mbwigule
JF-Expert Member
- Jan 21, 2012
- 235
- 103
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko ya kichinichini na waziwazi juu ya utendaji wa hii Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambayo inahusishwa na wizi wa fedha za wateja zinazobaki kama salio, utozaji wa gharama kwa huduma hewa, ulaghai na ukwepaji kodi uliokithiri ambao pia makampuni mengine ya mitandao ya mawasiliano yanahusika ingawa uhusika wa Vodacom ni wa kiwango kikubwa mno.
La kutia kichefuchefu ni jinsi Kampuni hii inavyoweza kufanya kila aina ya uhalifu mbele ya vyombo vyote vya usalama wa nchi hii; inashangaza kuona kwamba haya yanafanyika licha ya uwepo wa TAKUKURU, Usalama wa Taifa, TRA na hata hili dude butu, lisilo na maana yoyote liitwalo Tume ya Mawasiliano.
Je, ni kweli kwamba hakuna kabisa ndani ya serikali hii ya CCM anayefahamu lolote juu ya uhalifu wa genge hili la kihalifu au ndiyo uthibitisho wa ile dhana iliyoko mitaani kwamba kampuni hiyo haiwezi kabisa kuguswa na yeyote kwani miongoni kwa wenye hisa humo ni vigogo walioko ndani ya serikali wakiwemo kina Lowassa, CCM na hata "mkulu" wa kaya?
Kampuni zote wanaiba lakini hawa wametubanjua fora, kwani hata ukilaza Sh. 100 asubuhi huikuti! Mwenyewe nilikuwa siamini lakini niliamini baada ya kuacha 5000 nzima na kukuta asubuhi zimeliwa zote na kibaki na salio la 300! Ni nini hii kama si ujambazi unaosaidiwa na kufanikishwa na tuliowapa dhamana ya kulilinda taifa?