Nilikuwa Kitendaguro kwa wakwe zangu hivi karibuni na nikazunguka mji wa BK kwa siku 10 nilizokuwa pale!Kama niliyo yaona kwenye mji ule ndiyo Waziri Kagasheki anasifiwa kama kabadili mji basi wakwe zangu wana hali mbaya sana kimaisha!
BK hamna barabara nzuri,hamna maji ya uhakika,umeme kwa siku 10 nilizokaa pale ulikatika zaidi ya mara 11,BK hawana kiwanja kizuri cha ndege;meli zinazokuja BK toka Mwanza ni kuu kuu;BK nauli za ndege mlala hoi huwezi himili na huduma za matibabu nilijionea mwenyewe nilipompeleka mwanangu kwenye hospital ya mkoa ni kichekesho kabisa;shule za BK majengo yake ni hovyo kabisa na mengineyo mengi!
Wilaya ya Kyela ninapotoka iliyoko nje sana ya Mkoa wa Mbeya ni afadhali mara 100 kwa maendeleo kuliko jimbo la BK lililoko ndani ya makao makuu ya Mkoa Kagera!
asante sana shemeji yetu,umeandika ukweli,na kwa kawaida waafrika hatupendi kuambiwa ukweli pale inapofika ukosoaji!