Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,438
Masikini Mchambuzi niliposema wewe ni mwanazuoni wa siasa za vitabuni sikukosea inawezekana unasoma sana vitabu vya siasa na kusahau kuwa siasa hazina formula.
Kuwa itikadi ya NCCR ni nzuri kuliko zote??? then how didi you come up with such a conclusion?!!! ni baada ya kusoma mistari miwili mitatuys post ya Kahangwa?,and how do you know it is practical? may be am too weakto understand the real meaning of idiology. For your information hakuna chama kilichokuwa na itikadi na sera nzuri (practicable)kama CCM, hivi vyama vingine vinafanya kukopi na kupaste. Tatizo tulilonalo watanzania si itikadi wala sera ni viongozi na uongozi, waliopo si viongozi ni watawala hawana uchungu na mapenzi ya nchi kama wale wa kikoloni waliokuwa hawana uchungu na nchi zetu zaidi ya uchungu na maslahi yao. Ingekuwa viongozi au marais wanaazimwa tungeazima hata Rwanda tusiende mbali kwa wazungu aje atusaidie kwa sera na itikadi hizi hizi ndio maana kuna watu wanadiriki kusema tumpate rais dikteta angalau kwa miaka miwili hao nao si wajinga wameona tatizo lilipo.Tukiendelea kujidanganya tatizo ni itikadi inaonekana hatujui tatizo na itatuchukua muda mrefu sana kufika tuendako ingawa tutafika lakini tutakapofika majirani zetu Rwanda, Kenya, Sudani na wengine watakuwa mbali sana.
Mtindo unaotumia kuendesha huu mjadala ni ule wa kunivunja moyo, kwamba mwanazuoni, n.k, Lakini ningependa nikuhakikishie kwamba sitakufa moyo, nitazidi kueleza nayo yaona katika jamii yangu, na nipo tayari kuitwa chochote, mpaka siku wataalum au watu wenye heshima katika jamii watakapokuja yasema haya, kisha wana JF ku copy and paste habari za kwenye magazeti humu na kuanza kuunga mkono hoja.
Kwanza naomba tu niseme kwamba, angalau sasa unaelekea kuwa na uelewa kidogo juu ya wa umuhimu wa itikadi unaposema itikadi ya CCM ni more practical kuliko nyingine, na pia unaposema itikadi na sera za rwanda ni za kuigwa, ingawa mwanzo ulikuwa una discredit umuhimu wa itikadi kwenye vyama vyetu vya siasa Tanzania, na badala yake kuhimiza vyama kuendeleza mashambulizi kwenye yale yale ambayo nilishatolea ufafanuzi kwamba ni ya mpito, kwahiyo sitajirudia tena, kwani bado sijaona yakijibiwa kwa hoja, zaidi ya mifano ya hapa na pale. Ni dhahiri unayumba sana katika hoja zako, na hii inaniwia igumu kukufuatilia unalenga nini hasa.
Pia ningependa kusema kwamba haupo sahihi kuhusu CCM kuwa na the best itikadi, na pia haupo sahihi katika hoja yako kwamba rwanda can offer us mazuri ya kuiga, kwani hii ni a very dangerous approach, you are trying to take. Naomba sana uelewe maana ya itikadi. Hili suala sio la ku copy and paste. Hapo awali ulizungumzia kuhusu umuhimu wa kuto copy and paste yet, unatushauri hapa kufanya hayo hayo. Sasa tufuate nini, kauli zako au matendo yako? Kuhusu CCM na ubora wa itikadi na suala la Rwanda, haupo sahihi. Nitafafanua.
Kama ulipata nafasi ya kunisoma vizuri katika katika mada yangu nyingine titled: "Nape, Mnyika, Mtatiro: Wapi Itikadi Zenu", nina hoja kuu tatu:
1. Hoja ya kwanza, vyama vingi vya ya siasa Tanzania vina itikadi zao lakini haviendeshi siasa kufuatana na itikadi zao bali vinaendesha siasa kwa matukio pamoja na mambo ya mpito. Hili linafanya watanzania kushindwa kutofautiana katika ufuasi wa chama, based on core and unshaken values, na badala yake, 'in poverty, they unite.'
2. Hoja ya pili, pamoja na kuwa na itikadi zao, bado vyama hivi vina zina mapungufu ya wazi katika itikadi zilizopo kwani haziendani na uhalisia wa maisha ya watanzania walio wengi. Kwa mfano nikaelezea tatizo la itikadi ya uliberali chini ya CUF ambacho ni chama cha ukombozi. PiaNilitoa mifano mingi kuhusu watu wa vijijini, mijini n.k, wana mtazamo gani na maisha, wana spirit za aina gani, wanaitazamaje jamii inayowazunguka vis a vis ulimwengu, n.k, na kuyajadili haya katika mazingira ya itikadi za sasa katika vyama vyetu. Nazidi kuhimiza, elewa maana ya itikadi. Itikadi sio zao la chama cha siasa, bali itikadi ni zao la jamii kama ilivyokuwa chama cha siasa kuwa zao la jamii. Ukipata muda, naomba usome ile mada yangu, kwani utazidi kunielewa ili uwe katika nafasi nzuri zaidi ya kupingana na mimi kwa hoja, kwani hivi sasa hauna mtiririko ambao naweza kuufuatilia kwa makini, kwani hoja juu ya wazungu, wanyarwanda na itikadi na sera zao, unajichanganya sana kwa kweli. Wale ni wanyarwanda, sisi ni watanzania. Na naomba nizidi kusisitiza mawili. Kwanza, itikadi ni moyo, wakati sera ni damu inayosukumwa na moyo kusambaa mwilini. Usijichanganye na vitu hivi. Na pili, naomba sana nisisitize maana ya itikadi ili ujue kwamba haina chochote kinachohusu siasa, in its original format. Itikadi ni:
"Mtazamo, mwongozo, value system, spirit ya taifa, around which matukio na matendo yote ndani ya jamii revolves, hivyo kuimarisha maana, mwelekeo, na tafsiri ya masuala mbali mbali ya ulimwengu, kwa jamii husika."
Baada ya uelewa huu, ndipo vyama vya siasa hujaribu ku package aina mbalimbali za itikadi zilizopo miongoni mwa jamii, kisha kuzitengenezea sera, na kutoa ahadi kwamba vipo kwa ajili ya kupigania mtazamo, matarajio, spirit, etc, ya wanajamii husika. Hapo ndipo siasa huingia. Na just by logic,hapa utagundua kwamba ya Tanzania hayawezi kuwa ya Rwanda.
Naomba sana ubadili fikra kwamba itikadi ni kitu long term, kwani hata mtoto mchanga anapozaliwa, anazaliwa katika mazingia ya itikadi. Wazazi wake wanafanya maamuzi kiitikadi kuhusu malezi yake, na mipango yao ya baadae juu ya mtoto huyo. Na yeye akikua, anayapokea hayo. Tafadhali elewa kwamba hata kama dunia haina vyama vya siasa, itikadi ipo tu, hata kama ni jamii inayoishi porini kwa kutegemea jua, na matunda ya msituni. Modernity haileti itikadi, itikadi ni zao la jamii ya aina yoyote. Tenganisha suala hili na siasa kwanza, halafu ndio uingize siasa baadae, nadhani itasaidia upate uelewa vizuri.
3. Katika hoja yangu ya tatu, nikaelezea kwamba the future of this country ipo kweney social democrary, na nikaelezea kwanini.
Mwisho, umenishangaa sana kutojua itikadi ya NCCR mageuzi. Hii ilitakiwa iwe a wake up call for you kuelewa nini hasa maana ya hoja zangu. Otherwise, mimi kutojua itikadi ya NCCR kwa undani, ni suala lisilo kuwa na utofauti na utafiti wangu ule wa Arusha na Mbeya, kwani mimi ni sehemu ya umma, na inatakuwa niwe informed vizuri sana kuhusu core values za vyama mbalimbali, kazi ambayo ni ya idara za siasa na uenezi. Kwa sasa, idara hizi (chini ya CCM, CDM, CUF, NCCR etc), hazifanyi kazi zake vizuri kueneza itikadi zao, zinaacha itikadi kwenye vitabu, na badala yake kuendesha siasa a mpito kwenye magazeti kwenye vyombo vya habari. Nilishalifafanua hili katika nyakati mbalimbali.
Na mwisho, naomba usinidanganye mimi na wanachama wengine wa CCM kwamba CCM tuna itikadi practicable. Ni muhimu utambue kwamba Marxist - Leninist Socialism has discredited itself. Ni miaka zaidi ya 20 sasa. Otherwise, msimamo wangu ni kwamba - Ujamaa wa Kidemokrasia (Democratic socialism), offers the best package for CCM, CUF, CHADEMA, NCCR Mageuzi, etc, if kweli they desire to uplift majority of Tanzanians from abject poverty. Bila ya hivyo, vyama vyote vitakuwa vinapigaan vikumbo kukimbilia Ikulu kwenda kuwa watekelezaji wazuri zaidi wa sera zile zile za soko huria bila mchujo, zinazolazimishwa kwetu na IMF na WorldBank, sera ambazo kwa kiasi kikubwa ni sababu ya umaskini wetu. Chama chochote kitachoshinda uchaguzi katika mazingira haya kitanyang'anywa tonge lake mdomoni ndani ya miaka michache sana, na nilishafafanua hili.
Utatuzi wa umaskini Tanzania utakuwa ni matokea ya a radical orientation ya ki-itikadi, nje ya mengi ambayo yapo katika vyama vingi vya siasa vya sasa.