MJENGA
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 883
- 852
Wanajamvi kuna jambo linanitatiza sana wakati juu ambapo siasa zimeshika kasi kuelekea uchaguzi mkuu. Ni kwamba chama cha mapinduzi kimeweka wazi kuhusu kutoridhishwa na mwenendo Wa Lowassa Wa kuanza kampeni mapema tena kwa kutumia nguvu kubwa ya pesa. Mbaya zaidi amebadili modality kwa kuanza kuwajaza mahela wanaccm njaa na eti kurudi kwake kumshawishi agombee kwa kumchangia fedha ambazo wamezitoa kwake. Inashangaza sana, kwa ufuatiliaji nilioufanya, wanaoogoza kumpigia debe Lowassa mitandaoni ni wanachadema. Aidha vyombo vya habari vinavyompamba Lowassa ni ITV na gazeti la Tanzania daima. Ninajiuliza maswali na pia kuwaulizeni wadau, je, ni kweli Tanzania daima linalomilikiwa na Mbowe halijui uovu Wa Lowassa?. Je, Reginald Mengi, mmiliki Wa ITV hajui uovu Wa Lowassa?. Kuna ni nyuma ya pazia?.
Msaada Wa majibu wadau. Matusi kama baadhi yenu mnaona yanafaa, jitusi kwanza wewe kabla hujanitukana. Karibuni.
Msaada Wa majibu wadau. Matusi kama baadhi yenu mnaona yanafaa, jitusi kwanza wewe kabla hujanitukana. Karibuni.