Ni mwaka sasa, napata usingizi saa 8 usiku na naamka saa 11 alfajiri.Ndoto ninazoota ni ngumu

jsenyinah

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
249
338
NI MWAKA SASA, USINGIZI HUJA KUANZIA SAA 8 USIKU NA UNAKATA SAA 11 ALFAJIRI.

Kichwa cha habari hapo juu chajieleza.

Ni miezi isiyopungua kumi na tatu (13) sasa,hata niwe nimechoka vipi, hata niwahi kulala vipi , usingizi wangu huanza kuja kuanzia saa nane (8) usiku na hukatika saa 11 alfajiri. Nimejitahidi kujilaza mapema lakini wapi,ngoma tight.Ni tofauti na huko nyuma ambako ilikuwa nikidondoka kitandani saa 3 usiku, saa 4 haifiki ninakuwa nimeanza kukoroma na kuota ndoto tamu tamu.

Siku hizi hata hayo masaa machache ninayolala (tuite kupumzika), naota ndoto ngumu, chungu, za hasira na za uwoga sana.

Muda wote huo ninapokuwa macho, nachukua simu yangu na kuanza kuperuzi habari, matukio mitandaoni.Hii n kwasababu macho huwa makavu kabisa, kama asubuhi ya saa 4.

Naombeni ushauri ndugu zangu.Ni nn hiki kinasababisha nakosa hii raha namba 1 duniani.

Asanteni sana.
 
Smartphone zinasababisha ukose usingizi
Sasa nakushauri Fanya mazoezi jion utachoka so utalala mda mrefu angalau hata uhakikishe unalala masaa 7
 
Wewe ni dini gani?kama sio mpagani. Chukua kitabu cha dini yako uanze kukisoma muda unaotaka kulala,iwe saa mbili au tatu,nne(ni dawa tosha ya usingizi maana shetani ataona ukiendelea kukisoma atapoteza mfuasi hapo hivyo bora usafiri ndotoni tu)
 
Samahani mkuu,nijibu yafuatayo tuweze kupata pakuanzia..
1. Umetoka jela hivi karibuni?
2. Kuna tukio umefanya la hatari kiasi kwamba una mashaka mashaka?
3. Una familia na umefukuzwa kazi au biashara haziendi vema?
4. Kuna mwanamke\mwanaume uliyempenda sana na mmeachana au kaku dissapoint kwa namna yyte ile?
5. Unawachukia sana wasukuma? Maana miezi 13 ni sawa kabisa na umri wa madaraka wa Ngosha.

Embu angalia kama Upo ktk category yyte hapo nione namna ya kuanza kukushauri mkuu.
 
hakuna jibu sahihi
 
Hyo mimi iliwahi kunitokea miaka kadhaa iliopita....na nliteseka saaana....na nlikuja kuoneshwa dawa ambayo sikutegemea kama ntapona

Kama ww ni muislamu chukua karatasi nyeupe andika suratul falaq tatu kwenye karatasi kisha loweka kwenye maji halafu baada ya muda nawa kichwani maji yale na mengine kunywa BI IDHNILLAH Utapona tatzo hlo....mimi halikuchukua week ALHAMDULILLAH MPKA leo nipo swaaaafi
 
Hapa naona una pressure mwilini kwako (HBP) hicho ndio chanzo kikuu cha hizo ndoto! Baadhi ya mishipa ya fahamu inakuwa kwenye mgandamizo na yote hayo hutokea! Jitahidi kila uamkapo kabla ya chochote unywe maji lita moja na nusu baada ya week tuwasiliane
 
Lita na nusu chai mkuu?We n mganga wa kienyeji?
 
NI MWAKA SASA, USINGIZI HUJA KUANZIA SAA 8 USIKU NA UNAKATA SAA 11 ALFAJIRI.

Kichwa cha habari hapo juu chajieleza.

Ni miezi isiyopungua kumi na tatu (13) sasa,hata niwe nimechoka vipi, hata niwahi kulala vipi , usingizi wangu huanza kuja kuanzia saa nane (8) usiku na hukatika saa 11 alfajiri. Nimejitahidi kujilaza mapema lakini wapi,ngoma tight.Ni tofauti na huko nyuma ambako ilikuwa nikidondoka kitandani saa 3 usiku, saa 4 haifiki ninakuwa nimeanza kukoroma na kuota ndoto tamu tamu.

Siku hizi hata hayo masaa machache ninayolala (tuite kupumzika), naota ndoto ngumu, chungu, za hasira na za uwoga sana.

Muda wote huo ninapokuwa macho, nachukua simu yangu na kuanza kuperuzi habari, matukio mitandaoni.Hii n kwasababu macho huwa makavu kabisa, kama asubuhi ya saa 4.

Naombeni ushauri ndugu zangu.Ni nn hiki kinasababisha nakosa hii raha namba 1 duniani.

Asanteni sana.
Hata kama hukutaka Rais Magufuli awe Rais ndiyo Rais tena wewe endelea na kazi zako kama ni halali na siyo halali hautapata huo usingizi.

Rais anachotaka yeye ni wewe kufuata sheria na kufanya kazi au biashara zako tu.

Subiri 2020 tena umchague umpendaye na kama atapita.

Pole sana na ukikosa usingizi kwa muda mrefu unaweza kupata madhara kiafya.
 
Smartphone zinasababisha ukose usingizi
Sasa nakushauri Fanya mazoezi jion utachoka so utalala mda mrefu angalau hata uhakikishe unalala masaa 7
Hili usemalo ni kweli,hata mimi kuna kipindi nilijiendekeza sana na smart phone,nilikuwa almost silali kabisa na kibaya zaidi hata macho yangu yakapunguza uwezo wake wa kuona.Lakini niligundua pia kuwa kulala peke yako ni moja ya sababu kubwa na pili ni stress zikikubana vizuri na ukaziendekeza lazima uteseke na hiyo shida,pole sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom