Ni mwaka wa tatu naota nywele zinaniota mdomoni

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,071
Bandugu wana JF,

Nimekuwa naota ndoto ambayo mara nyingi inanipa shida nikiwa ndotoni kwani Mara kadhaa naota nina ndevu/nywele kwenye fizi zangu. Tabu ninayoipata ni kurudia rudia kwa ndoto na hasa usumbufu ninaoupata ndotoni pale ninapojaribu kuzing'oa nywele hizo.

Naomba wataalam wa mambo haya wanitafsirie ndogo hii.
 
Tafuta binaural beats music hakika utapona tatizo hilo. Ukipata Music wenye Alpha beat nakuhakikishia utapona. Ukipona uje utoe ushuhuda hapa.
 
Hiyo ndoto simpo sana mkuu na maana ni hii: muda si mrefu utakuwa kinyozi na hizo nywele zinazokuota mdomoni ni nywele za wateja wako zitakazokuwa zinaingia mdomoni mwako kwa bahati mbaya.
;);););)
 
Bandugu wana jf, nimekuwa naota ndoto ambayo Mara nyingi inanipa shida nikiwa ndotoni kwani Mara kadhaa naota Nina ndevu/nywele kwenye fidhi zangu. Tabu ninayoipata ni kurudia rudia kwa ndoto na has a usumbufu ninaoupata ndotoni pale ninapijaribu kuzing'oa nywele hizo.
Naomba wataalam wa mambo haya wanitafsirie ndogo hii. Sitaki majibu ya dhihaka kama huna mchango Baki kama msomaji
Jaribu kuwa mchunguzi. Unapoota unakuwa kwenye hali gani eg unakuwa na homa inakunyemelea? Ndoto nyingi za aina hii zinaashiria mwili wako uko kwenye hali fulani. Kwa mfano mimi ninapoota natembea kwenye sehemu yenye kinyesi na mwili unasisimuka lazima nitapata homa siku mbili zitakozofuata. Naomba usidanganyike na kuambia sijui zinaashiria mambo fulani ya imani au ushirikina. Mara nyingi ndoto kama hizi zinakuwa ni matokea ya mwili wako kuwa kwenye hali fulani
 
Dehydration, uwe unakunywa maji mengi before sleeping. Mdomo ukiwa mkavu ukiwa upo Usingizini hiyo hali utaipata, wengine huota wanakula chakula kikavu
 
Nashukuru kwa mchango wako.
 
Dehydration, uwe unakunywa maji mengi before sleeping. Mdomo ukiwa mkavu ukiwa upo Usingizini hiyo hali utaipata, wengine huota wanakula chakula kikavu
I will make investigation Mkuu.
 
Uko dar nenda kanisa la eagt mtoni mtongani kwa pastor katunzi,liko karibu na reli inakatisha barabara hapo utapona kwa maombi bure kabisa.imsure.
 
Hiyo ndoto simpo sana mkuu na maana ni hii: muda si mrefu utakuwa kinyozi na hizo nywele zinazokuota mdomoni ni nywele za wateja wako zitakazokuwa zinaingia mdomoni mwako kwa bahati mbaya.

Mh hebu fafanua vizur yan nywele Za,wateja Inamana atakuwa kinyoz au.
 
Bandugu wana jf, nimekuwa naota ndoto ambayo Mara nyingi inanipa shida nikiwa ndotoni kwani Mara kadhaa naota Nina ndevu/nywele kwenye fidhi zangu. Tabu ninayoipata ni kurudia rudia kwa ndoto na has a usumbufu ninaoupata ndotoni pale ninapijaribu kuzing'oa nywele hizo.
Naomba wataalam wa mambo haya wanitafsirie ndogo hii. Sitaki majibu ya dhihaka kama huna mchango Baki kama msomaji
Ndoto zina maana nyingi ndugu ramea, hata ukisoma vitabu vitakatifu vinazungumzia mengi kuhusu ndoto hasa pale wafalme na manabii walipokuwa wanapewa ujumbe na Mwenyezi MUNGU kupitia ndoto.
mfano ni farao wa misri alipoota ng'ombe saba waliokonda wakawameza ng'ombe saba walionona alishindwa kuielewa ile ndoto hadi alipoitwa yusuph akamueleza maana ya ile ndoto na kweli yale mambo yakatimia.
Hiyo ndoto yako sio ya kawaida sababu umeota vitu viwili visivyokuwa na mahusiano vikiwa sehem moja yani mdomo na nywele na imekuwa ikijirudia hiyo ndoto.
Kama we ni Mkristo kawaone wachungaji au mapadri wenye maono ya MUNGU watakusaidia pia kama ni muislam kawaone viongozi wako wa dini wenye maono watakusaidia kujua ukweli.
Mwenyezi MUNGU anawasiliana na watu wake kwa njia nyingi sana ikiwemo ndoto, magonjwa, ulemavu, viongozi wa dini.
Pia kama unajua kuna jambo baya unalolifanya halimpendezi Mwenyezi MUNGU ni wakati wako kuacha na pia sali sana MUNGU atakusaidia kuelewa maana ya hiyo ndoto unayoota na kujirudia.
 
Inawezekana kabisa unampango wa ku-rationalize denominator ya mdomo wako na among one of your excretory parts..... Just kidding though, watalaam watakuja hapa soon kuelezea kiufasaha zaidi so let's be patient and wait...
 
Tafuta binaural beats music hakika utapona tatizo hilo. Ukipata Music wenye Alpha beat nakuhakikishia utapona. Ukipona uje utoe ushuhuda hapa.
hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa umenifanya nicheke sana kweli jf kuna mamb
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom