Ni mtoto yupi mjinga zaidi ya mwenzake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mtoto yupi mjinga zaidi ya mwenzake?

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Shine, Apr 21, 2012.

 1. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  [h=6]Wazee wawili walikuwa kwenye ubishi mkali kila moja akitetea kuwa mwanae ndie mtoto mjingakuliko wote duniani, ubishiukawa mkali mwishowe mzee mmoja akamwita mwanae, 'We ngeli njoo' , mwanae akaja mzee akamwambia,'Heb u nenda pale kazini kwangu kanicheki kama nipo, ikiwa utanikuta nambie nirudi nyumbani kuja kula sawa...?', mtoto akajibu sawa akaondoka mbio. Yule mzee wa pili nae akamwita mwanae 'Jelo njoo' mwanae akaja, 'Mwanangu chukua hizi noti mbili za alfualfu, hii alfu moja kaninunulie gari, hii nyingine kaninunulie Blackberry sawa?' Sawa baba' Mtoto akatimka. Njiani ile mitoto ikakutana wa kwanza akaanza 'Baba mjinga kweli eti kanituma nikamuangalie kama yuko kazini, si angepiga simu tu wangemwambia kama yuko au hayuko', wapili akajibu, 'Si heri ujinga wa babako, mimi babangu kanipa noti mbili nikamnunulie gari na simu, sasa eti wala hajanielekeza noti ipi ninunue gari na noti ipi ninunue simu kama si ujinga ni nini hicho![/h]
   
 2. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  nimeshaileta hii tangu jana mkuu
   
 3. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,799
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kwahiyo mambo ya ''hati miliki'' sio? Usikonde Dr. Nchimbi kahaidi wkt wa mazishi ya Kanumba wizi huo mwisho June Mwaka huu.
   
Loading...