Gobole Lenye Risasi
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 11,477
- 23,574
Alhamisi iliyopita nilikuwa Kariakoo mtaa fulani hivi maarufu kwa kuuza matairi.Nilifika mpaka kwenye duka la jamaa yangu anauza Rims na Tyres from Japan.
Nikiwa naongea naye mara akaja bwana mmoja akiwa na mteja akimshawishi kumuuzia tyre.Mteja alionekana kuchoka na ushawishi wa yuke bwana maana alikuwa analazimisha amuuzie tyres za size tofauti.
Alipoondoka ndio yule jamaa yangu akaniuliza. Unamjua Mackmogan? Nilimjibu hapana.Akaniuliza kama nimewahi usikia wimbo wa Ali Kiba Mackmogan. Hapo nikataka kujua wimbo huo una mahusiano gani na huyo bwana, ndo kunisimulia.
"***** (Akitaja jina lake) alikuwa na pesa huyu mshkaji acha. Huyu bwana alifanikiwa kuuza nyumba ya urithi na ndugu zake hapa Kariakoo wakagawana yeye akapata mil 600. Jamaa alianza kuponda maisha ile kinyama, mademu alikuwa anawapanga tu hotel kali kali.
Jamaa alikuwa akikamua anahonga mpaka millions kadhaa. Alitembea mpaka South Africa kwenda kula maisha. Jamaa alitumia pesa zote mpaka kumaliza ndio karudi hana hata pa kukaa. Ilifikia kipindi anatembea na nguo kwenye mfuko kambi popote amechoka hana kitu kwa sasa. Ndo anakuwa kama dalali wa matairi akiongezea akapata 2000 au 5000 ndo maisha yanasonga.Huyu ndo aliimbwa na Ali Kiba Mackmogan"
Jamaa alimaliza huku akimtizama Mackmogan kwa mbali anatembea akisukuma gurudumu la gari.
Najiuliza hizi habari nani mwingine anazifahamu? Je, ni nini hasa kilimpata huyu jamaa maana hili jambo limekuwa likinisikitisha kila napolikumbuka.