jsenyinah
JF-Expert Member
- Jan 25, 2012
- 249
- 339
NI MWAKA SASA, USINGIZI HUJA KUANZIA SAA 8 USIKU NA UNAKATA SAA 11 ALFAJIRI.
Kichwa cha habari hapo juu chajieleza.
Ni miezi isiyopungua kumi na tatu (13) sasa,hata niwe nimechoka vipi, hata niwahi kulala vipi , usingizi wangu huanza kuja kuanzia saa nane (8) usiku na hukatika saa 11 alfajiri. Nimejitahidi kujilaza mapema lakini wapi,ngoma tight.Ni tofauti na huko nyuma ambako ilikuwa nikidondoka kitandani saa 3 usiku, saa 4 haifiki ninakuwa nimeanza kukoroma na kuota ndoto tamu tamu.
Siku hizi hata hayo masaa machache ninayolala (tuite kupumzika), naota ndoto ngumu, chungu, za hasira na za uwoga sana.
Muda wote huo ninapokuwa macho, nachukua simu yangu na kuanza kuperuzi habari, matukio mitandaoni.Hii n kwasababu macho huwa makavu kabisa, kama asubuhi ya saa 4.
Naombeni ushauri ndugu zangu.Ni nn hiki kinasababisha nakosa hii raha namba 1 duniani.
Asanteni sana.