Kuna mkuu hapo kaongelea list ya programs zilizoipa umaarufu mkubwa ITV.. Jamaa wanatembelea nyota ya vipindi vya zamani vilivowapa kickhiyo ndo siri ya mafanikio ya ITV kupewa tuzo ya superbrand kila mwaka. Yani kila kitu kipo vile vile marekebisho ni madogo mno wamefanya. mfano logo wameiacha ile ile hawajabadili kama channel ten. Sikiliza ule mlio wa habari ni ule ule tangu 2000 huko hadi leo. ujue kitu ambacho umekizoea kila siku unakiona na kinakuvutia siku kikibadilika kuna uwezekano na wewe ukabadilika ukakichukia. inshort jamaa bodi ya wahariri, warusha matangazo (mfano kina Benedict Lusese, Paul Urio), mafundi karibia wote ni wale wale coz elimu yao ni nzuri na hawajaona waku_replace nafasi zao hadi CEO wao ni yule yule haja_change, labda presenters ndo wanawabadilisha. na mission yao ni ile ile kama inachange bas wanabadilisha kidogo tu kuendana na ulimwengu mfano social networks, website, applications. jamaa contents zao hazipo complicated ni simple kuelewa na simple graphics yeyote anaweza kuelewa what is going on. Presenters wao wapo straight hakuna kuzunguka saana kama wengine. na wanaenda kwa matukio. kile kinachozungumzwa sana mtaani ndo kinarushwa ITV.
Pia walikosa mshindani wa kueleweka. Watu wote walikuwa wanaangalia ITV. Sa hizi audience imegawanyika sana. Asipotaka kuchangamka atapotea miaka michache ijayo