~**~ Ni Msemo wa Kikwetu ~**~

Kweli limetulia, ndugu hongera sana, maana dunia ya leo mh vipaji haba watu wanariti kazi za wazazi, ila nadhani wewe hujarithi. Tupage siku moja moja humu!
 
Mwanakijiji karibu, Jukwaa mahusiano,
Upate yetu mahabu, Siasa ni migongano,
Watakuvuta sharubu, Raha upate mswano,
Jukwaa mahusiano, Hapa ni kwako nyumbani.

Siasa ni kitu gani, Kichwa wajiumizia,
Mapenzi ni yako fani, Hakika umebobea,
Njoo tupe burudani, na hekima yako pia,
Mapenzi mahusiano, Jukwaa lakuhitaji
Xpin umejuaje tena??!
 
Mwanakijiji karibu, Jukwaa mahusiano,
Upate yetu mahabu, Siasa ni migongano,
Watakuvuta sharubu, Raha upate mswano,
Jukwaa mahusiano, Hapa ni kwako nyumbani.

Siasa ni kitu gani, Kichwa wajiumizia,
Mapenzi ni yako fani, Hakika umebobea,
Njoo tupe burudani, na hekima yako pia,
Mapenzi mahusiano, Jukwaa lakuhitaji
Hapa sasa naona Shaaban Robert atafufuka sasa hivi kukupa mkono kwa niamba ya manguli wenzie wa lugha alafu arudi kupumzika.
 
Na usipopenda je pale unapopendwa?sometimes huwa tunapendwa lakini mioyo huwa haitaki lakini pia huwa tunapenda pael tusipopendwa.
 
Asante mwanakijiji Umetukumbusha mbali na kutukuna patamu na kwa wale waliopitiiwa na baadhi ya maneno naimani hawato sita kutaka kujuvywa.(kila muonja Asali Haonji Kwa Mara Moja, na Mpenda chongo huita Kingeza.
 
Mapenzi ni kama homa, yanahitaji tabibu,
Moyo wako wasimama, hadi aje wa muhibu,
Ni dawa iliyo njema, tangu enzi za mababu,
Penda pale unapendwa, ni msemo wa kikwetu!!

hongera zako mkuu duu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom