Ni nafasi ya NCCR badala ya CCM, CDM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nafasi ya NCCR badala ya CCM, CDM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by February, Jan 27, 2012.

 1. February

  February Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Siasa za tanzania zinamezwa na vyama viwili CDM na CCM, kuna wakati vyote vinakosea na watz wangetamani mawazo nje ya vyma hivi viwili vikubwa nchini. Ukifanya uchambuzi vyama kama cuf,tlp,udp ni marehemu tayari huku bara. Chama pekee walau kinaweza kutoa mwanga huu ni nccr mageuzi kama kitawatumia wabunge wake vizuri kufikisha ujumbe na salamu za ukombozi. Ni wakati nccr waoneshe watz kuwa bado kuna matumaini nje ya ccm na cdm.nasema nccr kwasababu hakuna ubishi kuwa cuf ni sehemu ya sisiemu bada SUK, TLP,UDP ni matawi ya sisiemu miaka yote. Tumaini pekee hasa kwa vijana ni Nccr. Nawaomba viongozi nccr itazameni fursa hii watu wapo tayari. Mbatia ni mzoefu, dr Mvungi ni msomi aliyetukuka ktk taifa hili mkiunganisha nguvu na vijana wapambanaji kama mh machali na mh mkosamali mnaweza kuitumia hazina hii ya vijana wenye vipaji na tayari wapo bungeni. Ni wazo tu. Natoa wito kwa nccr kufungua njia kwa hoja na agenda zenu. Mambo ya migogoro yapotezeeni. Yatakwisha natural death. Hakuna sababu ya kujibizana baada ya maamuzi. Tusonge mbele jamani.
   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  February,

  Usijali, kwani zamu yenu itafika tu kwani hakuna Chama chochote cha siasa hivi sasa kinachoendesha shughuli zake kwa itikadi, jambo ambalo lingewasaidia kupata wafuasi na mafanikio ya kudumu. Badala yake vyama vyote vina umarufu wa mpito:

  1. Chama Changu Cha CCM (umaarufu wetu unatokana na personalities za baadhi ya wanasiasa ndani ya chama chetu ambazo zinawapa wananchi mvuto; tunamiliki dola na vimulimuli, hivyo wananchi wanaduwaa; na pia kuna suala la mazoea, hasa kwa wananchi wa vijijini - wana mazoea na CCM, so they are better off to deal with the devil that they know); Vinginevyo, Itikadi na Siasa yetu ya ujamaa na kujitegemea ipo kwenye vipeperushi tu;

  2. Chadema (wao pia wana umaarufu wa mpito kama vile personalities na profile za baadhi ya viongozi wake ambao wanawapa wananchi mvuto; pia umaarufu utokanao na kampeni dhidi ya ufisadi; na suala la katiba mpya); CDM wana itikadi ya 'mrengo wa kati', lakini hatuoni idara yake ya siasa na uenezi ikiifikisha hii mioyoni mwa UMMA; ukichukua wananchi kumi randomly uwaulize unapenda chama gani? nina hakika majority watasema Chadema; Ukiuliza, Chama Chako Cha Chadema kina itikadi gani? atakukodolea tu macho, na punde ataanza masuala ya kuchoshwa na ufisadi, madai ya katiba mpya...

  3. CUF ( umaarufu wao ni kutokana na malengo na mafanikio yao kuwakomboa zanzibar ambao sasa ni taifa jipya with self determination; lakini kama ilivyokuwa kwa chama chochote cha ukombozi africa, kitapitia hatua tatu za maisha yake - growth, maturity, then saturation; Kwa sasa CUF ipo kwenye growth bado, na soon kitaingia kwenye hatua ya pili ambayo mafanikio yatatokana na utekelezaji wa ahadi zake za ukombozi; kikishindwa, na vikija vyama vipya zanzibar, CUF itaingia katiak maturity, na baadae saturation, njia ile ile tuliyopitia sisi TANU/CCM, katika siasa za bara). Itikadi ya CUF ni uliberali, ambayo nayo haipo practised na chama, zaidi ya kauli mbiu ya 'haki sawa kwa watu wote' Isitoshe, itikadi ya uliberali ina mapungufu makubwa mno, kubwa ikiwa kutojali sana maisha ya watu wa chini. Give the fact kwamba wananchi wa Zanzibar waliokombolewa na CUF kutokana Tanzania Bara, ni wananchi walio nyuma sana kiuchumi, bila umakini, itikadi hii itaanguka kirahisi sana.

  4. NCCR (umaarufu wenu unatokana na jitihadi zenu za kugombania umaarufu wa wenzenu; siasa zenu ni za kujitahidi kujaribu na nyinyi msipitwe na kila jambo 'la kupita'.);

  Ndugu February, itikadi yenu NCCR ni ipi? tafadhali nielimishe.

  Masuala haya yote hayana mashiko ya kudumu kwa vyama vyote hivi.

  Hata Marekani, ilipata uhuru wake chini ya jamii isiyokuwa na vyama vya siasa, na hata katiba yake ilizaliwa katika mazingira yasiyokuwa na vyama vya siasa, na pole pole ikawa inafanyiwa marekebisho. Lakini pamoja na kutokuwepo kwa vyama vya siasa, jamii hii ilikuwa na itikadi zake mbalimbali, kwani itikadi sio zao la chama cha siasa bali ni zao la jamii, kama vile ilivyokuwa kwa chama cha siasa - chama sio zao la itikadi bali zao la jamii. Kumbuka,Itikadi ni:

  "Mtazamo, mwongozo, value system, spirit ya taifa, around which matukio na matendo yote ndani ya jamii revolves, hivyo kuimarisha maana, mwelekeo, na tafsiri ya masuala mbali mbali ya ulimwengu, kwa jamii husika."

  Ndio maana Marekani, ndani ya muda mchache, vyama vikaanza kuzaliwa ili kuanza kupigania itikadi zilizokuwepo kwenye jamii kwamba hii ni bora kuliko ile n.k; na matokeo yake ni vyama vikuu viwili democrats na republicans ambavyo core value zao wote ni itikadi.

  Kwahiyo usiwe na wasiwasi na NCCR yenu, kwani kwenye suala la umaarufu wa mpito nyinyi ndio waasisi, kwani miaka ya mwanzo hadi katikati ya 1990, mlikuwa juu sana, na mngeweza kabisa kuchukua nchi kama palepale mngewekeza katika itikadi, badala yake mkazidi wekeza kwenye personalities - bagenda, kaborou, mrema, Lamwai, mabere marando, na vile vile kwenye agenda ya ufisadi chini ya utawala wa rais Mwinyi. Pamoja na umuhimu wa vitu hivi, hakuna ubishi kwamba ni vya mpito, na nyinyi NCCR ilitakiwa liwe funzo kwa vyama vingine. Lakini inaonekana hata vyama vingine vinatenda makosa yale yale.

  Kwahiyo ningependa nikuhakikishie tu kwamba, as long as mambo yanabaki hivi hivi - yani siasa zisizoendeshwa kwa itikadi miongoni mwa CCM, CDM, CUF, zamu ya mafanikio yenu "PART 2" (kwani part one ni ile ya miaka ya 90), zamu yenu itakuja tu. Cha maana kwa sasa ni kuzidi kusali na kuombea vyama vilivyopo viendelee kung'a'gania masuala ya mpito badala ya kuendesha idara zao za siasa na uenezi kwa itikadi ambazo wanachama wao watazielewa na kuzishiba kama ndio core values za vyama vyama, hivyo kuwa na imani kwamba hiyo/hizo ndio direction wanataka taifa lao lielekee, na hivyo kuwa wanachama wa kudumu, wenye kupigania itikadi yao/zao na kuisambaza, huko kwenye makazi yao (mijini na vijijini), hata kwa kujitolea.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 3. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mchambuzi

  Umesema chama cha ukombozi kinapitia hatua tatu growth, maturity then saturation nafikiri umesahau na death, kama chama chako CCM kimepitia hatua zote hizo unatuambia sasa kipo kwenye hatua ya mwisho ya kifo.
   
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Niliacha 'death' kwasababu mara nyingi before chama cha ukombozi Afrika kifikie death, mara nyingi it has to cause death upon innocent citizens, sometimes in masses. Imani yangu ni kwamba CCM itaishia kwenye saturation level, then at some point, loose elections, ili tujipange upya, kwani tunachukulia uongozi wa nchi kama ni kitu guaranteed for ever. Otherwise upo sahihi.
   
 5. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,973
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nccr inaweza kweli kufufuka na kuwa chama chenye nguvu na mawazo mbadala? Mimi siamini Kama kinaweza.
   
 6. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kuna Vacuum kubwa sana ya itikadi hivi sasa. Chama chochote nje ya chadema, au hata kipya kinaweza geuza siasa za nchii hii miguu juu, iwapo kitawekeza katika itikadi. Vingonevyo kwa sasa vyama vingi vimewekeza kwenye mambo ya mpito kama katiba mpya, ufisadi, lakini zaidi vinashamiri kutokana na personalities za wanasiasa waliomo ndani ya vyama hivi.

  Hivi karibuni nilikuwa Arusha na Mbeya, nikaamua kufanya kautafiti kadogo. Nilikusanya vijana 20 randomly katika kila mikoa na kuwauliza, hivi nyinyi mnashabikia chama gani? Arusha, 16 of 20 said Chadema, Mbeya wote said Chadema. Nikawauliza, Chadema itikadi yake nini? Hawakunielewa, nikawauliza, kwanini mna imani na Chadema? hapo wakapata idea, na kusema kwamba wamechoka na Ufisadi wa CCM. Wengine pia walitaja suala la katiba. Nikawauliza, haya mawili yakipatiwa ufumbuzi je, mtakuwa wapenzi wa Chadema kwa sababu zipi? wakajibu kwamba Chadema wapo juu. Nikauliza, kivipi? Wakaanza kuzungumzia majina maarufu ya viongozi wa chadema kwamba wapo juu. Nikaondoka nikijiuliza, hivi kwa mfano ukiondoa viongozi wa chadema uwaweke pembeni, ukiondoa ufisadi, na ukiondoa suala la katiba, Chadema ina nguvu gani? Dont get me wrong, Chadema ina potential kubwa sana lakini bado sana kufikia mafanikio ya kudumu kwa sababa hawana core value iiliyokuwa unique na yenye mashiko ya kudumu kwa wananchi. NCCR ilikumbwa na haya haya kwani kilipata mafanikio makubwa sana in the 1990s kutokana na sababu za mpito kama vile majina makubwa - Marando, Kaborou, Bagenda, Lamwai, Mrema, n.k, na pia kutokana na udhaifu wa uongozi wa Mwinyi uliozaa ufisadi mkubwa. Laiti NCCR wangewekeza kweney itikadi, leo tungekuwa tunaongea mengine, hata kama Nyerere alikuwepo. Otherwise, kampeni zikawa zaidi on personalities, Nyerere Versus Mrema and Crew. Chadema wakaze mwendo katika hili, kwani CCM sasahivi kipo ICU, ila kinaweza kufufuka iwapo kitaliwahi suala la itikadi before Chadema. Otherwise tujiandae CCM kuanguka, Chadema kuchukua nchi, na baada ya miaka michache sana Chadema kupoteza nchi kutokana na wananchi kutoridhika na kaqsi ya Chadema kumaliza umaskini etc, kwani siasa za chadema za sasa zipo zaidi based on that, badala ya kuwa based on itikadi ambayo wananchi watakuwa tayari kuvumilia maendeleo ya kasi ya pole pole kwani vichwani watakuwa consumed zaidi na itikadi with hopes kwamba itikadi husika ndio njia sahihi kwa vizazi vyao vya baadae.

  Kauli ya Dr. Slaa hivi karibuni kwamba "Kazi yetu ni kuikosoa serikali, ikirekebisha matatizo yote, tutaishiwa na hoja", inathibitisha mengi ambayo nimekuwa naimba kama mwendawazimu kuhusu umuhimu wa itikadi kwa chama. Ipo siku watanzania watakuja kulibaini hili, na hata humu JF, suala hili litakuja kuwa kubwa baada ya kutamkwa na watu wenye heshima au nafasi kubwa kwenye jamii yetu. Hadi tufikie huko, kwa sasa nipo tayari kuonekana mwehu au kutafsiriwa vyovyote vile kutokana na kauli zangu juu ya umuhimu wa itikadi kwa mafanikio ya kudumu na yenye mashiko kwa chama cha siasa, badala y amambo ya mpito kama vile katiba mpya, ufisadi, na personalities/umaarufu za wanasiasa wa vyama husika. Tukumbuke tu kwamba vitu vyote hivi hufa au huisha, lakini itikadi hudumu.
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi hapo unaeleweka sawia!
   
 8. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mchambuzi

  Idiology Tanzania? you must be joking, kitu hicho ni stage ya juu sana wa upeo kwenye nyanja za siasa especially wa nchi zetu hizi, hata kwa nchi zilizoendelea ni wachache sana wanaoangalia idiology ya chama wengi wanapelekwa na matukio wananchagua chama kutokana na matukio mfano vita vya Iraki, healthcare reform, nani kamuua Osama nk. Kwenye uchaguzi wa US uliopita Sarah Palin aliyekuwa mgombea mwenza wa Mc Cain aliulizwa na Gibson -"Do you agree with the
  Bush doctrine" akabaki anashangaa doctrine ni kitu gani, sasa unataka kwenda Merelani ukaulize idiology ya Chadema unategemea nini.

  Mchambuzi unasema ufisadi ukiisha na katiba ikiandikwa Chadema itaishiwa hoja. Inaonyesha wewe si mwanasiasa bali ni mwanazuoni muumini wa siasa za vitabuni pale Kigamboni. Vita vya Iraki vimeisha Marekani imekosa cha kusema? Osama ameuawa je wameishia hapo kwamba wana relax? Kama unaamini kwisha kwa ufisadi ndio mwisho wa CDM hujiulizi kwa nini CCM haiwapeleki mahakamani watuhumiwa waufisadi. Wanajua wakithubutu kufanya hivyo utakuwa ni ushindi mkubwa mno wa Chadema wananchi ndio watazidi kukiamini chama tofauti na unavyofikiria. Elewa mwisho wa tukio ni mwanzo watukio lingine.
   
 9. M

  MPG JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maralia imekupanda wewe,hiyo Nccr ya mwenyekiti Mbatia kuwadi mkuu wa CCM imkomboe nani?Ukombozi wa Mtanzania ni mtanzania mwenyewe akiamua kujikomboa ataweza kwa kuachana na siasa za maji taka za CCM Pamoja na washiriki wenzake Cuf,NCCR,TLP,UDP!.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  NCCR? You are joking.Chini ya Mbatia? Ee Mola tunusuru
   
 11. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Feedback, umejenga hoja hai sana dhidi ya mchambuzi kwa jinsi ulivomjibu kuhusu kuisha kwa ufisadi, katiba mpya na CDM kuishiwa hoja, Hongera sana.
   
 12. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  NCCR majirani zangu ilala wako taaban. Ukiwapa nchi hawa watatuangusha kiasi tutashindwa tena kusimama. KUPANGA NI KUCHAGUWA. LAKINI CHAGUWA KUNAHITAJI TAFAKURI.
   
 13. Gerald

  Gerald JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu ni mara ya kwanza mwana CCM kidogo kuongea jambo makini ongera
   
 14. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,157
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Nimeingia kwenye hii thread najihisi nipo kwenye jukwaa la jokes/utani and gossips/udaku, nahisi kucheka lakini nitaonekana mwehu kwa sababu hapa si mahala pake, anyway ngoja niondoke nisije wakera bure kama harufu ya kwapa
   
 15. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Usijichanganye na bush doctrine. Do a little bit of home work on ideologies in US politics. For instance, one of the main pillars of the conservatives ideology is the stance on national security, which has been receiving tons of criticisms, both from the other ideological stand point (e.g.democrats), but also worldwide, whereby they argue kwamba, msimamo wa conservatives on foreign policy is too aggressive and might be counter productive, may lead to security destabilization within the US and the world at large. Lakini conservative pia defend themselves kwamba – America should present itself as strong and formidable and intervene where it deems necessary, and also sserting that, taking a more cautionary approach can be viewed as appeasement and encourage other states to act belligerently. Democrats are big believers of cautionary approach.

  Hoja yako kwamba suala la itikadi katika siasa za Tanzania kwamba ni suala irrelevant, I choose to disagree with you, kwa maelezo yale yale ambayo nitakuwa najirudia tu. Ningependa kuelezea kwa kirefu kwanini nchi nyingi za afrika vyama vyake vina pengo la itikadi lakini nitafanya hivyo siku nyingine. Vinginevyo tatizo hili, wengi wanalichukulia kama ni asili yetu wakati suala halipo hivyo. Pia nikuambie tu kwamba itikadi haina umri, na sio kitu cha jamii kukingojea, kama unavyojaribu kueleza. Kafanye utafiti kidogo kuhusu maana ya itikadi ni nini. Unanishangaza kidogo unapozungumza as if itikadi ni suala linalozaliwa na chama cha siasa, au linalokomaa kutokana na uzoefu wa kisiasa, wakati ukweli ni kwamba itikadi ni zao la jamii, hata kama hakuna chama cha siasa, itikadi ipo tu. Hata wewe hapo ulipo una itikadi, hata bila kufikiria siasa, ni kwa sababu tu hauna uelewa wa kutosha juu ya dhana ya itikadi, ndio maana unaielezea as if ni zao la siasa au chama cha siasa. Kinachofanywa na vyama vya siasa ni ku-hijack itikadi zilizopo kwenye jamii na kuzijengea mazingira ya kisiasa, kwa ahadi kwamba wakipata uongozi wataenda kutekeleza mawazo, matarajio, mwono, spirit n.k (zote hizi zikiwa ni elements za itikadi), za wanajamii husika. Hata ukiangalia historia ya CCM, nguvu yake ilitokana na itikadi ya ujamaa, kulikuwa na imani kubwa sana kuhusu itikadi hiyo. Na itikadi ya ujamaa ilizaliwa kutokana na experience ya ukoloni. Fanya utafiti kidogo kubaini kwanini Ujamaa ulikuja mwaka 1967, na sio kabla ya hapo. Jamii ilikuwa na itikadi yenye elements za kijamaa, hivyo mwalimu akaifanyia tu programming na kui - package vizuri kama sera.

  Hata marekani, itikadi zilizaliwa hata kabla ya vyama vya siasa, na jamii ile ilikuwa na itikadi zao (misimamo, mitazamo, mwono kuhus jamii yao versus ile inayowazunguka n.k), haya yalikuwepo hata kabla ya ujio wa vyama vya siasa, ni baadae vilipo zaliwa vyama vya siasa, ndipo wakaweka misimamo hii katika mazingira ya kisiasa, mfano umuhimu wa kujilinda kama taifa - lilikuwa ni koloni la mwingereza, and they fought for their independence, and it wasn't an easy walk to freedom. Nadhani nisijirudie zaidi, mengi nimeshayaeleza, ni sual tu la kukubaliana au kutokubaliana, especially kuhusu hoja zangu juu ya vyama vyetu vya siasa na umaarufu mpito kama vile katiba mpya, ufisadi etc. Utafiti wangu wa Mbeya na Arusha, ukiweza nenda kule kaurudie na wewe, utabaini haya haya. What's the core and unshaken value among wafuasi wa chadema? Je, ni uchovu na CCM? Bila shaka ni hilo. Sijui kwanini inakuwa ngumu kwa watu kuelewa tatizo hili. CCM imechoka, hilo halina ubishi, lakini chama chochote kikija kukitoa CCM madarakani, nacho kitakuwa hakina dira, bali mwongozo wa kushikwa masikio na IMF na WorldBank kama CCM. Ndio maan Chadema wakipata matatizo, sometimes wanakimbilia kule kule kwa maadui hawa wa maendeleo (mabalozi wa EU). Huu ni udhaifu mkubwa, na chanzo chake ni itikadi.

  Vinginevyo, ipo siku haya nayosema yatakuja dhihirika na kupewa umuhimu wa juu sana, natumaini basi angalau utakumbuka kwamba Mchambuzi aliwahi kuyasema haya. Until then, lets agree to disagree.
   
 16. George Kahangwa

  George Kahangwa Verified User

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2007
  Messages: 539
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu Mchambuzi,
  Ukisoma katiba ya NCCR-mageuzi utaona kwamba ni chama kinachotumia itikadi ya Social Democracy (Itikadi ambayo inakataa unyama wa ubepari lakini haiko sana katika kukubali kila hoja ya ujamaa)
  Aidha, mwanzoni mwa mwaka jana (2011) Halmashauri kuu ya NCCR-Mageuzi ililidhia kuboresha itikadi yake, na sasa Chama Kinajitambulisha kwa Falsafa na Itikadi ya UTU.
  Chama kinasema, misingi ya UTU ni UMUHIMUWaKE, yaani
  UDUGU
  MAADILI
  USAWA
  HAKI
  IMANI
  MABADILIKO au MAGEUZI
  UKOMBOZI
  WAJIBU
  KAZI
  ENDELEVU (sustainability)
  Misingi hii yapaswa kuwa ndio kiongozi cha masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
  Chama kiko mbioni kuchapisha kitabu chenye ufafanuzi wa kina wa Itikadi hii
   
 17. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Then hii ni itikadi more practical kuliko zote zilizopo sasa - ni more promising kuliko itikadi za to CCM, CHADEMA na CUF, kwani angalau hii ina upenyo wa kupingana na majangili wa IMF na WorldBank, kwani CCM, CDM, wote wanaendesha siasa za kuwapigia magoti watu hawa. Wanachoshindania CCM na CDM ni kwenda ikulu kuwa mtekelezaji wa masharti ya IMF na World Bank kwa ufanisi kuliko mwenzake. Hakuna sehemu ya sera zao ambako wanatambua jinsi gani madudu haya yanachangia umaskini katika nchi yetu. The future of Tanzanai lies on Political Parties with Social Democracy Orientation. Nitakuja kufafanua hili siku nyingine, kwani najua maelezo haya yameacha wengi na maswali zaidi. Natamani siku moja vyama hivi vikae kwenye TV LIVE, mada iwe ni kujadili itikadi za vyama mbali mbali, kuuza itikadi zao, na umma upate muda wa ku interact na wahusika - Nape, Mnyika, Mtatito, Mvungi,..., hakika mtabaini mapungufu mengi sana nayo yazungungumzia.
   
 18. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mkuu,unamkosea heshima mchambuzi...pamoja na kuwa mwana CCM amekuwa miongoni mwa watu makini kabisa humu jamvini!!!!
   
 19. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Mchambuzi

  Hakuna mtu anayekataa chama kuwa na itikadi yake ingawa sijakuelewa unaposema itikadi ipo tu hata bila kuwa na chama, ila nimesema kwa mazingira ya Tanzania leo kuanza kuhubiri itikadi kwa watu wenye njaa ni kujisumbua. Huwezi kwenda kijijini na kuanza kusema chama chetu kina mlengo wa kati wakati mwanakijiji anahitaji maji, anataka mbolea, ni sawa na kumlazimisha mgonjwa ale vyakula vya vitamini mbali mbali wakati hata ile hela ya kununulia mhogo hana. Lets have short-term plan (eradication of ufisadi) then we talk about idiology which i think need a long-term plan to build in people's mind.
   
 20. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  Masikini Mchambuzi niliposema wewe ni mwanazuoni wa siasa za vitabuni sikukosea inawezekana unasoma sana vitabu vya siasa na kusahau kuwa siasa hazina formula.

  Kuwa itikadi ya NCCR ni nzuri kuliko zote??? then how didi you come up with such a conclusion
  ?!!! ni baada ya kusoma mistari miwili mitatuys post ya Kahangwa?,and how do you know it is practical? may be am too weakto understand the real meaning of idiology. For your information hakuna chama kilichokuwa na itikadi na sera nzuri (practicable)kama CCM, hivi vyama vingine vinafanya kukopi na kupaste. Tatizo tulilonalo watanzania si itikadi wala sera ni viongozi na uongozi, waliopo si viongozi ni watawala hawana uchungu na mapenzi ya nchi kama wale wa kikoloni waliokuwa hawana uchungu na nchi zetu zaidi ya uchungu na maslahi yao. Ingekuwa viongozi au marais wanaazimwa tungeazima hata Rwanda tusiende mbali kwa wazungu aje atusaidie kwa sera na itikadi hizi hizi ndio maana kuna watu wanadiriki kusema tumpate rais dikteta angalau kwa miaka miwili hao nao si wajinga wameona tatizo lilipo.Tukiendelea kujidanganya tatizo ni itikadi inaonekana hatujui tatizo na itatuchukua muda mrefu sana kufika tuendako ingawa tutafika lakini tutakapofika majirani zetu Rwanda, Kenya, Sudani na wengine watakuwa mbali sana.
   
Loading...