaka kila kitu na ndio maana unashangaa mwanamke anachapwa nje ya mahusiano.
La msingi ni ni kukubali kuwa si kila kitu unaweza kupata. Pia si kila kitu mwenza wako anaweza kukupatia. Gharama ya kupata hicho ulichokosa yaweza kuwa kubwa kuliko gharama ya kutokuwa nacho. Ni hayo tu
Umenikumbusha kisa kimoja: Jamaa alimfumania mkewe live kitandani. Akaamua kumuua mkewe. Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo badala ya kumuua mbaya wake alijibu " Niliogopa kuendelea kuua wanaume kila baada ya siku chache!!". Baadhi ya wanawake hata wasuguliwe kisawasawa bila mapumziko watatoka nje. Kwao mumewe na wanaume wengine wa nje hawana tofauti na katika harakati zao hizo wanaweza kupambana na wanaume ambao hawana uwezo wa kusex kama walionao waume zao. Lakini hata wanawake watakuambia nao wanaume wako hivyo na zaidi.
Watu hawafanani..hivyo wanawake hawafanani!Ndo maana kuna ambao bila pesa hawezi kua na wewe ila sura..umbo na tabia hajali n.k.Situation ulizotaja hapo juu zinaweza kua ideal kwa baadhi ya wanawake ila sio wote!Ukirejea kwenye hizo story inawezekana kabisa aina ya mwanamke unayemwongelea hawezi kuappreciate anayofanyiwa bali anatumia huo kama udhaifu wa mumewe hivyo anautumia kikamilifu..au labda ana tabia tu ya kurandaranda..au labda hajaridhika!Kama kuna muhusika kweli ni vizuri akaulizwa yey
Mi naona Hulka na tabia ya mtu tu.
Kama mtu unafanyiwa kila kitu, na mume wako, kinachokupeleka nje sio, shida wala tamaa ya pesa.
Ni mwili wako tu, na tamaa za mwili wako uko hivyo.
Kwa mtoto wa kike, ni mbaya sana kufumaniwa na mume wako zaidi ya mara mbili halafu unaomba msamaha,
unasamehewa unarudia tena na tena.
Hata kama huridhiki namna gani, kwa mwanamke kutoka nje tena waziwazi namna hiyo ni mbaya, mi naona utakuwa humpendi huyo mume,
labda unaishi naye kwa tamaa ya vitu vyake tu.
Kwanza Biblia inasema Mwanamke ni mlinzi wa Mume wake, yeye ndo anatakiwa akae amuombee Mume wake asivutwe na makahaba,
kwa sababu wanaume wao huvutwa kwa kuona. Yeye ndo anatakiwa atengeneze mazingira ya kumsaidia mume wake, asishawishike na vibinti huko barabarani. Halafu tena mwanamke wewe ndo unakuwa wa kwanza kufanya huo uasi. Binafsi naona haipendezi kabisa.
Sina maana kwamba wanaume wafanye hivo hapana, lakini mwanamke amepewa nafasi ya pekee ktk kumtunza na kumlinda mume wake.
Kama humpendi ndo utamfanyia hayo mambo ya ajabu hivyo. Wanawake wamepewa Roho ya kuvumilia na kusamehe uovu wa waume zao kuliko hata wanaume. Sasa iweje mwanaume ndiyo awe na roho ya kuvumilia na kusamahe kwa kiasi kikubwa kuliko mwanamke?
Haijalishi huridhiki namna gani, njia ya kutatua tatizo lako sio kuruka ruka na huku unataka ubaki kwa mume wako.
Kama unaona hakuridhishi mwambie, halafu uamue kumuachia baba wa watu uhuru ili ukatafute hicho unachokitaka,
kwa uhuru zaidi.
mahusiano yanajumuisha mambo mengi,huwezi kutazama upande mmoja na kuutolea majibu.kinachoniridhisha mie kwenye mapenzi sio lazima kiwe kinafanana cha mwingine.
lakini kutokana na maelezo yako kama ni kweli huyu dada anafanyiwa yote hayo na bado anatoka nje ya ndoa yake atakuwa na matatizo ambayo sijui kama ataweza kutulia kwenye relationship yoyote ile,
tunapokuwa kwenye mahusiano hatutegemei kukutana na malaika,au kuchukua mapungufu yetu na kuyaweka kichwani pa wengine ili tukamilike ndio maana kuna neno uvumilivu la sivo utakuwa na mahusiano mapya kila siku.
nachoona huyu dada anatafuta mkamilifu ambaye hayupo na wala hatakaa atokee,anaendelea kujiongezea list ya watu wataompa stress zaidi za maisha .
nina maswali kwa dada ,kama alitoka mara moja hakuna jambo alilojifunza kwa kufanya ivo na je alipoanzisha uhusiano mwingine hakujiuliza maswali, lilimtoa kwa mumewe na kwenda kwa huyu mwanaume wa nje na bado wameachana na sasa ana mwingine.
kwangu huyu dada namuona kama !!!!..........nilikuwa niseme vibaya lakini ndo ukweli.
Mi naona Hulka na tabia ya mtu tu.
Kama mtu unafanyiwa kila kitu, na mume wako, kinachokupeleka nje sio, shida wala tamaa ya pesa.
Ni mwili wako tu, na tamaa za mwili wako uko hivyo.
Kwa mtoto wa kike, ni mbaya sana kufumaniwa na mume wako zaidi ya mara mbili halafu unaomba msamaha,
unasamehewa unarudia tena na tena.
Hata kama huridhiki namna gani, kwa mwanamke kutoka nje tena waziwazi namna hiyo ni mbaya, mi naona utakuwa humpendi huyo mume,
labda unaishi naye kwa tamaa ya vitu vyake tu.
Kwanza Biblia inasema Mwanamke ni mlinzi wa Mume wake, yeye ndo anatakiwa akae amuombee Mume wake asivutwe na makahaba,
kwa sababu wanaume wao huvutwa kwa kuona. Yeye ndo anatakiwa atengeneze mazingira ya kumsaidia mume wake, asishawishike na vibinti huko barabarani. Halafu tena mwanamke wewe ndo unakuwa wa kwanza kufanya huo uasi. Binafsi naona haipendezi kabisa.
Sina maana kwamba wanaume wafanye hivo hapana, lakini mwanamke amepewa nafasi ya pekee ktk kumtunza na kumlinda mume wake.
Kama humpendi ndo utamfanyia hayo mambo ya ajabu hivyo. Wanawake wamepewa Roho ya kuvumilia na kusamehe uovu wa waume zao kuliko hata wanaume. Sasa iweje mwanaume ndiyo awe na roho ya kuvumilia na kusamahe kwa kiasi kikubwa kuliko mwanamke?
Haijalishi huridhiki namna gani, njia ya kutatua tatizo lako sio kuruka ruka na huku unataka ubaki kwa mume wako.
Kama unaona hakuridhishi mwambie, halafu uamue kumuachia baba wa watu uhuru ili ukatafute hicho unachokitaka,
kwa uhuru zaidi.
Hii point yako no. 6 sita hainisaidii chochote kama hutaki kuniheshimu na kuona utu wangu uko wapi. Heshima iko wapi hapo, kunisikiliza katika maamuzi iko wapi hapo??? Na huwezi kunipa kila kitu bana
LD ningekuwa single ninge ku-PM! Napenda mtazamo wako!!
No. 6:
6. Mumeo huyo, anakuonyesha mapenzi makubwa usiku na mchana, anakutunza, anakupa kila kitu utakacho, anakupa pesa zozote unazohitaji na kukupeleka popote utakapo nakuridhisha kwa mahitaji yako yote ya kimapenzi, kimwili, kihali na kimali lakini bado hutulii wewe na wanaume tu.
Ni nini hasa Mwanamke anahitaji kutoka kwa Mwanamume na katika Maisha yake?
Assume:
1. Ni binti Mrembo wa asili wazazi wako ni watu makini, waelewa, wasomi na wanaoheshimika sana katika jamii na wamekulea vema, ukapata mume makini anayejiheshimu na mwenye upendo wa kweli akakuoa - Hutaki kutulia macho juu juu, memeo akagundua nyendo zako na kukukanya, ukaomba msamaha akakusamehe maisha yakaendelea.
2. Ulikuwa huna kazi, mumeo akakukabidhi kampuni uiendeshe, ukaifanya kampuni kijiwe cha mashoga zako na mawasiliano na wanaume zako na kisha kutafuna mapato ya kampuni, mumeo akakuondoa kukunusuru wewe na kampuni. Ukakusamehe makosa yako maisha yakaendelea.
3. Mumeo kwa upendo ili usiwe bored akakutafutia kazi nzuri na makini ya kuheshimika, ukaanza kufanya kazi lakini kiwango chako cha utendaji kikawa chini na pia bado unajihusisha na wanaume nje ya ndoa. Mumeo akagundua, kakukanya tena ukaomba msamaha. Mwajiri akaamua kukuondoa kazini kwa kuwa kazi huwezi.
4. Mumeo akaamua kukutafutia mtaji mkubwa ufanye biashara zako, ukatumia bado nafasi hiyo kuendeleza mambo yako na wanaume.
5. Bado mumeo kakununulia gari na unaweza kutumia magari mengine yaliyopo nyumbani, lakini bado huonekani kuridhika.
6. Mumeo huyo, anakuonyesha mapenzi makubwa usiku na mchana, anakutunza, anakupa kila kitu utakacho, anakupa pesa zozote unazohitaji na kukupeleka popote utakapo nakuridhisha kwa mahitaji yako yote ya kimapenzi, kimwili, kihali na kimali lakini bado hutulii wewe na wanaume tu.
7. Elimu yako ilikuwa ya chini akakuendeleza kufikia level ya Chuo Kikuu (Degree), lakini bado wewe na wanaume tu kila kukicha.
8. Mumeo kwa upendo hakutaka mambo yako yajulikane nje hata hivyo mara kadhaa katumia rafiki yake wa familia wa karibu sana kukuonya ili ujirekebishe, kila wakati unaomba msamaha utaacha na kujirekebisha lakini huachi. Anajitahidi kukuchukua mara kwa mara mkapime HIV ili kujinusuru na kukufanya uwe makini lakini somo halieleweki.
9. Mumeo anakuchukua nje ya nchi mahali kwa likizo muwe wawili tu mpate kudumisha mapenzi na kurelax, lakini muda mwingi wewe unautumia kupiga simu kuongea na wanaaume wako na SMS kibao.
10. Hatimaye mume wako anaamua kukufuatilia ajue ni nini shida yako hasa, anagundua miaka yote mliyopo katika ndoa umekuwa na mahusiano na wanaume wengine na kibaya zaidi ni kuwa si moja tu bali ni zaidi ya watatu. Ili kusikia kauli yako kama ni kweli unafanya hayo mambo safari hii anamuhusisha mama yako mzazi ambaye ndoyo tegemeo la mwisho la kwako, unakubali mbele ya mama na mumeo kuwa ni kweli hayo mambo umekuwa ukiyafanya na kutahayari kuonyesha kuchanganyikiwa na sasa mume umeamua "Kujiweka Pembeni, kuepusha msongamano".
Lakini bado hili jambo linaaacha maswali mengi moja wapo ni hili: NI NINI HASA MWANAMKE ANAHITAJI KUTOKA KWA MWANAUME NA KATIKA MAISHA YAKE?
Refer No. 6. inasema:
6. Mumeo huyo, anakuonyesha mapenzi makubwa usiku na mchana, anakutunza, anakupa kila kitu utakacho, anakupa pesa zozote unazohitaji na kukupeleka popote utakapo nakuridhisha kwa mahitaji yako yote ya kimapenzi, kimwili, kihali na kimali lakini bado hutulii wewe na wanaume tu.
Kunipa kila kitu sio sababu hata unifanyie birthday kwenye ndege sitaridhika.
Mwanamke anahitaji:
Kupendwa hata kama yeye hapendi (kubali kataa lakini hiyo ndo hali)
Kudekezwa
Kubembelezwa hata kama amekosea yeye
Kuombwa samahani
Kuambiwa nakupenda sweet, baby na mengine
Kufanyiwa kila kitu na kuonyeshwa
Kujaliwa sana
Sita kwa sita pia imo
nk
Jamani tusikimbilie kuwafanyia vitu bila kuonyesha unajali, unampenda, unamuheshimu hasa katika maamuzi ndani ya nyumba,
Ndoa au mahusiano ni zaidi ya pesa za kunifungulia miradi na kunitafutia kazi.
Tunahitaji attention kubwa kutoka kwenu nyie wanaume kunipa magari na mabiashara yako si mali kitu kabisa bila kunijali.
Nitarudi
Ukweli ni kwamba complete satisfaction is impossible.
Bali kwa hofu ya kumkasirisha Mungu ndio inawezekana kuzuia tamaa zisizo za msingi kwa wanadamu
Inasikitisha mhh