Ni Maswali Gani Serikali Inapata Shida Kuyajibu kwenye Hoja za Tundu Lissu?

Binafsi nashangaa sana kwamba Dr Mollel hajaitwa kuisaidida polisi; atawasaidia hata kujua ulinzi pale area D uliondolewa kwa amri ya nani na CCTV cameras ziliondolewa kwa amri ya nani!
Wanamsubiri kwa hamu Mh.Lissu na Dereva wake kama vifaranga wa ndege wasubirivyo mama yao arudi wapate kurarua atakacholeta.
Sina uhakika kama watajishughulisha na walinzi au CCTV footage zilipo.Wanahamu na Mh.Lissu/Dereva wawararue ili wasemeni kina nani waliwashambulia?
Aibu!!!
 
Na kwa nini Serikali yetu ijibu hayo maswali kama Tu ndu Lisu ameshahitimisha kwamba Serikali yeti imempiga risasi? Sasa hayo majibu yatabadilisha nini?
Serikali inatakiwa ijibu hoja hizo si kwa ajili ya kumridhisha mlalamikaji bali kusema ukweli ili Watanzania waone ukweli ni upi na uogo ni upi kwenye eneo hilo.
 
Pale kanisani aliwafuata IGP na Director wa TISS na kuwaambia hao vijana wanaowatuma kwa nini wanasumbuka hivyo? Kama kuna tatizo wanashindwa nini kumwita na kuzungumza?
Alisema wale vijana amewajua na akawataka waachane na mpango huo.
Jambo alilieleza wazi na mamlaka hazikukanusha
..kuna vijana / gari ilikuwa ikimfuatilia akiwa Dar Es Salaam.

..TL alidai "aliwabana" vijana hao maeneo ya Saint Peters, na akadai kuwa ni vijana wa Usalama wa Taifa.

..Je, ni kweli vijana hao wanatokea usalama wa taifa? Walitumwa na nani?

Pascal Mayalla, Mag3

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo maana yake ni kwamba serikali haina namna ya kujinasua?
Look..... Upelelezi na au uchunguzi wa kina ukifanyika ukweli utajulikana.
Jambo la msingi ni serikali kutoa uthibitisho wa nani alihusika.
Kama watendaji wake iseme, kwani haina maana kwamba itakuwa imewatuma. Ukituhumiwa ukakaa kimya au kuja juu bila kufuata taratibu za kukunasua, tuhuma zitaonekana kweli.
Ijisafishe kwa nani kama Tu ndu Lisu anasema sacrosanct Raisi wetu kampiga risasi? Tena hahoji bali anathibitisha hivyo, sasa ulitaka Serikali inisafishe vipi kwenye hali kama hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jibu ambalo Serikali yetu itatoa liliridhishe maadui wa TZ yetu, unamjibu nini mtu anayekwenda foreign media kusema kwamba Raisi Magufuli amempiga risasi, sacrosanct ?

Hakuna jibu lolote litakalokubalika na haijalishi nani au uchunguzi gani umefanyika kama hautasema ,,Raisi Magufuli kampiga Tu ndu Lisu risasi “ sasa kuna haja gani kuwajibu watu ambao tayari wana jibu?

Kwa maoni yangu iko jinsi ilivyo na Tu ndu & Co. fanyeni mnavyotaka kufanya na kama mbwai na iwe mbwai.
Utter Rubbish.
 
Niliposikia Lissu kashambuliwa na kapona, one thing was clear, huyu jamaa atakuwa mwiba mkali kwa Serikali. Watu wasiojulikana waliamini asingepona, dead people don't talk. Sasa kapona, wanahaha kutafuta majibu ya maswali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maswali ni mepesi mno na yamejibika tayari.
Swali la 1 ni dhahania kwani hakuna mwenye uhakika kama kweli ulinzi uliondolewa. TL hili anachagiza tu maneno na kukuza jambo.

Swali la pili ni kwamba nchi yetu ni sovereign state ambayo kwasasa inajitoshereza kulinda raia wake kwahio hailazimiki kukodi vyombo vingine vya ulinzi na usalama kulinda raia wake au kuchunguza jinai. Landa vyombo vyenyewe kweli vishindwe na kukiri ila sio kushinikizwa na bado Jeshi la Polisi halijashindwa kuchunguza kubaini ni wakina nani waliohusika. Ni ukaidi tu wa TL na dereva wake kutotaka kuhojiwa kwa kupanga wao namna ya kuhojiwa yaani wanalipangia Jeshi la Polisi namna ya kichunguza tukio hilo....hii haiwezekani hata kidogo.

Swali la tatu. Tayari hizo nchi zilionesha upande katika kesi. Hata nchi ambazo TL na wapambe wenzake walitaka zifanye uchunguzi tyr kama nchi tulikuwa na ugomvi nazo katika kudhibiti rasirimali zetu, je wangekuja na mauchunguzi yao ya uongo kufarakanisha nchi? Serikali makini haiwezi kuruhusu upuuzi huo.
Mkuu nadhani hujaelewa swali la kwanza,swali ni je walinzi walikuwepo au hawakuwepo?kama walikuwepo wameshahojiwa na police kueleza what happened kwenye lindo lao na hatua walizovhukua,je hawakuwaona washambuliaji au kunakiti namba za gari walilotumia? Na kama hawakuwepo why hawakuwepo lindoni? Hicho ulichoandika hapo wewe kama si mwanaccm mwenziwe kukuelewa ni ngumu sana
 
Umenena ukweli. Halafu najiuliza hivi akimaliza kuzuru vyombo vya habari hapo Marekani ataenda wapi Aljazeera? Yani naona vyombo vya habari vimeisha kifuatacho ni kurudi wodini [/QUO ok kachukue malipo sasa
 
Rais ni amiri jeshi mkuu. Baada ya tukio alipaswa kuamuru vyombo vifanye kazi .
Kumbuka, the same week kuna mjeshi mstaafu alishambuliwa na kuporwa hela, wiki moja tu wahusika walipatikana.
Kwa Lisu tunaienda Mwaka wa pili. Hii ndiyo hoja kuu ya Lisu, kwamba kama anashindwa kuagiza vyombo kufanya kazi basi yeye ndiyo kahusika
Watu wengi wanashindwa kuelewa Logics/Mantiki, na Lisu ni mtaalamu wa logics.
Matumizi ya Maneno "Either", "Or", "And", " Nor" , " Neither" na " And/or" yanaleta kizungumkuti sana kama mtu hayajui
Tafuta interview ya hardtalk isitoshe amesema mara nyingi sana hata alipoita Waandishi wa habari alipotoka Nairobi hosp. alisema moja kwa moja bila ya kumumunya wala kusita kwa Raisi wetu alihusika na kupigwa kwake risasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishu ya Sovereignity haina mashiko. Nyerere amewahi kuomba msaada wa Kijeshi kutoka Kwa Mkoloni/Beberu Uingereza ili Serikali yake isipinduliwe mwaka 1964

Tumewahi kuomba wachunguzi wa nje kuchunguza mauaji ya Mapadri Zsnzibar

Kwa hiyo maadamu jeshi la polisi mpaka sasa limeshindwa kuchunguza tukio la shambulizi la Lissu na kwa kuwa Lissu anaituhumu element kuu ndani ya serikali kuhusika ni muhimu Wachunguzi wa nje wakaja kuchunguza ili ukweli ujulikane
Mbaya zaidi police wetu wamekiri kutokuwa na uwezo wa kuchunguza tukio hili bila kwanza kumhoji Lissu na dereva wake na hawana nauli wala uwezo wa kufika ubeligiji kuwa hoji,wakati wa kikwete kamati ya bunge ilipata nauli ya kwenda mpaka majiji ya washington na Richmond kuchunguza sakata la richmond,hii serikali misifa huku ikiwa fukara imeshindwa nauli ya askari wawili tu kwenda kumhoji Lissu hospital kama ni muhimu hiyo.Ningekuwa na uwezo ninaofikiriaga sometimes haki ya Mungu ningewachomoa mmoja baada ya mwingine
 
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
Vita ya Uchumi ni mbaya sana na ina madhara mapana sana kwa Taifa bila ya kuangalia Wewe ni Chadema au CCM.
Mabeberu wameguswa pabaya hapa nchini na "interest" zao zimetikisika. Kuna baadhi ya Dots ukiziunganisha kwa makini Kama una akili timamu unaweza kupata picha halisi ya mambo yanayoendelea.

U.S Gov kwa kupitia CIA wamekuwa VINARA katika kuchafua na kuharibu Amani Ulimwenguni pale Maslahi yao yanapotikiswa achilia mbali kuguswa. Mifano iko mingi sana.
Walimtengenezea zengwe Sadam Hussein na kutunga UONGO ya kwamba ana "Weapons of Mass Destruction"....WTF is Weapon of Mass Destruction !!!!????? Mpaka leo hii wameshindwa kueleza kwa undani na kutoa ushahidi wa hizo Silaha uko Iraq.

Sioni wala sitaona ajabu ikiwa hii Sinema ya Shambulizi la Mhaini Tundu ikiwa imeratibiwa, kutengenezwa na kuingizwa sokoni na VINARA wa kutengeneza machafuko na figisu Ulimwenguni kupitia kwa J. smith agent wao mkuu barani Afika. Muda utaongea.
Inachotakiwa mjue na kuelewa ya kwamba itakapotokea la kutokea hapa nchini, madhara hayo hayatachagua kama nyinyi ni Chamdema au CCM. Mtaonja joto la jua. Na mara nyingi watu wanaounga mkono serikali na serikali yenyewe pindi yanapoanza machafuko huanza kushughulika na nyinyi Vibaraka wa hao VINARA kwa kuwa mnajulikana na mnafahamika wapi mnapatikana.
Vibaraka ni watu hatari sana katika Taifa letu na bara zima la Afrika kwa ujumla.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Ibariki Afrika.

Tundu Lissu is just another greedy and unpatriotic Politician to sit on J-Smith lap - JamiiForums
 
Hakuna swali lisilojibika. Mtu akijibu "sijui" nalo ni jibu. Kuna maswali na hoja nyingi zimeibuliwa na Lissu kabla ya jaribio la kuuawa dhidi yake na muda wote wa matibabu hadi hivi sasa anapoendelea kutengemaa kiafya. Majibu mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa ama na vyombo vya dola au wanasiasa wa chama tawala au watendaji mbalimbali yanaonekana ama si ya kuridhisha au yasiyogusa moja kwa moja maswali na hoja za Lissu.

Kwa baadhi yetu tunaomuunga mkono Magufuli baadhi ya majibu haya yanaudhi na yanafanya watu wajiulize kama serikali haina watu wenye uwezo kweli wa kujibu hoja na maswali mbalimbali... hadi hivi sasa ni maswali au hoja gani za Lissu ambazo unaona hazijajibiwa vizuri, kwa usahihi, na hata weledi fulani... na zipi unaona zimejibiwa kisiasa zaidi...

Kumbuka hata jibu la "sijui" nalo ni jibu...

Nataka nione kama ningekuwa mimi katika Usemaji wa Serikali au mtu fulani ambaye anatakiwa kutoa majibu (Polisi, Bunge n.k) ningetoa majibu gani kama mazingira yote yangekuwa ni haya haya...
Kuna kitu kimoja watanzania hasa "mashabiki" wa serikali iliyoko madarakani wanashindwa kuelewa!

Si kila hoja inajibiwa kwa maneno matupu, hoja nyingine zinahitaji vielelezo thabiti

Nimeona watu wengi wanailalamikia serikali kwa kushindwa/kuacha kumjibu Lisu, hao wanaolalamika nadhani kuna kitu kimoja hawataki kukiwaza!

Hivi unadhani maswali kama:

1.Walinzi walipelekwa wapi siku hiyo!?

2.Hao walinzi waliokuwa zamu wameshahojiwa kumtaja aliyewapa amri ya kupumzika siku hiyo!? Kwanini hawajahojiwa!? Kati ya hao walinzi na dereva au Lisu mwenyewe nani shahidi muhimu!?

3. Unadhani kujibu swali kwanini CCTV camera ziliondolewa na hadi leo hazijasemewa chochote kama zilichukuliwa kwa uchunguzi au la ni kazi rahisi!? Huoni kama jibu la swali hili litazusha swali jingine, kwanini wamesubiri hadi Lisu alalamike kama walikuwa na nia njema ya kupeleleza kesi hii!?

4. Na unadhani Kangi Lugola kusema kesi imetelekezwa kisa Lisu na dereva hawapo nchini ili wahojiwe limeibua maswali mangapi!?

Nacho kiona mimi, ni vema tu waendelee kukaa kimya kama kweli hakuna uchunguzi uliofanyika! Kinachoweza kuzima malalamiko ya Lisu na wafuasi wake ni vyombo vya usalama tu kuja hadharani na kuulezea umma upelelezi umefikia hatua gani na status yake ikoje! Vinginevyo itakuwa ni kuendelea kuleta maswali yenye taswila isiyopendeza kwa jamii!

Hivi unadhani ni majibu gani yanaweza kutolewa hadharani kwa hoja za Lisu na serikali bila kutaja hatua ya upelelezi wa jaribio la mauaji yale na hayo majibu yakawa na mashiko!?

Mimi naamini waziri ni mtu mzito sana, tangu aseme kesi ya Lisu haipo maana dereva amefichwa asihojiwe sioni kama kuna mwingine atakuja atoe majibu zaidi ya hayo maana hata Balozi Masilingi alisisitiza hilo hilo, warudi nchini wahojiwe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
1. Kwani hao maadui wa tundu lissu hawawezi kuwapa fedha walinzi waondoke lindoni ikiwemo kuwatishia uhai wao iwapo watagoma..hayo ni ya kuhoji kweli kwa tanzania hii..? Hata jaji eliutha kapinga aliuawa nyumbani kwake wakati ana mlinzi.
2. Serikali ilishafanya uchunguzi..ilichokuwa inasubiri ni ushahidi wa dereva na sote tulisikia toka kwa mbowe kuwa dereva anapewa tiba ya saikolojia..huwezi kumruhusu kila mtu aingie chumbani kwako.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nadhani hujaelewa swali la kwanza,swali ni je walinzi walikuwepo au hawakuwepo?kama walikuwepo wameshahojiwa na police kueleza what happened kwenye lindo lao na hatua walizovhukua,je hawakuwaona washambuliaji au kunakiti namba za gari walilotumia? Na kama hawakuwepo why hawakuwepo lindoni? Hicho ulichoandika hapo wewe kama si mwanaccm mwenziwe kukuelewa ni ngumu sana
Mkuu toka lini Polisi wakawa kila hatua ya uchunguzi wao wanai-expose? Kwanini tunataka kuwa Polisi? Polisi wanasema TL aje na dereva wake wamhoji ili wakamilishe uchunguzi. TL anasema anaendelea na matibabu wakati huohuo anazurura Ulaya na Amerika kwanini asitumie muda huu kuja ili kusaidia uchunguzi maana anaonekana anazo taarifa nyingi.
 
Jamaa wa MATAGA mbona hawatupi taarifa za Bomberdiers, Dreamliner na Airbus...vipi zile safari za nje ya nchi zimeanza? Tukiwa wadogo niliwahi kusikia story za mtu mwny GUNDU. Eti chochote anachokifanya hakifanikiwi. Sijui Meko ana GUNDU?
Mkuu kwa ulivyosikia wewe safari za nje walisema zinaanza lini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu toka lini Polisi wakawa kila hatua ya uchunguzi wao wanai-expose? Kwanini tunataka kuwa Polisi? Polisi wanasema TL aje na dereva wake wamhoji ili wakamilishe uchunguzi. TL anasema anaendelea na matibabu wakati huohuo anazurura Ulaya na Amerika kwanini asitumie muda huu kuja ili kusaidia uchunguzi maana anaonekana anazo taarifa nyingi.
mkuu jalada la uchunguzi limeshafungwa unless useme wanataka kulifingua upya?ila for now nothing is going on.na hata wakati wanafunga hawakusema wamefikia wapi wala kipeleka mahakamani suspect
 
Back
Top Bottom