Jindal Singh
JF-Expert Member
- Sep 9, 2015
- 1,857
- 1,538
Wadau nimeamua kuandika huu uzi ili watu wajaribu kutumia njia ya kupeleka mamilioni bank bila kuibiwa. Kunajamaa kaniajili kumpelekea pesa zake bank kila wiki, ni tajiri mmoja wa size ya kati. Kuna njia moja ambayo nilikuwa naipenda kuitumia wakati ninapokwenda ofisini mwake kuchukua pesa yaani nilikuwa najifanya ni fundi magari mkononi nikibeba dumu la oil na nikitupia ovaroli. Ofisini kwake bosi kuna vijana wanaofanya kazi ya kubeba mizigo huwa washanizoea kama fundi kumbe mimi huwa na mambo yangu mda mwengine napitaga na hadi 50m ndani ya dumu la oil, ila kwa sasa nishachana na kazi ya kumnufaisha mtu na kuhatarisha maisha. Kwa hiyo wafanyabiashara mnaposafirisha pesa tumieni akili nyingi na kuweni makini na watu mnaofanyanao kazi.