Ni nani atakayekulilia siku ukifa?

Ni nani atakayekulilia siku ukifa?

Papa Mobimba

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
1,153
Reaction score
1,359
Hivi umewahi kukakaa na kuwaza kama ukifa leo, ni nani atakaye kulilia? Je ni mama yako? Au yule dada yako? Au mchepuko wako ulioununulia Iphone ya gharama au mangi aliyekuwa anakukopesha vitu unalipa mwisho wa mwezi? Au yule baada maid aliyewahi kukuandikia kwenye bili wewe kaka mwenye kitambi naomba uninulie bia moja. Ni nani hasa atayekulia

Je katika maisha yako umekuwa mtu wa majivuno? Umekuwa mtu wa kujipenda wewe mwenyewe kuliko binadamu wenzako. Hivi umewahi kumpa mwaliko hata wa chakula cha mchana yule jirani yako ambaye unajua kabisa hana hali nzuri kama wewe hapo!

Unafikiri mama yako atalia, wakati inapita wiki hata salamu hujamjulia? Dada yako atakulia? Fikiria tena kama mchepuko wako atakulia? Ni mkeo au mmeo? Nani atakulialia?

Hivi umewahi kugusa maisha ya nani hata kwa kidogo ulichobarikiwa. Umewahi kumsaidia nani wakati wa dhiki? Wewe umejitoa kwa ajali ya nani?

Lakini pia sio lazima mtu akulilie kwa sababu hujawahi kugusa maisha yake. Sio lazima kuliliwa kwa sababu waliokufa hawana ijara tena. Waliokufa hana walijualo?

Hata mimi sijui ni nani atanililia siku nikifa, lakini najua wengi watalia kwa sababu nimewahi kugusa maisha yao. Nimewahi kurudisha nuru na furaha katika maisha yao.

Asante kama umenielewa! Kama hujanielewa, utajifunza taratibu
 
Sasa utajuaje kua nani atakulilia wakati hujui ni nani kati yako na hao watakaokulilia ndiye atakayetangulia kufa? mtu anasema "Mama yangu atanililia" unajuaje kua wewe utatangulia kabla yake?

Ishi vizuri na watu,jiheshimu,heshimu wenzako kisha mpende Mungu,kama huna matendo mema hata kama dunia nzima itakulilia baada ya kufa kwako ni kazi bure tu,

Mtu hulipwa kwa matendo yake mema aliyoyatanguliza na sio kwa idadi ya watu waliomlilia baada ya yeye kufa.
 
kwan wasipolia hautazikwa, ama kuvishwa sanda ama hauto oshwa kabla ya kuzikwa?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu huwa nikiwa nina matatizo familia yangu huwa inakuwa na mimi bega kwa bega, watalia na mimi pia watahuzunika na mimi najiuliza namna hii niko hai siku nikifa watalia kiasi gani 🤔🤔kifupi familia yangu italia sana nikifa.
 
Mkuu huwa nikiwa nina matatizo familia yangu huwa inakuwa na mimi bega kwa bega, watalia na mimi pia watahuzunika na mimi najiuliza namna hii niko hai siku nikifa watalia kiasi gani [emoji848][emoji848]kifupi familia yangu italia sana nikifa.
[emoji860][emoji860]tafiti zisizo rasimi zinadai kuwa wanaolia sana msibani wanatakiwa wachunguzwe kwa umakini maana wanaweza kuwa ni moja ya chanzo cha kifo cha marehem eg wachawi.

kwa upande wang hata nisipoliliwa ni sawa tu, maana huwezi jivunia kuliliwa wakati tendo lenyewe la kuliliwa haulioni..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom