Ni nani kwa maamuzi yake Binafsi ametumia Sheria zetu kuwatesa vijana hawa?

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
842
2,467
Wakati umefika sasa tuwe tunawajua watu kwa majina pale wanapotumia ofisi za umma kihuni na kutesa watu bila huruma kwa kisingizio cha sheria.

Suala la vijana viongozi wa BAVICHA (Nusrat na Mwaipaya) waliowekwa ndani Singida na ofisi ya DPP kuamua kuomba wanyimwe dhamana kwa sababu za kijinga na kisha kukaa ndani siku 133 yaani zaidi ya miezi minne sio LA kuangalia kitoto na kuliacha liendelee kimya.

Iweje Leo Mahakama Kuu ikiwa tayari kutolea maamuzi DPP atoe tamko kuwa hana nia na kesi hiyo tena? Hii inaonyesha kesi haikuwa na maslahi ya taifa bali mtu binafsi, ni nani huyo?

Lazima tumjue, maana maonezi ya aina hii ndio yamezua matendo ya kigaidi au uhujumu kwa nchi nyingine ambapo madhara yaliwakuta waliohusika na wasio husika.

Tafadhali tutajieni ni nani mhusika mkuu aliyetumia sheria za nchi kwa manufaa na furaha yake binafsi?
 
IMG_7649.JPG
Compare & Contrast
 
Mkuu usihangaike hayo ni maelekezo kutoka juu kwa Mhutu , Biswalo Mganga na Hakimu mkazi Singida ni watekelezaji tu . Watanzania someni dua ya kuwasomea viongozi dhalimu na jeuri kifayaatu ssabat Mungu atatusikia tu na atawanyoosha watesi wetu inshallah .
 
Mtu wakulaumiwa na kushitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi ni huyu DPP mshambaa!! Ameshanusa na kuona hana Tena uthibitisho wala hawezi kuwatia hatiani akaamua kuachana na kesi, maana yake ninishitaki kwa taratibu za kidhalimu za mahakama na sheria yetu mtuhumiwa aliyeonewa hana uwezo wakufungua kesi ya madai dhidi ya uonevu aliyotendewa kwakigezo Cha kesi hakufika mwisho.

Poor DPP
 
Wakati umefika sasa tuwe tunawajua watu kwa majina pale wanapotumia ofisi za umma kihuni na kutesa watu bila huruma kwa kisingizio cha sheria.

Suala la vijana viongozi wa BAVICHA (Nusrat na Mwaipaya) waliowekwa ndani Singida na ofisi ya DPP kuamua kuomba wanyimwe dhamana kwa sababu za kijinga na kisha kukaa ndani siku 133 yaani zaidi ya miezi minne sio LA kuangalia kitoto na kuliacha liendelee kimya.

Iweje Leo Mahakama Kuu ikiwa tayari kutolea maamuzi DPP atoe tamko kuwa hana nia na kesi hiyo tena? Hii inaonyesha kesi haikuwa na maslahi ya taifa bali mtu binafsi, ni nani huyo?

Lazima tumjue, maana maonezi ya aina hii ndio yamezua matendo ya kigaidi au uhujumu kwa nchi nyingine ambapo madhara yaliwakuta waliohusika na wasio husika.

Tafadhali tutajieni ni nani mhusika mkuu aliyetumia sheria za nchi kwa manufaa na furaha yake binafsi?
DPP anapokea maelekezo kutoka ikulu, speaker ndugai pia, mahakamani kuna baadhi ya hukumu zinatayarishwa na kupitishwa na ikulu. Huo ndio maana ya udikteta kamili
 
DPP anatumia ofisi yake vibaya!! haya ndiyo mambo unaweza kujikuta baadaye unashitakiwa - makosa ya matumizi mabaya ya ofisi huwa hayafutiki hata ukiwa na miaka 80 unakabiliana nayo tu.
 
Hapo tatizo ni la DPP au Hakimu mkazi?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom