huyu ametokea BOT Taraining Institute Mwanza, amekuwa pale kwa muda tu ni mchumi mbobezi, ni mtaratibu na mchambuzi mzuri wa uchumi, kwa waliobahatika kusikia uchambuzi wake katika kikao cha mwisho cha bune lililopita, badala ya kulalamika kama wengine, yeye alijikita katika kuhoji sera za serikali zinafanya nini kuhakikisha kukua kwa uchumi, kunaenda sambamba na kuboreka kwa hali ya amaisha kwa wananchi walio wengi hususani vijini.
alitolea mfana mchango mdogo wa sekta ya fedha katika kukua kwa maendeleo vijiji ambapo kwa takwimu alizotaja Tanzania ni ya mwisho kwa ukuaji wa sekta ya fedha vijini, inatanguliwa na Kenya na Uganda kwa mbali.
akadokeza kwamba katika miaka ya karibuni, mchango wa sekta ya kilimo katika GDP umeshuka sana, na kwamba hali hiyo ingekubalika kama sekta zilizochukua nafasi (kukua badala ya kilimo) zingekuwa zinatoa mchango wa kuboresha maisha vijijini, jambo ambalo sivyo kwani sekta zinazokua sasa ni mfano sekta za madini ambazo zinawanufaisha zinazowajua wao, kimsingi ana maono, sasa sijui wamempa liwizara hilo ili kuonesha kwamba tanzania imeshindikina ikiwa na yeye atashindwa kudhibiti mfumuko wa bei na kutawanya uchumi kwa wananchi, au watashirikiana naye kufanya kile ambacho wamekuwa wakishindwa, Namtakia kila la heri..