Mkongwe Mzoefu
JF-Expert Member
- Aug 10, 2018
- 842
- 2,467
Wakati umefika sasa tuwe tunawajua watu kwa majina pale wanapotumia ofisi za umma kihuni na kutesa watu bila huruma kwa kisingizio cha sheria.
Suala la vijana viongozi wa BAVICHA (Nusrat na Mwaipaya) waliowekwa ndani Singida na ofisi ya DPP kuamua kuomba wanyimwe dhamana kwa sababu za kijinga na kisha kukaa ndani siku 133 yaani zaidi ya miezi minne sio LA kuangalia kitoto na kuliacha liendelee kimya.
Iweje Leo Mahakama Kuu ikiwa tayari kutolea maamuzi DPP atoe tamko kuwa hana nia na kesi hiyo tena? Hii inaonyesha kesi haikuwa na maslahi ya taifa bali mtu binafsi, ni nani huyo?
Lazima tumjue, maana maonezi ya aina hii ndio yamezua matendo ya kigaidi au uhujumu kwa nchi nyingine ambapo madhara yaliwakuta waliohusika na wasio husika.
Tafadhali tutajieni ni nani mhusika mkuu aliyetumia sheria za nchi kwa manufaa na furaha yake binafsi?