Ni muda wa Jeshi la Polisi sasa kubadilika,enendeni na wakati uliopo

mandella

JF-Expert Member
Oct 29, 2011
3,048
3,227
Jeshi la Polisi naomba niwambieni Jambo.
Je mnafahamu hii Dunia inakwenda kasi sana ? Tambueni Technolojia inakua kwa kasi ya ajabu sana,Elimu ya Uraia inatolewa kwa kiwango kikubwa sana na Serikali,Taasisi na hata watu Binafsi,tambueni Elimu hizi zinaabadilisha fikra za watu juu ya kuzifahamu haki zao.

Kwa hayo naomba niwaambie acheni kuendelea kuishi KIMAZOEA.
Acheni kuomba Rushwa kimazoea,acheni kubambikiza watu kesi kimazoea,acheni kunyima watu dhamana kimazoea.Mambo haya ya kimazoe kwa nyakati hizi ni kwamba tumekua tukiona nyendo nyingi za kesi mnazushuhulikia Matokeo yake ni ya Aibu na fedhea kwenu,na hii ni kwajili tu ya kuwa Nyakati ZIMEBADILIKA.

Na niwambie tu Suala la Nyakati litawarudisha kwenye mstarii mnyoofu,Trustme ,Kwa hali inavyokwenda Wananchi wengi wametoka uwoga kabisa na wamekataa kuonewa kama ilivyokua awali, Wananchi wengi wamepata japo elimu kidogo Juu ya maswala ya Haki zao za msingi.

Itafika mahala Automatically tu Polisi hawataweza kumnyima mtu dhamana bila sababu za msingi,
itafika mahala polisi hatoweza kumuweka mtu ndani kwa kesi za kubambikiza ,itafika mahala hakuna Polisi ataweza kumuweka mtu ndani kiholela bila kufuata PGO,na itafika mahala swala kupata Ushahidi halitafanikiwa Bila Police wenye uweledi,Elimu na Wenye Kutenda haki.

Itafika mahala tu , Ipo Siku.

Polisi walizoe mambo ambayo watu wengi kwa sasa wanaona ni kawaida,Walizoea wakishakukamata basi huna haki,walishazoea swala la kuomba Rushwa ni haki na ni halali kwao , Watu wamebadilika sana.

Kama Mama,mnajitaji kujichunguza na kujitathmini,Mambo ya Kimazoea hayapo tena.

Nimezungumza haya baada ya kuona Kesi mbali mbali zinazoendelea zikiwa zinawaendeeni Vibaya.

Tizama Kesi ya Mbowe ilivyokwenda , Tizama kesi Ya Kijana wa Mtwara, tizama Kesi ya Vijana wa Mange Kimambi. Zipo kesi nyingi sana.

Embu epukeni fedheha na aibu kwa kutambua jambo Dogo tu , NYAKATI ZIMEBADILIKA

Mwisho niwape Kongole kubwa sana kwa Askari polis {wachache} wanaotimiza majukumu yao wakizingatia Haki na kufuata taratibu na misingi ya sheria.

Na huo ni Upendo wangu wa kweli kwenu.
 
Back
Top Bottom