Ni mazoezi gani yatanisaidia kujenga pumzi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mazoezi gani yatanisaidia kujenga pumzi?

Discussion in 'JF Doctor' started by mfukunyunzi, Mar 17, 2011.

 1. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba mnisaidie kujua aina tofauti tofauti za mazoezi yatakayoniwezesha kuwa na pumzi kwa maana nikifanya zoezi dogo tu naishiwa pumzi.

  Ndugu wanajamii naomba msaada wenu tafadhali.
   
 2. L

  Lepapalongo Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Anza zoezi la kukimbia umbali wa kati kama kuzunguka uwanda wa mpira huku ukiongeza round zake jinsi siku zinavyosonga uta gain speed ya kutosha.
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Jaribu zoezi la kuogelea, kwa kuwa umesema huwa unaishiwa pumzi mapema, basi mwanzoni ukiona ugumu huo usikate tamaa, endelea hivyo hivyo na baada ya muda mwili utazoea... Pia kama alivyo tanabaisha mdau hapo juu, Jogging nayo ni nzuri sana kwenye kujenga pumzi. Hivyo unaweza ukaanza na jogging na baada ya muda uka-join kuogelea..

  Angalizo.

  Mazoezi huwa yana ugumu wake hasa pale unapokuwa unaanza, usikate tamaa wala usikubali uvivu au maumivu yakakurudisha nyuma. Jitengee muda maalum kwa ajili ya kufanya mazoezi na usianze kwa kufanya mazoezi magumu bali anza na mepesi mepesi ili kuupa mwili nafasi ya ku-adopt mabadiliko.
   
 4. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu sema hapo kwenye kuogelea nitajaribu japo nipo mbali na vyanzo vya maji.
   
 5. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana kesho nitaanza
   
 6. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Fanya mazoezi ya kukimbia huku ukivuta pumzi ndani vuta mpaka mwisho kisha ibane muda mrefu kati ya sekunde 30 hadi 60. Kisha unaachia pumzi kwa nguvu,unavuta tena
   
 7. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ili nikushauri ningependa kujua yafuatayo.

  1. Una umri gani?
  2. Una uzito gani?
  3. Unafanya kazi gani?

  Basing on the answers for the above questions I would be in the better position of assisting you. Ila kwa haraka haraka unaweza kutembea umbali wa takriban kms5 kila siku, kuruka kamba kuanzia ishirini na kuendelea asubuhi na jioni, jogging. then from there you can go swimming, squash, tennese, badminton etc. Lakini pia punguza vyakula vya mafuta na wanga mwingi
   
 8. mfukunyunzi

  mfukunyunzi Senior Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umri miaka 27 kilo 65 na kazi mjasiliamali
   
 9. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Unavuta sigara? Ikiwa ndio, wacha. Na ikiwa ndio, ukifanya kwa dhati mazoezi uliyoelekezwa hapo juu Post 8 utawacha mwenyewe.
  Good Luck
   
 10. sumaibra

  sumaibra JF-Expert Member

  #10
  May 14, 2016
  Joined: Sep 1, 2013
  Messages: 212
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Ushaur:
  Nlianza mazoez ya jogging nna wiki ya tatu sasa...
  Mwanzo pumzi ilikua inasumbua ila sasa angalau ...
  Yakafata maumiv ya kiuno yanafanya nipunguze umbali ...
  Maumivu ya kiuno hayajaisha sasa yamekuja ya magoti...

  Wakuu ngependa kujua nakosea wapi
   
 11. kimbendengu

  kimbendengu JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2016
  Joined: Jun 7, 2013
  Messages: 2,146
  Likes Received: 1,071
  Trophy Points: 280
  wewe suma mazoezi ndiyo yalivyo vumilia usitumie dawa hiyo ni misuli inakaa sawa
   
 12. Nahonyo

  Nahonyo JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2016
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,120
  Trophy Points: 280
  Umepa ushauri sahihi kabisa, fanya mazoezi yote yanahohitaji kutumia punzi au kakata punzi, kuegelea ni zoezi linalohitaji punzi hasa na zuri Ila tahadhari anza na kina kidogo.
   
 13. LIKE Niku ADD

  LIKE Niku ADD JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2016
  Joined: Jul 21, 2014
  Messages: 3,472
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  fanya mazoezi ya kuogelea,zamia kwa dakika kadhaa kishaibuka.
   
 14. Don255

  Don255 JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2016
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 989
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Jaribu kufunga mdomo kipindi unakimbia(usikimbie mdomo wazi)hii itakusaidia kumentain pumzi

  Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
   
 15. sumaibra

  sumaibra JF-Expert Member

  #15
  May 16, 2016
  Joined: Sep 1, 2013
  Messages: 212
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Asante mkuu
  Najikongoja hvyo hvyo naamin yatapoa
   
 16. zegamba180

  zegamba180 JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2016
  Joined: Oct 8, 2014
  Messages: 748
  Likes Received: 386
  Trophy Points: 80
  Piga pushapu
   
 17. v

  vegas JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2016
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 986
  Likes Received: 405
  Trophy Points: 80
  Jogging, kuruka kamba, kuogelea, kuendesha baiskeli (cycling) ukisha kuwa na uwezo wa kufanya jogging umbali kiasi unaweza kuanza short sprints.. ( ni mazoezi yanayofanya moyo kuwa na uwezo wa kupump damu muda mrf- cardivascular capacity)
  Ukiweza kujenga huo uwezo mazoezi mengi utayamudu.
   
 18. merengo90

  merengo90 JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2016
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 6,465
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Hapa unampoteza .
  Pumzi usiachie kwa nguvu control it mdogo mdgo
   
 19. merengo90

  merengo90 JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2016
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 6,465
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Kosa lako ni kupunguza maumivu sometmz huwa ishara ya kuonyesha una exceed limit yako ya kawaida, hapo ulitakiwa uonge core excercise na miguu uongezee mazoez yake pia mbona utakuwa well.

  1463505114417.jpg
   
 20. merengo90

  merengo90 JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2016
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 6,465
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Kwanza tuanze na vyakula

  Epuka kula misos yenye pilpili, sigara, maji baridi.
  Chai tangawizi nzuri boy.

  Mazoezi fanya zoez lolote huku ukibana pumz usipumue then ikikata iachiwa taratibu.
  Kukimbia , kuruka kamba, kunyakua , push ups ni mazuri.
  Kuogelea ni zoez zuri coz viongo vyote vinahusika.

  Note . Ukiona unachoka hapo ndo komaa ongeza muda coz ndio unajaribu kuvuka kiwango cha kawida na kuji upgrade, otherwise utabaki hapo hapo.
   
Loading...