Ni mila zipi za kabila lingine uliwahi kukutana nazo zikakushangaza

Bibi yangu aliwahi nihadithia kuwa wao (wanyaturu) zamani zile kama mwanaume amerudi kutoka kunywa pombe anahasira basi mke anachukua kigoda anakaa uwani anapigwa weeeeee hadi mwanaume hasira ziishe then maisha yanaendelea.
Nimecheka km chizi haki ya nani
 
Bibi yangu aliwahi nihadithia kuwa wao (wanyaturu) zamani zile kama mwanaume amerudi kutoka kunywa pombe anahasira basi mke anachukua kigoda anakaa uwani anapigwa weeeeee hadi mwanaume hasira ziishe then maisha yanaendelea.
Duuuh ukipata ukilema je kwa kipigo
 
Teh wasukuma wana vituko sana. Wasukuma hasa wanyantuzu mwanamke akifariki wakati wa kujifungua wanawake wanachuma fimbo na kuanza kutembea barabarani ole wake wakutane na mwanaume atakula viboko vya kutosha.
Wanadai bila mwanaume huyo mama asingefariki (asingepata mimba)

Safi sana wanawake wa Kinyantuzu. Hii mila ienezwe isibaki huko huko au kuachwa ife.
 
Wasukuma bwana..... kukiwa na sherehe hasa zile za kilimo wakati wa chakula ni ugali kwanza unatangulia, watu wanakula na kushiba halafu wali unafuatia. Yaani kwao wali ni mboga tu, ukiwapa wali na ndizi au nyama wanasema MBOGA KWA MBOGA.
So ukishiba ugali ndio basi tena wali unaishia kuuangalia?
 
Hahahaha! Tuvumilie Mkuu ila hata mie inanikera sana, siku moja miaka ya nyuma tulienda kulima kwa jamaa kwa kutumia ng'ombe sasa muda Wa chakula cha mchana wakaleta ugali na hawaonyeshi dalili ya wali, watu tukapiga ugali dadeki kumbe wali umepikwa asubuhi ili tusigundue kuwa kuna wali, yaani watu wameshiba ugali halafu wanaleta wali.
Ni ugali mtupu bila mboga hata kidogo au ni vipi
 
Teh wasukuma wana vituko sana. Wasukuma hasa wanyantuzu mwanamke akifariki wakati wa kujifungua wanawake wanachuma fimbo na kuanza kutembea barabarani ole wake wakutane na mwanaume atakula viboko vya kutosha.
Wanadai bila mwanaume huyo mama asingefariki (asingepata mimba)
Kila mwanaume anachapwa aiseee so hiyo hali ya kutembea na fimbo ni kwa muda gani
 
Kwa mtu wa kawaida asie mzoefu atashindwa kuendelea kula wali, maana atakuwa kesha shiba. lakini wao wanapakia tu, sijui hawashibagi! Wenyewe wanakuambia wali ni kishushio tu hauna nguvu mwilini.
Na huo ugali ni mtupu kabsa au una vimboga kidogo
 
Na huo ugali ni mtupu kabsa au una vimboga kidogo
Wasukuma kwenye chakula hawajinyimi. Hapo kama kuna shughuli lazima ng'ombe au mbuzi achinjwe, Nyama kwa sana. huwa wananifurahisha sana kwenye maakuli. Unakula nyama hadi unazichoka, au samaki hadi unakimbia. Wasichojua ni kuunga mboga! Nyama inachemshwa tu na kuliwa bila viungo (yaani wanakula ugali, mboga ni supu).
 
Kuna jamaa wa mkoa wa mara ,mtu mzima kakaake akisafiri analala chumbani kitanda kimoja na mke wa kakaake .anadai kawaida bro akirudi namba shida.hii ilikuwa 1990s
 
Wasukuma kwenye chakula hawajinyimi. Hapo kama kuna shughuli lazima ng'ombe au mbuzi achinjwe, Nyama kwa sana. huwa wananifurahisha sana kwenye maakuli. Unakula nyama hadi unazichoka, au samaki hadi unakimbia. Wasichojua ni kuunga mboga! Nyama inachemshwa tu na kuliwa bila viungo (yaani wanakula ugali, mboga ni supu).
Baada ya msosi huo wa nguvu unaletewa wali si utavimbiwa jamani
 
Back
Top Bottom