GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,623
- 108,986
Nilipoona tu tamko la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likisema kuwa haliwezi Kuingilia kati Mgogoro wa Matumizi ya Maji ya Mto Nile kati ya nchi za Misri na Ethiopia kwakuwa inajua kuwa Misri ina uhalali wa 87% ya Maji ya Mto huo nimeshtuka na kuwa na maswali mengi mno.
Hivi ni lini Waafrika na hasa huu Umoja wa Afrika (AU) utasimama imara kabisa Kutetea na Kusimamia Maslahi ya Bara la Afrika na Rasilimali zake kwa ujumla? Kwanini iliyokuwa (OAU) miaka ya nyuma ilishindwa kuwa Sauti ya Kujiamini kwa nchi zote za Afrika ili Afrika tusikike, tueleweke na tuheshimike mno.
Hainiingii Akilini kabisa leo hii kusikia nchi kama za Misri na Ethiopia kila Uchao tu zinagombania Umiliki wa Mto Nile wakati sehemu Kubwa na iliyoanzia hadi hata kupita nchi kama za Uganda na Sudan nazo zina haki ya Umiliki lakini zimenyamaza na zikiwaangalia kama hata si Kuwashangaa pia.
Wazungu wanapenda sana Kutuingilia na Kutupangia mambo yetu mengi Waafrika na kwa jinsi Viongozi wengi wa Bara la Afrika walivyo Goi Goi na wa hovyo hovyo kiasi cha Kuwaogopa Wazungu hawa Waafrika wote tunadharaulika na kuonekana hakuna tunalolijua na hata kuliweza zaidi ya kuwa Waongo, Wavivu na Wachawi wa Kutukuka.