Naona atleast tunasimama sehemu ambayo labda fikra zetu zikafikia muafaka, isipokuwa tu natofautiana na wewe unaposema kwamba vitu tunavyoongea huku "gizani" hatuwezi kuvisimamia kwenye jukwaa la hoja, hiyo sio kweli, hivi ni vitu ambavyo tunajadili mitaani kwetu, kwenye magazeti makini, kwenye midahalo mbalimbali ya wazi na kwa taarifa yako tu ni vitu hivi tu ambavyo vimekinyima ushindi chama "chako" huo wa kishindo wala sio eti hayo magamba mnayohangaika nayo sasa! Mi napendaga kusema kuwa hapa JF tunajadili TANZANIA MPYA (wengi wetu, sio wote).
Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Nakubaliana na mawazo yako kwa kuyaweka kwenye hoja kwamba tunahitaji mjadala kitaifa kufikia muafaka wa Tanzania tunayoitamani badala ya kushikana uchawi...... kama sijakosea!
Mi naweza kusema kuwa, kwa fikra zangu, labda nipate ushauri au muongozo toka kwa wataalamu wa siasa sioni wala sijui ni namna gani mnaweza kufikia mabadiliko na mapinduzi matakatifu ya namna ya kujitawala na kusimamia rasilimali zetu na ustawi wote (wengine wanasema hii kuanza upya), kwa amani kama mnaserikali inayotawala ni kama hii yetu. Rejea baadhi niliyoyaandika hapo juu, pia mifano mingi tu kudhibitisha kuwa tunaserikali ya watu wa namna ninayoisema.
Natambua kwenye historia na mpaka sasa kuna baadhi ya nchi ambapo sarekali ndio kiongozi mkuu wa harakati za kupigania mustakabali wa watu wake (hata hapa kwetu ilipata kuwepo wakati wa mwalimu tu) lakini sio serikali zetu(kwanzia Mwinyi,Mkapa na huyu wa saiv)
Sipingi wazo lako, ndio maana nkasema naomba mtu anielekeze falsafa hapo kama hilo wazo lako linatekelezeka katika mazingira ya sasa? Mi binafsi naona hiyo ni nadharia tu, unazungumzia kuwa watu wanalalamika tu na kuwa malalamiko hayana tija..... narudi palepale pa saa zile kuwa katika mfumo ambapo hamna mkondo uliorahisi na wazi wa raia wa kuwasilisha matakwa yao ya jinsi wanavyotamani mambo yaende katika maisha yao ya kilasiku, wakati wamezungukwa na kero tupu toka mtu anapoamka hadi anapolala, pia kwa namna hiyo siju unataka watu wa kawaida wafanyaje.... ikumbukwe kuwa kuna asasi kadhaa za kiraia lakini nazo malalamiko yao juu ya serikali hii kila mtu anayasikia (tunaweza kulijadili kivyake hili) Sasa katika hilo wakulaumiwa sio watu kama mzee mkapa akakurupuka eti "....mitanzania mivivu" Mungu akamuumbua kupitia kwa Rais wa Botswana, watanzania wanaijenga Botswana huku... Ndugu yangu serikali ya Mkapa ambayo wengi wanaisifia saivi wanaisifia ndio hiyohiyo ya bwana JK (chama ni kilekile)
Sawa sisis ni watu wa kulalamika tu, ila ndio serikali zetu zimetujenga hvyo kwa manufaa yao kwamba wakati sisi tutaendelea kuwa walalamishi tu wao waendelee na zoezi la kubadili utajiri wa nchi kuwa wakwao na familia zao,
Ndugu yangu, mataifa yanajengwa na yanajengwa na watu wake lakini chini ya usimamizi wa wenzao miongoni mwao, Marekani ya leo ni zao la ndoto ya zaidi ya miaka mia nyuma na Obama anzungumzia Marekani ya miaka zaidi ya mia baada yake.
Na zaidi sana lazima tukubali kuwa uharibifu huu unaoendelea kwenye taifa hili utakuwa na athari kubwa sana kwenye kizazi kijacho, katika namna ambapo hamna namna yoyote ya kitaifa kuandaa vijana wake kuwajengea moyo wa kizarendo na uwezo wa kiutendaji na utaalamu (fuatilia mfumo wetu wa elimu kwanzia toka chekechea hadi chuo kikuuu, tutalijadili mda mwingine) juu ya nchi yao, hapo ni lazima bomu litalipuka tu marabaada ya utawala wa sasa, kwamba ni kweli nchi itayumba tu sio wakichukua upinzani bali hata wakibaki hao CCM,
Nimalizie, samahani kama nitakuwa nimekuelewa vibaya ila sauti ya maandikio yako ni kama mtu unaeamini katika "CCM MPYA", sitaki kukuhukumu pia ila kuendelea kuamini katika ccm tu ni kizingiti kingine cha kifikra...... kuna mambo ni kama "classical" kwa ccm tusipoteze mda kuaminisha kwenye ccm mpya, au msipoteze mda kujenga ccm, hizo rasirimali ni za thamani sana kwa nchi hii, ni bora watu makini kama nyie muache uoga wa kichama..... mje mjenge upinzani imara kwa manufaa ya taifa hili kwa vizazi vijavyo japo maana kizazi hichi chetu najua hatutaiapata hiyo TANZANIA MPYA, sababu ccm ishavunja misingi yote.