Ni mapambano ya kulidhoofisha Taifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni mapambano ya kulidhoofisha Taifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Consigliere, Apr 20, 2011.

 1. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Japo ni vigumu lakini yatupasa tujifunze ustaarabu mpya, labda huo unaweza ukatusaidia.
  Kama CCM imejaribu kufanya jambo ambalo linalenga kuleta muafaka wa kijamii, kwa nini isipongeze kwa hatua hiyo? Kama tutaamua kujivalisha unafiki na kujitia upofu wa kutoona jambo ambalo lipo dhahiri sidhani kama tutafika kule ambak tumekuwekea matamanio ya siku moja kukufikia.

  Sidhani kama miongoni mwetu kuna mtu aliemsafi kwa kiwango kinachohitajika, na sielewi ni gauge ipi tunaitumia kupima na kuwapata watu wale tunaodhani kuwa ni wasafi.

  Kuna watu wamejichagulia tabia ya kupinga kila kitu kifanywacho na watu walio upande wasio utaka wao, hapo tutakuwa hatujifunzi kitu wala hatujiandaa na mafanikio ya baadae, ieleweke kuwa CCM peke yake bila ushirikiano toka kwa watu walio na itikadi ya vyama vingine haiwezi kuongoza nchi hii, vivyo kwa CDM, sasa sioni kwanini tusijenge ustaarabu katika kukosoana na kushauriana, badala yake tunajikita katika kudharirishana na kutiana maudhi, mbinu ambayo hutumika pale ambapo malengo ni kuangamizana na si kusaidiana na kurekebishana.

  Kuna njia ambazo ni za kisaokolijia zingeweza kutumika katika kurekebishana na hali na watu wangeelewana na maisha yangeendelea na maendeleo kupatikana, lakini kwa kuwa njia hizi za kisaikolojia ni tofauti na utashi wa kisiasa, acha na mimi niliongee katika mlolongo wa kisiasa.

  Tuache tabia ya kubuni na kuunga unga taarifa ambazo mwisho wake ni kuchafuana kusiko na tija, kama wote lengo letu ni kusimama kama taifa moja imara katika nyanja zote za kijamii, yatupasa tushirikiane, tuwe wazi kiutambuzi kuwa pamoja na kelele zote CDM pia wana nafasi kubwa ya kushindwa kutimiza au kuyafanyia kazi yale wanayoyaahidi kwa wananchi kama vile ambavyo CCM inavyoshindwa.

  Tuwe wakweli na kutambua mchango wa kila kundi katika kuijenga nchi yetu. Hakuna kundi la malaika miongoni mwetu, makundi yote yanaundwa na raia/binaadam dhaifu wenye mioyo na miili yenye asili na tabia za umimi, uchoyo, majivuno, tamaa, ubaguzzi,dharau,kukata tamaa, chuki,kuzaliwa, kuumwa kuishi na kufa.

  Kama kuna watu wa kundi au chama fulani kinaundwa na watu wasio na tabia nilizozitaja hapo juu na wajitokeze.
   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  utumbo tuuuu,unataka tuwasifie CCM kwa lipi,nani asiyejua kuwa JK alipita kila kona ya nchi hii na kuwanadi EL,RA, na AC??leo hi Kikwete huyu huyu anasema eti hao marafiki zake wa zamani ni mafisadi ,,heee??alikuwa wapi wakati wa uchaguzi na alipowanyanyua mikono na kusema ni wasafi alikuwa anamdanganya nani??

  KUWA WAZI KAMA NA WEWE UMEOLEWA KWA KIKWETE TUJUE SIO UNATULAZIMISHA KUSIFIA UTUMBO
   
 3. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Bora kupambana kupiga vita ufisadi, uchakachuaji wa CCM kwa Tanzania kuliko kusifia upuuzi na upotofu, uzandiki na ujambazi ili kuijenga Tanzania mpya na nzuri kwa vizazi vya baadae! UHUNI WA CCM WA UTAWALA WA HAUKUBALIKI! I WILL PERSONALLY FIGHT IT AT ANY COST!

  HIZI SI ZAMA ZA WOGA!
   
 4. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Hueleweki unapinga kitu gani, sijaagiza mtu asifie upande wowote hapo, in my articles I didnt deal with the means, but the methods jaribu kukua na kuacha akili zako wazi, usijizungushie ndani ya kuta za upofu na upumbavu, ingia katika ulimwengu wa uchanganuzi ili ujijengee uwezo wa kushauri, ukijikita katika kupinga kila kitu utaishia kuwa mlalamikaji mahiri of all the time.
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Hii dunia hatuhitaji watu walio wasafi mfano wa malaika na wala hatuwezi kuwapata,tunachokihitaji sisi ni wale watu wenye kujua nini maana ya usafi na wenye kuonekana wanapenda usafi...tofauti na hili ccm wanaonekana wachafu na wanapenda uchafu kana kwamba bila ufisadi uongozi ni impossible,sasa hilo sisi hatulikubali,we are going to eliminate all of them.
   
 6. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Mkuu elewa kuwa sifundishi kusifia wala kutukana, ninachokifanya ni tujiangalia na kujitambua sisi ni wakina nani na mahitaji yetu ni yapi, tukosoane sawa, tushambuliane sawa, lakini CCM si ya kulaumiwa katika ujumla wake, na wala hatukatai kuwa ndani ya CCM hakuna aina ya watu wanaotuhumiwa kwa kiwango hicho, wapo na wamechangia sana kudhoofisha hali ya nchi na kutuacha hapa tulipo.
  Ninachojaribu kuonyesha hapa ni kuwa munaposhambulia CCM ieleweke kuwa ndani ya chama hicho kuna kundi lingine ambalo nalo linapambana kama wafanyavyo wafanyavyo watu wa vyama vingine dhidi ya watu au kundi lile lile.
  Ndiyo maana nimesema matusi ya jumla ni kujenga ufa tu kitu ambacho hata baada ya vita kulishinda kundi kundi linalolalamikiwa hatutaweza kukaa pamoja na kuwajibika kwa maslahi ya taifa, kwasababu tayari tutakuwa tumejijengea picha kwamba kitendo mtu kuwemo ndani ya chama fulani ni tayari huyo ni mdhambi. Kila upande unahitaji changamoto ili kuwza kujijenga na kuwa imara.
  Hapo ndipo tunapofika mahali tujihoji je dhamira yetu ni ipi?
  CHADEMA ilijipanga vizuri sana, kwa kiwango ambacho kama ingeshinda uchaguzi wa mwaka jana ingepata ushirikiano mkubwa na wa hali ya juu kutoka kwa watu mashuhuri waliopo ndani ya CCM, hii inatokana na ukweli kuwa katika uchaguzi wa mwaka jana walikuwa na uungwana mkubwa kwa kuweza kuwatenganisha watu dhai na watuhumiwa waliomo ndani ya CCM na CCM yenyewe.
  Lakini sasa hivi inaonekana kuwajumuisha wote kuwa ni sehemu ya tatizo....hebu tufikiri kwa pamoja, nini kitarajiwe hapo mkuu?
   
 7. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wale wale waliokuwa Dodoma.

  kwanza: hatuwezi kuijenga nchi hii ikafika mahali tunapotaka ifike chini ya CCM.

  pili: njia pekee za kisaikolojia ni kupeleka lami kwa wananchi wa mashambani, umeme, maji safi. tuna raslimali za kutosha kufanya hivyo, lakini Tanzania chini ya CCM imegeuza rasilimali zetu kuwa mali binafsi ya viongozi wa serikali na hawajali.

  tatu: hakuna aliye msafi ndiyo, lakini CCM ni wachafu zaidi.

  nne: nani amekuambia kujivua gamba kwa ccm ni kwa manufaa ya jamii? nani? tutajie mmoja tu.
   
 8. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni kweli uyasemayo, pamoja na yote na hisia ulizoonyesha katika suala hili.... kuna vitu vya msingi nadhani bado chama tawala katika nchi yetu lazima kibebe lawama zote na majukumu ya kila kianachotokea katika matukio yanayotokea saiv hapa kwetu.

  Ni kweli chama hicho kimewahi kufanya mambo ya maana sana kwa nchi hii hiyo hamna anayeweza kukataa, lakini nao hawana sababu ya kusimanga watu na hilo sababu wao waliyafanya hayo mema kwakuwa lilikuwa jukumu lao la msingi, na wananchi hawalazimiki kushukuru kwa chochote kwani ni haki yao kutendewa mema na serikali yao.


  Unazungumzia kuwa tupongeze kwenye hatua waliyochukua juu ya ufisadi (kuvua gamba)... ndugu yangu hii itakuwa ni unafiki uliokithiri, sababu utakuwa hujamtendea haki mkulima na mfanyakazi wa kawaida eti ajitokeze kupongeza kujivua gamba kwa chama, ambapo zoezi lenyewe limehusisha kiini macho kwa wajumbe wa 3 tu (EL,RA & AC), nasema kiini macho sababu wajumbe hao bado ni wanachama hai tena bado wamo NEC, pia nasema itakuwa hujawatendea haki wakulima na wafanyakazi sababu tatizo lao wao sio mafisadi binafsi kama hayo magamba yanayodaiwa, tatizo kuu hapa ni mfumo wa ufisadi ambao upo toka serikali ya mtaa/kijiji hadi serikali kuu.

  Nakubali miongoni mwetu hamna mtu aliyekamilika japo wapo wenye uthubutu wa kuwanyooshea wenzao vidole bila wewe kuweza kuwanyooshea vidole, watu hao wapo... ila tusiende huko, bado nipo kwenye hili la mfumo wa kifisadi. Wazarendo kadhaa wakashauri japo turekebishe sheria ya TAKUKURU ili kuipa nguvu na meno zaidi (kuitoa kwenye ofisi ya rais) hamna aliyesikiliza, hata Dr Hosea analilalamikia suala hili (Wiki leaks alituja hilo)


  Sasa ndugu yangu kwa hili unataka mkulima na mfanyakazi apongeze nini hapo? Nini kimefanyika kwakweli??

  Unasema watu wamejichagulia kupinga kila kinachofanywa, sidhani kama watu wanapinga kila kinachofanywa ila watu tunapinga mengi yanayofanywa na kila jambo husika linalopingwa watu wanatoa hoja za kupinga na wanasuggest njia zenye maana zaidi na zenye manufaa ya wazi zaidi kwa watu wote lakini serikali hizi hazisikii la mtu awe mtaalamu au mwanaharakati.

  Rejea masuala ya umeme na tanesco yetu, kupanda kwa gharama za maisha (bei ya mafuta), hata la muswada wa marekebisho ya katiba (badala ya katiba mpya).... pia kubwa zaidi nakupa mfano mmoja wa namna tunavyotelekeza wataalamu wetu na vipaji vyao..... kwenye Gazeti la Raia Mwema la Aprl 6. ukurasa wa 12 kuna stori ya Dr Mselly Nzotta, mtanzania anayetamba uko Sweden kwenye masuala metallurgy ( teknolojia ya vyuma), kajaribu kuja hapa kuleta utaalamu hamna wa kumpokea, wakati chuma kule liganga tunampa mchina bila wataalamu
  wazawa wa kutosha, huo ni mfano mmoja tu kwenye eneo hilo moja.


  Ifike sehemu tuanze kuwa watu wa kufikiria makubwa kwa nchi yetu sababu nchi hii Mungu aliiumba ili liwe taifa kubwa sana ndio maana akaipa utajiri wote kuliko nchi zote duniani, kwa maana hiyo ni lazima tuache siasa nyepesi za kinafiki za kusifiana kijingajinga tu wakati tunapiga hatua moja mbele na kurudi kilomita nzima.

  Tukiringanisha potential za nchi kwa maana ya resource za kila namna na hapa tulipo baada ya miaka 50 ya uhuru, ukweli ni kwamba hamna kinacho fanyika na viserkali vyetu hivi vya watu wenye mawazo madogo wasioona mbali...!
   
 9. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Wewe umeshiba hautujui sisi wenye njaa kwa nini tunalalamika.
   
 10. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naona unatafuta Comfort zone Mkuu, hapa sio zenji kutaka muafaka baada ya kuona mambo yanaenda doro. CCM and its bureaucratic machinery will never bring the change we want in Tz. Na hatutaki Suluhu katika hili. Tumeshatafakari tafakuri zote, hadi unazohisi hatujatafakari. Hatutaki muafaka wala kisingizio chenu cha oooh mnahatarisha amani, oooh mnakua wachochezi. CCM ni nyoka mbaya sana, mnatuchekea majukwaani na kwenye hotuba huku mwatutafuna sisi na nchi yetu, wazi wazi na nyodo mnatuletea!

  Kwa nidhamu ya woga na ufisadi wenu mtachakachua hadi nguo zetu za ndani!

  WE WANT CCM OUT, (WABAYA NA WAZURI WAKE WAKIWEMO) CCM OUT CCM OUT CCM OUT CCM OUT!
   
 11. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Bado tuna tatizo katika uelewa, japo hoja zinazotolewa ni nzito na uzito wake unatokana na ukweli uliomo ndani ya hoja hizo.
  Lakini kitu ninachokiongea mimi hapa ni kifuatacho, tulikuwa na NCCR, waliokuwa NCCR waliongea waliyoyaongea wote tunaelewa kilichotokea. Tujiulize iko wapi NCCR ni nini kilitokea. Ninachokiongea hapa ni kwa ajili ya afya ya siasa zetu.

  Tunapojadili na kuchangia katika siasa ni vizuri tuongee katika hali ya kwamba wakati wowote tunaweza sisi tukapewa majukumu ndani ya vyama vyetu, je mara muda huo utakapofika tutaendelea kuongea mambo haya tunayoyaongea tukiwa ndani ya majina ya bandia? Hatuoni kuwa kwa kutumia muda mrefu kujiamini tukiwa gizani kunatuondolea fursa ya kujizoeza kuongea hadharani na hivyo kukomaza udhaifu wetu wa kutokuwa na ujasiri wa kuwakibili wale tunaodhani ni tatizo kwetu? Pia tunajiondoa binafsi katika nafasi ya kuwa viongozi itakapobidi hivyo kuishia kudhani kuwa kuna watu maalum wapo kwa ajili ya kutuongoza?

  Binafsi sijawahi kusita kuongea kile ninachokiamini, ninasikia faraja kama mtaniokosoa na kunihukumu kwa hoja na mtazamo wangu, na nipo tayari kubadilika kama nitathibitisha kuwa hoja yako ni sahihi. Ila jambo baya kuliko yote katika maisha yangu ni kuwa mtu mwenye kauli mbili katika maisha, yaani mchana niongee hivi na usiku niongee vingine, kwa kuzingatia hilo hapo ndiyo msingi wa hoja yangu unapotokea kuwa je kauli na matendo yetu yanaweza kuleta mchango wowote ili kupata mageuzi?

  Kuna mtu amesema hatuhitaji malaika wala watu wasafi kwa kiwango hicho bali wanaotambua kuwa kuna usafi katika maisha na watu na wanaotamani kuwa wasafi, hilo ni kweli kabisa, tatizo ni kuwa hoja nyingi zinazotolewa ni za mkato sana na zinazohitimisha kuwa kuwa anaehitajika ni mtu mwenye vigezo vya malaika.

  Tunahitaji viongozi wanaowajibika kwa wananchi, ambao watatutengenezea miundo mbinu itakayoharakisha maendeleo yetu na aina hiyo ya viongozi inapatikana na ndani ya jamii ya watanzania sisi ambao tumegawanyika katika misingi ya kiitikadi tofauti, je ni sahihi tofauti hizi za kiitikadi zitunyime fursa ya kutumia uwezo wa watanzania wengine waliopo katika vyama vingine.

  Ndani ya CCM kuna tupo tunaoshauri kuwa katiba ya chama ibadilishwe ili kuruhusu wapinzani kuingia katika baraza la mawaziri kwasababu kuna rasilimali watu ya nzuri sana kule, ndani ya CCM tupo wanachama ambao tunathamani mchango wa upinzani nchini na na wengine wanavipa msaada, tupo wengi ndani ya CCM ambao tunaamini kuwa maslahi ya chama si jambo la kupangiwa mkakati na kuingia gharama, bali ni suala la chama kuwajibika kwa wananchi kwa kadiri ilivyotarajiwa.

  Hapo ndipo ninapokuja kuhoji usahihi wa lawama za jumla, aina ya lawama ambazo kwa hakika hazitasaidia bali zitalizorotesha na kudumaza maendeleo ya taifa. Lawama na mashambulizi ambayo tuna ujasiri wa kuyafanya tukiwa gizani lakini hadharani hatupo tayari.

  Ndiyo maana nasema tusimame pamoja na tuongee kama taifa lugha itakayomfanya mtu kujitambua na tuungane pamoja kumpiga vita kwa namna yoyote ile mtu ambaye anahatarisha maslahi ya taifa na anayejaribu kufuja mali za nchi, na kudhani kuwa anstahili zaidi hayo kuliko wengine.

  Sijui kama kuna mwana-CCManayeweza akasimama hadharani na kuongelea uzuri wa CCM, pamoja na kuwa na mambo mazuri iliyoyafanya katika utawala wake, lakini haya mabaya yaliyofanywa ya kuweka kigingi katika guruduma na kukwamisha maendeleo ya taifa hakika yametuchafua wote ndani na nje kama wanachama na kama watanzania, watu hawa hatuna haja ya kuwaonea huruma wala kubembelezana nao.

  Lakini swali langu lina baki pale pale kuwa je lawama za jumla zina tija yoyote kwetu kama taifa??
  Pia muelewe kuwa kama mimi na ninyi hatutajiandaa na kuwa tayari kuwa viongozi kwa kuishi, kutenda na kuongea vile inavyompaswa kiongozi aliyepo madarakani basi tuelewe kuwa tunatengeneza kundi la walalamikaji daima dawamu.
   
 12. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #12
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Anzisha wimbo wa kusifu na kuabudu mi nitaitikia.
  Hata mimi nimechoka kuiisakama CCM ya watu.
  Maadamu imejivua gamba tuanzeni mapambio ya kuisifu.
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Naona Musembi unavuta shuka asubuhi. Huu ushauri kawape akina makamba kule Lushoto hapa jf tunajadili jinsi ya kuizika ccm maana ilishakufa
   
 14. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,071
  Likes Received: 7,554
  Trophy Points: 280
  Kati ya wote, wewe nadhani wewe ni kati ya wale wanaostahili unastahili heshima kwa namna ulivyokuwa muwazi, mtu akiwa muwazi kwa kiwango chako, ni rahisi sana kumuelewa, hicho ni moja ya vitu vinavyohitajika

  Big Up sana.
   
 15. Mwanahakij

  Mwanahakij Senior Member

  #15
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni muda wa kuwaambia chama cha magamba kuwa imetosha, hatudanganyiki tena! Tuwasifu kwa lipi, kwa sanaa ya kujivua magamba! ili tuwaamnini, kwanza watupatie list ya hao mafisadi wao, kama ubavu huo wanao, badala ya kupiga ngonjera! si hawa hawa walisema ccm hakuna mafisadi, sasa ndio wanajua mafisadi wapo?

  Isitoshe, hivi tuhuma za mauaji alizotoa dk Mwakyembe zimeishia wapi? na za Mengi kuhusu njama za kumbambikia mtoto wake madawa, hii sirikali ya ccm imechua hatua gani! ccm si ndio imeshika dola? tuwasifu kwa lipi? Waambie huu ni muda waa muafaka wa kujitoa moyo na sio magamba!
   
 16. F

  Falconer JF-Expert Member

  #16
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  CCM imeoza "to the core". Lipi tunategemea kutoka kwao wakati yote yaliotokea katika taifa hili la ubadhirifu wa mali ya umma hakuna hata mmoja aliyefikishwa mahakamani. Vipi tuwakubali viongozi wa CCM wakati wao hawawakubali wananchi wao wenyewe kama wana haki ya kidemokrasia katika taifa lao. Udikteta ndio ulioko CCM sisi hatuna haja nao. Wakati wao umekwisha. Kura zilizopita walishindwa kila jimbo lakini wameiba kura na ushahidi upo. Hii sio serikali halali kutawala tanzania. Hiki ni cha cha kuiangusha nchi na kurudisha nyuma ya maendeleo.
   
 17. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Huwezi ukakubali muafaka kwa namna yoyote ile kwa sababu hilo halitokuwa na maslahi kwako binafsi. Tunafahamu hata cabinet ya Chadema iliandaliwa hata kabla ya uchaguzi na kwa mfano nafasi yako unaijua.
  Ni kwa namna gani utaweza kutanguliza maslahi ya umma halafu ukabaki bila hata uDC kwa mfano.
  Nikukumbushe pia kuwa unaposema sisi/nchi yetu kumaanisha ujumla wa watanzania kaka you are wrong!! The majority said no for your party so next time you post jitahidi kukiwakilisha vizuri chama chako au mawazo yako kwa sababu hauwawakilishi watanzania...
   
 18. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Sina hakika na vigezo unavyotumia kupata scrape value, kwa maoni yangu ni vya kibinafsi sana, labda utajiri na madaraka.
  Kusema kila pesa inayopatikana inaishia kwenye mifuko ya mafisadi kunakutambulisha vizuri wewe ni nani na upo hapa kwa lengo gani, kwa sababu wizi upo lakini kuna barabara nyingi tu, madaraja yaani huduma za jamii japo siyo kwa kiwango ambacho tungependa. Sasa labda utuambie pengine ni wamarekani ndiyo wanatuletea mafanikio hayo kidogo au labda unatumia takwimu gani kupata hizo conclusions.
  Sisemi Chadema hawawezi lakini kama mtanzania naamini kuwa siyo lazima Chadema ishike dola ili nchi iendelee kama wadau wengi wanavyoonekana kuamini hapa...
   
 19. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu, siko hapa kujibishana mipasho, ingawa naona matapishi yangu yamekuchafua. HALAFU kumbe we ni CCM sasa nimejua, tena haujauvua GAMBA bado mwana MAGAMBA wewe, na akili yako ngumu kama gamba lako linalokufanya ujione kama mfalme kobe. Lililo la msingi kwetu tunalijua, Hizo HIV/AIDS,MARALIA,MAGONJWA MBALIMBALI,MAMBO YA KILIMO,UFUGAJI kafundishaneni nyie na nyumba ndogo zenu. Siasa za kihuni, kimabavu, kifisadi sasa mwisho. tutapambana na nyie, neno kwa neno, sera kwa sera, uhuni kwa uhuni, mtu kwa mtu. There was time to negotiate, talk, mediate sijui blah blah blah but sasa ni mwisho, no giving in.

  Wengi wenu kama si wote mnajiona kama mnamiliki nchi hivi, saa zote mnajipomasi pompasi, mkipita mmefura kwenye mashangingi ya Millioni 200 huku mama zetu mnawaletea ambulance za BAJAJ! Dumavu akili zenu zilizofinyuka sasa mwatoa fikra kwenye matumbo yenu, kwenu mwenye kitambi kikubwa ndo ana busara nyingi!

  Sasa muanze kujiandalia maisha nje ya serikali maana mtaabika wengi, ukianza na wewe kibarua cha mzee anaekuweka mjini kitakapoota nyasi!
  Chadema tutaiweka Tanzania Huru kwa Mara ya pili na ya kweli toka kwa mkoloni mnyonyaji, tapeli CCM!
   
 20. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Naona atleast tunasimama sehemu ambayo labda fikra zetu zikafikia muafaka, isipokuwa tu natofautiana na wewe unaposema kwamba vitu tunavyoongea huku "gizani" hatuwezi kuvisimamia kwenye jukwaa la hoja, hiyo sio kweli, hivi ni vitu ambavyo tunajadili mitaani kwetu, kwenye magazeti makini, kwenye midahalo mbalimbali ya wazi na kwa taarifa yako tu ni vitu hivi tu ambavyo vimekinyima ushindi chama "chako" huo wa kishindo wala sio eti hayo magamba mnayohangaika nayo sasa! Mi napendaga kusema kuwa hapa JF tunajadili TANZANIA MPYA (wengi wetu, sio wote).
  Niende moja kwa moja kwenye hoja yangu. Nakubaliana na mawazo yako kwa kuyaweka kwenye hoja kwamba tunahitaji mjadala kitaifa kufikia muafaka wa Tanzania tunayoitamani badala ya kushikana uchawi...... kama sijakosea!
  Mi naweza kusema kuwa, kwa fikra zangu, labda nipate ushauri au muongozo toka kwa wataalamu wa siasa sioni wala sijui ni namna gani mnaweza kufikia mabadiliko na mapinduzi matakatifu ya namna ya kujitawala na kusimamia rasilimali zetu na ustawi wote (wengine wanasema hii kuanza upya), kwa amani kama mnaserikali inayotawala ni kama hii yetu. Rejea baadhi niliyoyaandika hapo juu, pia mifano mingi tu kudhibitisha kuwa tunaserikali ya watu wa namna ninayoisema.
  Natambua kwenye historia na mpaka sasa kuna baadhi ya nchi ambapo sarekali ndio kiongozi mkuu wa harakati za kupigania mustakabali wa watu wake (hata hapa kwetu ilipata kuwepo wakati wa mwalimu tu) lakini sio serikali zetu(kwanzia Mwinyi,Mkapa na huyu wa saiv)
  Sipingi wazo lako, ndio maana nkasema naomba mtu anielekeze falsafa hapo kama hilo wazo lako linatekelezeka katika mazingira ya sasa? Mi binafsi naona hiyo ni nadharia tu, unazungumzia kuwa watu wanalalamika tu na kuwa malalamiko hayana tija..... narudi palepale pa saa zile kuwa katika mfumo ambapo hamna mkondo uliorahisi na wazi wa raia wa kuwasilisha matakwa yao ya jinsi wanavyotamani mambo yaende katika maisha yao ya kilasiku, wakati wamezungukwa na kero tupu toka mtu anapoamka hadi anapolala, pia kwa namna hiyo siju unataka watu wa kawaida wafanyaje.... ikumbukwe kuwa kuna asasi kadhaa za kiraia lakini nazo malalamiko yao juu ya serikali hii kila mtu anayasikia (tunaweza kulijadili kivyake hili) Sasa katika hilo wakulaumiwa sio watu kama mzee mkapa akakurupuka eti "....mitanzania mivivu" Mungu akamuumbua kupitia kwa Rais wa Botswana, watanzania wanaijenga Botswana huku... Ndugu yangu serikali ya Mkapa ambayo wengi wanaisifia saivi wanaisifia ndio hiyohiyo ya bwana JK (chama ni kilekile)
  Sawa sisis ni watu wa kulalamika tu, ila ndio serikali zetu zimetujenga hvyo kwa manufaa yao kwamba wakati sisi tutaendelea kuwa walalamishi tu wao waendelee na zoezi la kubadili utajiri wa nchi kuwa wakwao na familia zao,
  Ndugu yangu, mataifa yanajengwa na yanajengwa na watu wake lakini chini ya usimamizi wa wenzao miongoni mwao, Marekani ya leo ni zao la ndoto ya zaidi ya miaka mia nyuma na Obama anzungumzia Marekani ya miaka zaidi ya mia baada yake.
  Na zaidi sana lazima tukubali kuwa uharibifu huu unaoendelea kwenye taifa hili utakuwa na athari kubwa sana kwenye kizazi kijacho, katika namna ambapo hamna namna yoyote ya kitaifa kuandaa vijana wake kuwajengea moyo wa kizarendo na uwezo wa kiutendaji na utaalamu (fuatilia mfumo wetu wa elimu kwanzia toka chekechea hadi chuo kikuuu, tutalijadili mda mwingine) juu ya nchi yao, hapo ni lazima bomu litalipuka tu marabaada ya utawala wa sasa, kwamba ni kweli nchi itayumba tu sio wakichukua upinzani bali hata wakibaki hao CCM,
  Nimalizie, samahani kama nitakuwa nimekuelewa vibaya ila sauti ya maandikio yako ni kama mtu unaeamini katika "CCM MPYA", sitaki kukuhukumu pia ila kuendelea kuamini katika ccm tu ni kizingiti kingine cha kifikra...... kuna mambo ni kama "classical" kwa ccm tusipoteze mda kuaminisha kwenye ccm mpya, au msipoteze mda kujenga ccm, hizo rasirimali ni za thamani sana kwa nchi hii, ni bora watu makini kama nyie muache uoga wa kichama..... mje mjenge upinzani imara kwa manufaa ya taifa hili kwa vizazi vijavyo japo maana kizazi hichi chetu najua hatutaiapata hiyo TANZANIA MPYA, sababu ccm ishavunja misingi yote.
   
Loading...