Ni nani anayewapa kiburi walicho nacho Vodacom?

mbwigule

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
235
195
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko ya kichinichini na waziwazi juu ya utendaji wa hii Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom ambayo inahusishwa na wizi wa fedha za wateja zinazobaki kama salio, utozaji wa gharama kwa huduma hewa, ulaghai na ukwepaji kodi uliokithiri ambao pia makampuni mengine ya mitandao ya mawasiliano yanahusika ingawa uhusika wa Vodacom ni wa kiwango kikubwa mno.
La kutia kichefuchefu ni jinsi Kampuni hii inavyoweza kufanya kila aina ya uhalifu mbele ya vyombo vyote vya usalama wa nchi hii; inashangaza kuona kwamba haya yanafanyika licha ya uwepo wa TAKUKURU, Usalama wa Taifa, TRA na hata hili dude butu, lisilo na maana yoyote liitwalo Tume ya Mawasiliano.
Je, ni kweli kwamba hakuna kabisa ndani ya serikali hii ya CCM anayefahamu lolote juu ya uhalifu wa genge hili la kihalifu au ndiyo uthibitisho wa ile dhana iliyoko mitaani kwamba kampuni hiyo haiwezi kabisa kuguswa na yeyote kwani miongoni kwa wenye hisa humo ni vigogo walioko ndani ya serikali wakiwemo kina Lowassa, CCM na hata "mkulu" wa kaya?
Kampuni zote wanaiba lakini hawa wametubanjua fora, kwani hata ukilaza Sh. 100 asubuhi huikuti! Mwenyewe nilikuwa siamini lakini niliamini baada ya kuacha 5000 nzima na kukuta asubuhi zimeliwa zote na kibaki na salio la 300! Ni nini hii kama si ujambazi unaosaidiwa na kufanikishwa na tuliowapa dhamana ya kulilinda taifa?
 

mwanza_kwetu

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
687
195
Peleks malalamiko yako TCRA. Humu utaongea tu then what. Umeshaenda hata kulalamika au umesubscribe VAS services na sasa zinauma
 

mchillo

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
488
250
Mkuu umesema yote, ni lazima iko namna; si bure! Maana ukimwona mbwa juu ya mti ujue kapandishwa!
Kwa kweli inasikitisha.
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,062
2,000
haya unayolalamika leo nishakumbana nayo miezi kadhaa iliyopita na nilikuwa nikiwatunakana wale wahudumu wa customer care bure tu.nilichokifanya nilihamia airtel na ile line ya Vodacom nikaiweka kwenye ka simu ka tochi na ina miezi 4 sijawekamo hata mia.
 

Mwihadisa

JF-Expert Member
Dec 31, 2012
608
195
Kumbe.....ngoja tuhamie kwa bingwa wa mabingwa pengine tutaenda Old Trafford kupiga pichana Wayne Rooney...
 

tusichoke

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
1,313
1,250
Ndugu ktk matajiri waliotajwa Tanzania yumo mmoja wao ambae alikuwa mbunge asiri ya kiasia anamiliki his a kubwa ndani ya vodacom Tanzania. Huu unaweza kuwa mkakati maalum wa kukusanya pesa Kwa kazi maalum
 

rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,268
2,000
rostam,lowasa na pale kwenye wizara ya mawasiliano kuna mpambe wao naibu waziri pia usisahau wao ndio walienda wakagawa simu bure kwa wabunge wote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom