Ni mbunge gani ktk mkoa wa Kagera atarudi 2015?

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,927
2,000
Mbali na jimbo la B'mulo ambapo kuna lile jembe letu (CDM) Sioni mbunge mwingine anaeweza kurudi mjengoni. Chato ya Magufuri imechomolewa mkoani Kagera imerudi Geita. Mwenye kuona mwenye mwelekeo atuwekee hapa.
 
Greard

Member
Dec 23, 2010
64
95
Charles Mwijage Ingawa yuko kwenye chama cha magamba lkn katimiza ahadi nyingi pamoja na jitihada zake dhidi ya wahamiaji haramu toka Rwanda
 
Tiger One

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
568
500
Mwijage hana jipya ni mtu wa masifa na kujipaisha tu. Ndo mbunge wa kwanza kupigwa mawe jimboni kwake. Hawezi kurudi mjengoni yule.
 
mwabakuki

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
266
195
Mbali na jimbo la B'mulo ambapo kuna lile jembe letu (CDM) Sioni mbunge mwingine anaeweza kurudi mjengoni. Chato ya Magufuri imechomolewa mkoani Kagera imerudi Geita. Mwenye kuona mwenye mwelekeo atuwekee hapa.

Ndg hawa nsomile wote wameshaangukia pua hata kabla ya Uchaguzi
Mh.Katagrira- Kyerwa (ccm), labda kwa muujiza, nadhani huyu ni mahtuti kuliko wote, juzi kazomewa jimboni
Blandes - Karagwe (ccm),, huyu alipata ubunge wa mezani a.k.a mchakachuaji...mara hii zitapigwa na kulindwa no wizi
Mshama - Nkege (ccm),, huyu kwanza darasa la nane, anasubiri tsunami tu... namsihi asithubutu kupoteza muda wake
Ntukamazina - Ngara (ccm), Huyu yuko ICU siku nyingi tu na inavyoelekea ashajikatia tamaa, kazi kweli kweli
Kagasheki - Bkb mjn(ccm)- cjui atachomokea wapi. nadhani hata umri hauko upande wake kabisa
Rweikiza - Bkb vjjn (ccm), huyu alichaguliwa kwa bahati tu,, 2015 bahati haina nafasi tena,, ni uwezo tu
Mwijage - Muleba Kaskazini (ccm), huyu mbwembwe zake pale mjengoni zinamfanya aonekane katuni mbele ya wananchi
safari yake inaishia 2015, akalime kahawa.
Prof. Tibaijuka - kutotimia kwa ahadi alizotoa ni kikwazo kikubwa sana kwake

Sababu mbaya zaidi inayowaathiri wote ni chama walichopo..hakichaguliki kabisa..

nawatakia kila la kheri ktk safari yao kuelekea 2015... mwenye hekima atangaze mapema kutoshiriki uchaguzi 2015
 
Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,325
0
ndg yangu yangu haya ndo moja ya mambo yanayowafanya watu wawadharau... wenzio tunajadili mambo ya msingi we unakuja na luga ambazo hazieleweki..tumia lugha ambayo watz wengi tutakuelewa.
Nina maana......we niache.....i know exactly what i am doing....anyway ciao na karibu mmu.
 
Bunsen Burner

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
630
1,000
ndg yangu yangu haya ndo moja ya mambo yanayowafanya watu wawadharau... wenzio tunajadili mambo ya msingi we unakuja na luga ambazo hazieleweki..tumia lugha ambayo watz wengi tutakuelewa.
Ndo tatizo lingine la nshomile hakawii kutune external service service kushaua nakusahau kupeleka maendeleo na kusifia ,naishi Dar bwana wakati kimji cha bukoba kichovu huwezi amini ndipo nshomile wanatokea! Aaaaarg....... badillikeni!
 
rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,927
2,000
Nashindwa kuamini kabsa maana pamoja na uelewa wa hawa watu lakini wameshindwa kabisa kutuletea idadi kubwa ya wapambanaji... Matokeo yake Kigoma mwanza na musoma wamefanya vizuri sana. Hii hali inatisha.
 
kevin nathan

Member
Apr 20, 2012
20
0
sioni kama nyote mnaochangia ili kama mna akili nzuri yaan taifa lipo kwenye misukosuko mingi mnaleta ukabila eti karne hii, acha hizo bwana, huyo naye sema bukoba imechoka kairinganisha na mkoa gani au wilaya gani? niambie bukoba maendeleo yaliyoko utayalinganisha na tarime, au mtwara au musoma, au kigoma ,au iringa, au babati au chalinze au songea au singida au taboraaa, au shinyanga au geita au kahama au morogoro misitu hadi mjini, yaan vimiji nilivyotaja hivyo vyote havifikii bukoba hata nusu wee ndo unapayuka kusema eti kimji kimechoka nenda sasa hivi usisimuliwe tu ukadhan umejua anthropology ya bukoba nenda mpaka vijijini mfano katoma kiziba na vijiji na vikata vingine uone kama utakuta nyasi au wameezekea udongo kama dodoma, wee umetugusa pabaya, wataje wenye miji nawe usimame
 
MAMC

Senior Member
Jan 3, 2012
139
195
Ndo tatizo lingine la nshomile hakawii kutune external service service kushaua nakusahau kupeleka maendeleo na kusifia ,naishi Dar bwana wakati kimji cha bukoba kichovu huwezi amini ndipo nshomile wanatokea! Aaaaarg....... badillikeni!

Mkuru! we hujui? Watu wa Kagera ni wa mabingwa wa "rwango" wao kwa wao!
yani nimeanimi ubinafsi ni dhambi mbaya sana! Wakati wa wa uhuru mlikuwa mbele kwa kila kitu -elimu,Pesa,exposure,etc lakini kwa kupenda "urangila" - kujidai, na kutaka nyie mtu ndo mbaki juu (hasa miongoni mwa wahaya wenzenu) ndo imewafanya mrudi nyuma kwa sana! Mnabaguana sana Mara Waangaza,wanyambo,waganda Kyaka,waziba, wasubi,etc inakula kwenu mnapitwa hadi na Kigoma!

Hivi sasa wabunge wa Kagera ukitoa Mbassa ni "maiti" pale mjengoni! Kagera (200 kms from Kampala) inarudi nyuma kila kukicha - in all spheres, huku nyie mkibaki kujishow off Dar na ma vogue,hammer,etc
 
Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,401
1,500
Charles Mwijage Ingawa yuko kwenye chama cha magamba lkn katimiza ahadi nyingi pamoja na jitihada zake dhidi ya wahamiaji haramu toka Rwanda

We umelewa bhangi ka si rubisi. Mwijage aliingia kwa rushwa kwa kuchangiwa na watu walioko dar ka omba omba. Pia alipewa kibonde wa kupambana naye!! Na usisahau kumalizwa kwa mzee wetu Chritopher!!!! Kingine wabunge wote mbali na kuiba walibebwa na Prof. Ana Tibaijuka baada ya kuwa UN na kukosa mpinzani. La kukosa mpinzani lilikuwa kosa kubwa la kisiasa ambalo mkoa wa kagera unatakiwa kulijutia.

Sasa jimbo liko wazi nadhani ata ukipeleka jiwe pale ila atachukua Ansbert Ngurumo ndo chaguo la pale.
 
Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,401
1,500
ndg yangu yangu haya ndo moja ya mambo yanayowafanya watu wawadharau... wenzio tunajadili mambo ya msingi we unakuja na luga ambazo hazieleweki..tumia lugha ambayo watz wengi tutakuelewa.

Mkuu, huyu bishanga ni GAMBA lililokoma ambalo aliwezi ata kuvulika toka kwa joka zee bali kufa nalo. Mara zote ana aha na kulazimisha watu waende MMU ambapo anadhani watu watapotewa muda bila kujadili mambo ya kitaifa. Alafu ana vitisho.

Mimi ni mtu wa Muleba na nakiri kuwa kule majimbo yote ni kumsukuma mrevi! Kilichowabeba mbali na kuiba ni Prof. Ana alafu kampeni haikuwa na mashiko, kwakuwa tayari watu wanajua ni dhahiri CDM tuingie had mashinani maana magamba wamechukua majimbo na kufunga milango yetu kwenda mashinani
 
Paul Kijoka

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
1,401
1,500
Mkuru! we hujui? Watu wa Kagera ni wa mabingwa wa "rwango" wao kwa wao!
yani nimeanimi ubinafsi ni dhambi mbaya sana! Wakati wa wa uhuru mlikuwa mbele kwa kila kitu -elimu,Pesa,exposure,etc lakini kwa kupenda "urangila" - kujidai, na kutaka nyie mtu ndo mbaki juu (hasa miongoni mwa wahaya wenzenu) ndo imewafanya mrudi nyuma kwa sana! Mnabaguana sana Mara Waangaza,wanyambo,waganda Kyaka,waziba, wasubi,etc inakula kwenu mnapitwa hadi na Kigoma!

Hivi sasa wabunge wa Kagera ukitoa Mbassa ni "maiti" pale mjengoni! Kagera (200 kms from Kampala) inarudi nyuma kila kukicha - in all spheres, huku nyie mkibaki kujishow off Dar na ma vogue,hammer,etc

Nakuunga mkono, tatizo ni Ulkevi wa gongo na Lubisi. Na ndo sababu ya kumchagua Zimbiile kila mara huko Muleba sasa kusini na kaskazini.
 
mwabakuki

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
266
195
sioni kama nyote mnaochangia ili kama mna akili nzuri yaan taifa lipo kwenye misukosuko mingi mnaleta ukabila eti karne hii, acha hizo bwana, huyo naye sema bukoba imechoka kairinganisha na mkoa gani au wilaya gani? niambie bukoba maendeleo yaliyoko utayalinganisha na tarime, au mtwara au musoma, au kigoma ,au iringa, au babati au chalinze au songea au singida au taboraaa, au shinyanga au geita au kahama au morogoro misitu hadi mjini, yaan vimiji nilivyotaja hivyo vyote havifikii bukoba hata nusu wee ndo unapayuka kusema eti kimji kimechoka nenda sasa hivi usisimuliwe tu ukadhan umejua anthropology ya bukoba nenda mpaka vijijini mfano katoma kiziba na vijiji na vikata vingine uone kama utakuta nyasi au wameezekea udongo kama dodoma, wee umetugusa pabaya, wataje wenye miji nawe usimame

kaka hasira kiasi hiki haiwezi kukudaidia kujifunza. kujifunza ni pamoja na kukubali changamoto. kwa kiasi hiki cha hisira me nadhan jamvi hili si mahali pako. humu tunachambua, tunashauri, tunapeana changamoto, tunaambizana ukweli hata kama ni mchungu kiadi gani, tuna-compromise, na kufanya hivi tunajifunza zaidi; tunaboreka kiuwezo , kiuchambuzi, kimtuzamo, na hatimaye tunakuwa marafiki. wakati mwingine urafiki wetu unatokana na kutofatiana kwetu. tofauti hizi na uwezo wetu kukabiliana nazo ndo unatutofautisha wengine. kwa hiyo calm down. persevere tutavuka pamoja. lengo ni moja ni kuifanya Tanzania iwe bora zaidi. VIVA LA DEFFERENCE(na zidumu tofauti zetu) . ALUTA CONTINUA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom