Ni Maswali Gani Serikali Inapata Shida Kuyajibu kwenye Hoja za Tundu Lissu?

Hakuna jibu ambalo Serikali yetu itatoa liliridhishe maadui wa TZ yetu, unamjibu nini mtu anayekwenda foreign media kusema kwamba Raisi Magufuli amempiga risasi, sacrosanct ?

Hakuna jibu lolote litakalokubalika na haijalishi nani au uchunguzi gani umefanyika kama hautasema ,,Raisi Magufuli kampiga Tu ndu Lisu risasi “ sasa kuna haja gani kuwajibu watu ambao tayari wana jibu?

Kwa maoni yangu iko jinsi ilivyo na Tu ndu & Co. fanyeni mnavyotaka kufanya na kama mbwai na iwe mbwai.
Hata hiyo comment yako ni MAJIBU, ila hayaridhishi!
 
Kujibiwa kwa usahihi maswali, au hoja zake zote, hilo halitawezekana. Hii ni siasa, na kama ni siasa, basi maswali mengine atajibiwa kisiasa tu, kama ambavyo yeye anavyotengeneza uongo mwingi kisiasa kujenga hoja zake.

Nafikiri yapo maswali mawili ambayo bado hayajajibiwa kwa usahihi na pengine yanayoleta utata mkubwa mpaka sasa, lakini papo hapo kwenye maswali hayo kuna maswali mengine juu ya maswali yanayotakiwa kujibiwa kwa usahihi.

Maswali yenye utata; walinzi wanaolinda eneo husika walikuwa wapi siku hiyo ya tukio? Na CCTV Camera ambazo zinadaiwa kuwepo eneo hilo nani kaziondoa?

Maswali juu ya maswali; huyu mtu pamoja na dereva wake naweza kumwita kichaa, ilikuwaje eneo linalolindwa na watu siku zote, siku hiyo wao ilikuwaje waingie kichwa kichwa kama wanaingia msalani? Je, CCTV Camera zinazodaiwa kuwepo, zilikuwa zimefungwa kutokea upande gani? Isiwe anapoishi huyu mtu hakuna kitu kama hicho, hivyo anategemea kupata msaada kutoka kwa jirani. Huo ni mtazamo wangu, twendeni taratibu tutafika tu!
Kirikuu ni KIRIKUU tu mpaka kichwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya maswali ni mepesi mno na yamejibika tayari.
Swali la 1 ni dhahania kwani hakuna mwenye uhakika kama kweli ulinzi uliondolewa. TL hili anachagiza tu maneno na kukuza jambo.

Swali la pili ni kwamba nchi yetu ni sovereign state ambayo kwasasa inajitoshereza kulinda raia wake kwahio hailazimiki kukodi vyombo vingine vya ulinzi na usalama kulinda raia wake au kuchunguza jinai. Landa vyombo vyenyewe kweli vishindwe na kukiri ila sio kushinikizwa na bado Jeshi la Polisi halijashindwa kuchunguza kubaini ni wakina nani waliohusika. Ni ukaidi tu wa TL na dereva wake kutotaka kuhojiwa kwa kupanga wao namna ya kuhojiwa yaani wanalipangia Jeshi la Polisi namna ya kichunguza tukio hilo....hii haiwezekani hata kidogo.

Swali la tatu. Tayari hizo nchi zilionesha upande katika kesi. Hata nchi ambazo TL na wapambe wenzake walitaka zifanye uchunguzi tyr kama nchi tulikuwa na ugomvi nazo katika kudhibiti rasirimali zetu, je wangekuja na mauchunguzi yao ya uongo kufarakanisha nchi? Serikali makini haiwezi kuruhusu upuuzi huo.
Wewe ndiyo hopeless kabisa.

Hivi Lisu na dereva wake, ni wakati gani walikataa kuhojiwa? Unakumbuka kuwa IGP mpaka alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa alikuwa ametuma wapelelezi kwenda kumhoji TL na dereva wake, kumbe ilikuwa ni uwongo?

Kama askari hawakuondolewa kwenye eneo la makazi ya viongozi alikoshambuliwa TL, hao si ndiyo wawe wa kwanza kuhojiwa maana watakuwa walishuhudia kila kitu, na ndio ambao ina maana waliwafungulia washambuliaji wakati wa kuingia na wakati wa kutoka.

Majibu yako ni afadhali ya Masilingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..1. Ni nani alitoa maelekezo ulinzi usiwepo area D siku aliyoshambuliwa TL?

2. kwanini serekali ilikataa ombi la familia ya TL kuwashirikisha WACHUNGUZI TOKA NJE ktk suala hili?

3.Kwanini serekali imegoma kutafuta msaada wa Polisi wa Kenya na Ubelgiji ili TL na dereva wake wachukuliwe maelezo?
Kwann viongozi wa chama na serikali hawajawahi kwenda kumuona alipokuwa hosp?
Kwann Magufuli alimkataza Ndugai kutoa fedha za matibabu kwa Lisu?
 
Wewe ndiyo hopeless kabisa.

Hivi Lisu na dereva wake, ni wakati gani walikataa kuhojiwa? Unakumbuka kuwa IGP mpaka alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuwa alikuwa ametuma wapelelezi kwenda kumhoji TL na dereva wake, kumbe ilikuwa ni uwongo?

Kama askari hawakuondolewa kwenye eneo la makazi ya viongozi alikoshambuliwa TL, hao si ndiyo wawe wa kwanza kuhojiwa maana watakuwa walishuhudia kila kitu, na ndio ambao ina maana waliwafungulia washambuliaji wakati wa kuingia na wakati wa kutoka.

Majibu yako ni afadhali ya Masilingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahio wewe unawapangia Polisi nini cha kuhoji na kutohoji? Na wahoji vipi? Hio sio kazi yako. Wenye kazi yao wanamtaka TL na dereva wake waje Bongoland wahojiwe....hivi umeishajiuliza kwanini TL hataki kuhojiwa akiwa hapa nyumbani? Wakati anazo nguvu za kuzurura huku na huko?

Pia suala la kuondolewa ulinzi ni suala la uchunguzi maana mimi na wewe tunasikia kwa TL ila siwezi kuwa na hakika kama huwa kuna ulinzi 24/7.
 
Mbona maswali yote yameshajibiwa? Lisu anamjua aliyemshambulia halafu anataka uchunguzi gani huru kushinda huo?

Bahati nzuri umepona hujafa kwenye tukio wewe umewaona waliokushambulia rejea sasa home kafungue kesi ya kushambuliwa kisha upeleke ushahidi mahakamani viachie vyombo Vya ulinzi vianze kufanya Kazi. Sasa wewe unakalia maneno tu yasiyona msaada wowote kwako ivi umesoma kweli ?

Tuhuma Kwa JPM unazotoa juu yake ni mwendelezo wa Kazi uliyokuwa unafanya kabla hata ya shambulio, hakuna siku JPM aliwahi kuwa mzuri kwako wewe cku Zote ulituaminisha ni adui yetu hasa pale ulisema,nakunukuu
Hajaijawahi kutokea tangu nchi yetu ipate Uhuru kuwa na rais wa ajabu kama huyu"" mwisho wa kunukuu.

Kwa hali hii roho yako , kinywa chako na vita yako itakwisha na kutulia pindi utawala wa JPM utakapo kwisha Kwa salama au Kwa kuangushwa Ndiyo itakuwa furaha yako Tundu Lisu

Hufanyi siasa bali ni chuki binafsi yawezekana una ka ugomvi binafsi na yeye maana wewe una hasira na mtu hadi basi hata hivi mshukuru Mungu Magu ana dini ningekuwa mm tungemaliza pori!

Nyie wapambe wa Lisu mshaulini mshikaji apunguze jazba hana faida na anachokifanya kwenye media zaidi ya kutaka tujue anauwezo gani wa kuchukia mwanaume hachukii hadi kuzionyesha hasira Kwa Adui Yake hadharani, huo ni utoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..unayoyasema ni kweli.

..lakini ni ukweli vilevile kwamba zipo kesi nyingi za mauaji au mashambulizi ambazo zimekuwa solved ndani ya muda mfupi, au muda unaoridhisha.

..katika uchunguzi wa jaribio dhidi ya TL sina uhakika kama Polisi wetu wameonyesha nia ya dhati ktk kuchunguza kwa haraka, na kutoa taarifa kwa wakati.

..kwa jicho la kawaida suala hili lilikuwa " cold case " too soon, bila Polisi wetu kuonyesha juhudi za kufuatilia.

..Wachunguzi wa kimataifa watatusaidia kuongeza credibility ya ripoti ya uchunguzi. Naamini tutafaidika kuliko kupoteza ikiwa watashirikishwa.
Mbona ya Dr Mvungi hatukuivalia njuga? Unajua iliishaje? Tatizo hatushughuliki na mzizi wa tatizo ndio maana sometimes wengine tunaona kuna usanii.

Yametokea mengi huko nyuma lakini Chadema hamkuwahi kuchukua hatua yoyote ingawa mlijitapa kuwa na kila ushahidi! Mbowe alisema anao ushahidi wote wa issue ya mabomu Arusha, ilifia wapi? Au kwavile walikufa na wengine kubaki vilema wananchi wa kawaida?

Issue ya Dr Ulimboka unajua ilikufa vipi? Mtafute Dr Ulimboka akupe kisa kizima na kwanini aliamua kukaa kimya na kutojihusisha na yeyote (sidhani kama anaweza hata kusimulia).

Mambo mengi yametokea na Chadema wamekuwa hawako aggressive enough kusimamia kujua kilichotokea na sheria imefata mkondo.

Issue Alphonce Mawazo si imeshakufa? Lakini baada ya hili la Lissu mnaitangazia dunia kuwa hili ndio tukio la kwanza la ajabu! Hivi wale vilema na waliopoteza wapendwa wao walioumizwa na bomu kule Arusha wanajisikiaje?

Mnalifanya tukio la Lissu kutaka nchi isimame lakini mnasahau wapo watu muhimu pia akiwemo Dr Mvungi vifo vyao tata vilipuuzwa na hakuna hata anayezungumzia sasa.

Hata hili la Lissu litapita maana dhambi ile ile itaendelea maana ina mizizi. Lissu kwa nature yake atapambana lakini itaisha kirahisi tu baada ya chorus kuchokwa na kama kawaida mtarukia tukio lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahio wewe unawapangia Polisi nini cha kuhoji na kutohoji? Na wahoji vipi? Hio sio kazi yako. Wenye kazi yao wanamtaka TL na dereva wake waje Bongoland wahojiwe....hivi umeishajiuliza kwanini TL hataki kuhojiwa akiwa hapa nyumbani? Wakati anazo nguvu za kuzurura huku na huko?

Pia suala la kuondolewa ulinzi ni suala la uchunguzi maana mimi na wewe tunasikia kwa TL ila siwezi kuwa na hakika kama huwa kuna ulinzi 24/7.
Hivi Polisi wewe unawaona ni miungu watu? Unajua kuwa polisi wapo kwaajili ya nani? Au wewe unadhani sisi ni watupu kabisa kwenye masuala ya usalama na ulinzi? Kwa taarifa yako mimi nina mafunzo katika masuala hayo, na nimeyapata toka kwa wataalam wa Jeshi la NATO. Na nina certificate.

Tuna uwezo, pengine kuwazidi hata hao unaofikiria kuwa hawastahili hata kuhojiwa au kutiliwa mashaka. Tunaheshimu tu mamlaka yao ya kikatiba lakini siyo lazima kuwa wabatuzidi ujuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ya Dr Mvungi hatukuivalia njuga? Unajua iliishaje? Tatizo hatushughuliki na mzizi wa tatizo ndio maana sometimes wengine tunaona kuna usanii.

Yametokea mengi huko nyuma lakini Chadema hamkuwahi kuchukua hatua yoyote ingawa mlijitapa kuwa na kila ushahidi! Mbowe alisema anao ushahidi wote wa issue ya mabomu Arusha, ilifia wapi? Au kwavile walikufa na wengine kubaki vilema wananchi wa kawaida?

Issue ya Dr Ulimboka unajua ilikufa vipi? Mtafute Dr Ulimboka akupe kisa kizima na kwanini aliamua kukaa kimya na kutojihusisha na yeyote (sidhani kama anaweza hata kusimulia).

Mambo mengi yametokea na Chadema wamekuwa hawako aggressive enough kusimamia kujua kilichotokea na sheria imefata mkondo.

Issue Alphonce Mawazo si imeshakufa? Lakini baada ya hili la Lissu mnaitangazia dunia kuwa hili ndio tukio la kwanza la ajabu! Hivi wale vilema na waliopoteza wapendwa wao walioumizwa na bomu kule Arusha wanajisikiaje?

Mnalifanya tukio la Lissu kutaka nchi isimame lakini mnasahau wapo watu muhimu pia akiwemo Dr Mvungi vifo vyao tata vilipuuzwa na hakuna hata anayezungumzia sasa.

Hata hili la Lissu litapita maana dhambi ile ile itaendelea maana ina mizizi. Lissu kwa nature yake atapambana lakini itaisha kirahisi tu baada ya chorus kuchokwa na kama kawaida mtarukia tukio lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unadhani kwa vile huko nyuma watu hawakuhoji na kuchukua hatua, ni sahihi haii hiyo iendelee hivyo hivyo?

Mimi nadhani ni busara kufurahia hatua aliyoichukua TL na wote wanaounga mkono ili matukio yale yote hovyo ya akina Mawazo, Mvungi, Ulimboka, Azory, Ben Saanane, Roma, Mo, n.k., yakome. Wewe unataka yaendelee kwa sababu tu yaliwahi kutokea na huko nyuma?

Double standards mkuu. Lazima tunywe ukweli wakati tukihangaika na hili la Lissu. Issue ya mabomu Arusha Chadema walisema hadharani wanao ushahidi wote na serikali wasipochukua hatua wataweka hadharani. Kwanini ilikufa kiaina?

Tusipojiuliza maswali kama haya hatutapona kama ambavyo hatukujiuliza kipindi viongozi wengine wanauawa na kuumizwa lakini sasa hivi tunasema bila aibu kuwa haya matukio ya mashambulizi katika awamu hii haijawahi kutokea utawala wowote!

Hatujifunzi, tunawekeza nguvu kwenye tukio la Lissu huku mengine yakitajwa kama matukio baada ya habari. Lissu yupo serious kuhangaika na JPM wakati anajua hata kama JPM akiondoka kesho bado CCM itatawala na wao Chadema hawawezi kushinda uchaguzi na hawajajiandaa kushika dola. Shortly hili tukio liko capitalised against JPM ambaye atakuwa JK wa kesho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona ya Dr Mvungi hatukuivalia njuga? Unajua iliishaje? Tatizo hatushughuliki na mzizi wa tatizo ndio maana sometimes wengine tunaona kuna usanii.

Yametokea mengi huko nyuma lakini Chadema hamkuwahi kuchukua hatua yoyote ingawa mlijitapa kuwa na kila ushahidi! Mbowe alisema anao ushahidi wote wa issue ya mabomu Arusha, ilifia wapi? Au kwavile walikufa na wengine kubaki vilema wananchi wa kawaida?

Issue ya Dr Ulimboka unajua ilikufa vipi? Mtafute Dr Ulimboka akupe kisa kizima na kwanini aliamua kukaa kimya na kutojihusisha na yeyote (sidhani kama anaweza hata kusimulia).

Mambo mengi yametokea na Chadema wamekuwa hawako aggressive enough kusimamia kujua kilichotokea na sheria imefata mkondo.

Issue Alphonce Mawazo si imeshakufa? Lakini baada ya hili la Lissu mnaitangazia dunia kuwa hili ndio tukio la kwanza la ajabu! Hivi wale vilema na waliopoteza wapendwa wao walioumizwa na bomu kule Arusha wanajisikiaje?

Mnalifanya tukio la Lissu kutaka nchi isimame lakini mnasahau wapo watu muhimu pia akiwemo Dr Mvungi vifo vyao tata vilipuuzwa na hakuna hata anayezungumzia sasa.

Hata hili la Lissu litapita maana dhambi ile ile itaendelea maana ina mizizi. Lissu kwa nature yake atapambana lakini itaisha kirahisi tu baada ya chorus kuchokwa na kama kawaida mtarukia tukio lingine.

Sent using Jamii Forums mobile app

..unachosema ni KWELI.

..kwamba kelele za CDM mara nyingi zimekuwa kama "KELELE ZA CHURA" na haziwatishi wenye mamlaka.

..Tujiulize sasa kama tunafaidika vipi kwa kuwa na watawala wenye uwezo wa kuziba masikio huku maovu yakizidi kujitokeza. Is it good for our future?

..Kwa mfano hili la TL nalo likipita, then what next? Kwa kuzingatia historia yetu kuna uwezekano wa kutokea jambo kubwa au baya zaidi.

..Ninachoogopa mimi ni kwamba tunaweza kufika mahali wananchi wakakosa imani na wakaamua na wao kujichukulia sheria mkononi.

..kuna clip moja nilimsikia IGP Sirro akilalamika vijana wa Mkiru kujiunga na itikadi za ajabu.

..kwa mtizamo wangu hayo ni matokeo ya vijana kukata tamaa kwamba political pressure haiwezi kuleta mabadiliko au kuhakikisha haki za watu zinapatikana.

..Rai yangu ni kwa WATAWALA. wanapaswa kuwa wasikivu.
 
Hii mada ilipaswa iungwe na zingine nyingi tu. Ila kwa kuwa mtoaji wa mada ni muasisi wa JF na shabiki kindakindaki wa "CCM ya Magu" basi itaachwa.

Ila kule FB ukimjibu hovyo Mwanakijiji tegemea kuminywa korodani na watu wa kitengo!

Account yake inalindwa na wale maafisa wasiojulikana. Uzuri watu wa kitengo tumesoma nao wametutonya tunajua na tumeepuka kule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata majibu ya uchunguzi ungetolewa na polisi bado yasingeridhisha isipokuwa tu wangeridhika kusikia magufuli ndiye aliyepiga zile risasi!
kabisa ,jiwe ndiyo aliyepanga mpango huu asilimia mia na kwenye kikao cha siri kilichohusisha watu wachache jinsi ya kummaliza tulishiriki!
 
Mzee mwenzangu tusichanganye Mambo. Wapo wengi tunamuunga mkono JPM humu lakini hatuungi mkono udhalimu aliofanyiwa TL.

Hili swala halihitaji siasa wala siyo rocket science. The government has been incredibly incompetent to give clean answers.

Mimi numsupport JPM. Lakini daima siungi mkono matendo ya kishenzi kama haya. Ni unwanted na unwarranted. Yanachafua taswira ya taifa letu without gaining anything.

Wengi humu supporters wake jiwe tunaumia... however tunaona aibu kukubali kwamba kilichofanyika ni ushenzi wa Karne ya 19. Hata kama ni mzazi. Akikosea mnaambiana ukweli. Tusihalalishe unyama wa namna hii kwa sababu yoyote. Lazima viongozi wetu wawe accountable.

Leo usipokemea ya TL tomorrow it could be You or Me. Muuaji Hana rafiki. Be warned!

Masanja!
Maana halisi ya Uzalendo kwa Taifa. Kongole Mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutamka kuwa hujawahi kupiga kura kuna mawili, pengine hujatimiza umri wa kupiga kura na hapa tunapoteza muda wetu kujibishana na katoto au hujapiga kwa sababu wewe ni MJINGA SANA hivyo hujui maana ya iupiga kura
Au hana akili timamu au kila uchaguzi ukifanyika anatumikia kifungo jela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yes amesema anahusika lakini hakusema kama ndiye alikuwa sniper. So swali ni alihusika kwenye kutoa tu ruhusa tu au hata kwenye mikakati na mipango ya zoezi zima?
Tafuta interview ya hardtalk isitoshe amesema mara nyingi sana hata alipoita Waandishi wa habari alipotoka Nairobi hosp. alisema moja kwa moja bila ya kumumunya wala kusita kwa Raisi wetu alihusika na kupigwa kwake risasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo unataka waache tu wasiulize, wasihoji na wala wasifuatilie ili kuepuka the double standards you're talking about?
Double standards mkuu. Lazima tunywe ukweli wakati tukihangaika na hili la Lissu. Issue ya mabomu Arusha Chadema walisema hadharani wanao ushahidi wote na serikali wasipochukua hatua wataweka hadharani. Kwanini ilikufa kiaina?

Tusipojiuliza maswali kama haya hatutapona kama ambavyo hatukujiuliza kipindi viongozi wengine wanauawa na kuumizwa lakini sasa hivi tunasema bila aibu kuwa haya matukio ya mashambulizi katika awamu hii haijawahi kutokea utawala wowote!

Hatujifunzi, tunawekeza nguvu kwenye tukio la Lissu huku mengine yakitajwa kama matukio baada ya habari. Lissu yupo serious kuhangaika na JPM wakati anajua hata kama JPM akiondoka kesho bado CCM itatawala na wao Chadema hawawezi kushinda uchaguzi na hawajajiandaa kushika dola. Shortly hili tukio liko capitalised against JPM ambaye atakuwa JK wa kesho tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasema wanamsubiri Lissu na dereva wake warudi wakatoe statement ndo uchunguzi uendelee wakati waliweza kumfuata Lissu Nairobi kumpa pole kwa kumtumia makamu wa rais na usalama wa taifa juu. Kwanini hawakuchua statement ya Lissu na dereva wake wakati huo? Halafu wanakua wakali wakihusishwa na tukio.
Wapelelezi wetu hawana tofauti na waganga wakienyeji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini baada ya dodoma serikali ilijitenga na tatizo la lissu?.
Kwa nini serkali kupitia spika ndugai walianza propanda juu ya ndege iliyo msafirisha lissu to nairobi,hadi pale yule mbunge wa pemba alipoingilia kati na kumuumbua spika.?kwa nini walitaka ionekane kua bunge/CCM NDO WALIO LIPIA GARAMA ZA NDEGE?.

kwanini hadi leo taarifa ya kitaalam kuhusu hata maganda ya lisasi haijatolewa?.

kwanini hadi leo hakuna yeyote yule aliyehojiwa juu ya kadhia ile,ila nguvu kubwa inaelekexwa kwa lissu na dereva wake?.hata walinzi wenyewe kwanini hawajahojiwa hadi leo?.

kwa nini imechuku zaidi ya mwaka kupita ndo baada ya lisu afya yake kutengemaa na kuanza kusema yeye mwenyewe ndo roho ziwatoke?.

kwanini police waliahirisha kwenda nairobi kumuhoji lissu na dereva waka kama walivyokua wameahidi?.

kwanini ndugai nae ameshindwa timiza ahadi yake ya kenda muona lissu aliyo itawa?.

kwanini wanalazimisha ionekane kua makamu wa rais na mzee mwinyi walienda nairobi kwa kwa magizo ya serikali?.

Kwanini yale yanayo itwa maagizo ya rais ya kufanyika haraka kwa uchunguzi wa tukio hilo hayajatekelezwa.japo yalikua kwa njia ya mtandao?.

kwanini nawe Mzee Mwanakijiji baada ya mwaka mzima ndo uone ipo haja ya majibu kutolewa,tena baada ya muhusika mwenyewe kuanza kuja huko uliko(KWA MABEBERU)kuchafua kama manavyodai,ndo ukoke mafichoni.

kwanini ile kauli ya wafukeze huko mbungeni wakija huku nje nita deal nao isihusishwe na tukio zima?.
 
Back
Top Bottom