Ni muhimu kumuogezea kiongozi mkuu ulinzi wa uhakika zaidi kwakuwa adui kadhamiria kutenda maovu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Mchakato wa kumpata mkuu wa nchi ni mchakato wenye gharama kubwa. Na anapopatikana mmoja basi jukumu kubwa la kwanza ni afya yake na ulinzi wake!

Kama vile hakuna binadamu anayekosa rafiki, vilevile hakuna binadamu anayekosa adui na rais wa nchi si malaika wala kizuka.. Rais ni binadamu hivyo hata awe mwema vipi hawezi maadui kwakuwa hawezi kuwafurahisha wote ukiachana ma wale 'natural haters' chuki bila sababu!

Kila awamu mpya ya mtawala yeyote yule huja na miongozo mipya ambayo huweza kuathiri makundi fulani kwenye jamii. Athari hizo huwa za matokeo hasi ama chanya! Kuna makundi faidika ambayo huwa kwenye kila awamu ya utawala. Ni makundi haya ambayo awamu ya utawala inapobadilika huwa kwenye hatihati ya kuendelea kula bata kama mwanzo! Haya makundi ndio huwa hatari sana kwa awamu mpya hasa yakiona yanatengwa na kuwekwa pembeni.

Mabadiliko ya kiutawala ngazi ya juu yalitujia kwa ghafla na bila kutarajia na ni katiba pekee iliyosimamiwa kikamilifu ndio iliokoa dhahama kubwa! Lakini ni wazi kuna kundi kwa maslahi binafsi lilitaka kupindua meza. Tuhuma hii haijawahi kukanushwa wala kuthibitishwa popote na yoyote! Imebaki kuwa minong'ono yenye asili hai na inayozidi kupata nguvu kila uchao.

Mabadiliko ya kiutawala yameligusa vilivyo kundi tuhumiwa. Ni wazi halifurahishwi hata chembe na yanayoendelea kwasasa.. Kuna hisia za mapinduzi makubwa yanayofanywa na awamu mpya. Na mapinduzi haya ni mwiba mkali kwa makundi faidika ya utawala ulopita.

Kwenye cycles za ulinzi wa viongozi wakuu kuna cycles kama sita au saba hivi
  • Ulinzi wa kisayansi na kielectroniki
  • Ulinzi wa usalama wa nchi
  • Ulinzi wa majeshi
  • Ulinzi askari polisi
  • Ulinzi wa jeshi la akiba
  • Ulinzi wa kiroho
  • Ulinzi wa askari kanzu na maafisa vipenyo
Hizi cycles zote huchujwa kwa umakini na weledi wa hali ya juu mno kwakuwa kwa saa 24, siku saba za wiki na miezi 12 ya mwaka ndio zinahusika na afya na ulinzi wa kiongozi mtawala mkuu.

Kwa hali hii kama si kuboresha basi ni muhimu kumuogezea kiongozi mkuu ulinzi wa uhakika zaidi kwakuwa ni kama vile adui kadhamiria kutenda maovu ama kukwamisha juhudi chanya za uongozi wa awamu mpya.
 
Vipi tena mkuu!
Wewe hukubaliani na wenzako kwamba mama hataki mbwembwe

Maana mavifaa yote ya mwendazake yalikuwepo kwemye msafara, badala yake ilionekana mwendazake anafaidi,ila amama anatakiwa anongezewe zaidi.
 
Vipi tena mkuu!!
Wewe hukubaliani na wenzako kwamba mama hataki mbwembwe

Maana mavifaa yote ya mwendazake yalikuwepo kwemye msafara,badala yake ilionekana mwendazake anafaidi,ila amama anatakiwa anongezewe zaidi.
Hii ni dhana pana zaidi na ulinzi si lazima uwe na mbwembwe za misafara mikubwa na migari yenye mitambo ya mawasiliano kila kona
 
Tatizo hamchelewi kubadilika. Leo hii wengi mnakubaliana na utawala wa mama na kufikia hatua ya kumuombea ulinzi zaidi, siku atakayoibuka mbeleji kumchafua bimkubwa na nyinyi mtarudi tena kuungana nae kumchafua mama.
 
Tatizo hamchelewi kubadilika. Leo hii wengi mnakubaliana na utawala wa mama na kufikia hatua ya kumuombea ulinzi zaidi, siku atakayoibuka mbeleji kumchafua bimkubwa na nyinyi mtarudi tena kuungana nae kumchafua mama. We subiri tu maana mbeleji na genge lake hawana jema.
Kutoa ushauri tu ndiyo kukubaliana!! Na huyo Mbeleji mbona unamuogopa sana? Mbeleji 🥵
 
Tatizo hamchelewi kubadilika. Leo hii wengi mnakubaliana na utawala wa mama na kufikia hatua ya kumuombea ulinzi zaidi, siku atakayoibuka mbeleji kumchafua bimkubwa na nyinyi mtarudi tena kuungana nae kumchafua mama. We subiri tu maana mbeleji na genge lake hawana jema.
Hizi sio enzi za mwendazake za siasa za chuki na visasi na si kila wakati ni kukosoa penye kuhitaji pongezi nitafanya hivyo bila kuhofia chochote
 
Tatizo hamchelewi kubadilika. Leo hii wengi mnakubaliana na utawala wa mama na kufikia hatua ya kumuombea ulinzi zaidi, siku atakayoibuka mbeleji kumchafua bimkubwa na nyinyi mtarudi tena kuungana nae kumchafua mama. We subiri tu maana mbeleji na genge lake hawana jema.
Sisi tupo huru Sasa Huo ujinga wenu wa kuteka na kuua binadamu bila hatia ndio umekufa na mwendazake..shubamit
 
Back
Top Bottom