Ni makosa kuandika ''TUNAUZA MKAA'' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni makosa kuandika ''TUNAUZA MKAA''

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Gang Chomba, Dec 16, 2011.

 1. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  sehemu mbali mbali hapa Tanzania nimekuta
  tangazo ''TUNAUZA MKAA''.

  Unapoandika unauza MKAA inamaana unauza kipande kimoja.
  Ila neno fasaha linalotakiwa kutumika hapo ni ''TUNAUZA MAKAA''.

  Ukiwa mmoja unaitwa MKAA.
  Na yakiwa mengi yanaitwa MAKAA.

  Na ndio maana huwezi kukuta neno MKAA WA MAWE huku yakiwa mengi. bali utakuta neno MAKAA YA MAWE.

  So ukikuta mahali pameandikwa hivyo basi mtafute
  muhusika kisha mnase vibao. Akikupeleka polisi nitafute kisha watajuwa kama kuna wanasheria wa kuzaliwa na wanasheria wa kusomea...
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa sheria gani hasa inayokuruhusu kupiga vibao watu wanaokosea maandishi ya maneno ya kiswahili?
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo basi itakuwa namna hii au sio....!?

  Mkaa = Makaa (Mikaa?)
  Jiwe = Mawe

  Makaa ya mawe (Wingi)
  Mkaa wa jiwe (Jiwe la mkaa? Mkaa wa mawe?)

  Hapa ni confused dot com
   
 4. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Aiseee yaani wewe ndio umenivuruga kabisa, hata kile nilichokuwa nataka kuchangia kimetoweka! khaa..
   
 5. Jayfour

  Jayfour Senior Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wala usichanganyikiwe na haya maneno mawili ambayo ni tofauti.
  Mkaa = (charcoal) aina ya nishati inayotokana na miti au mimea uliyoungua nusu kwa kukoseshwa oxygen ya kutosha.
  Makaa = (coal) ni aina ya nishati inayotokana na miamba ya mawe.

  Mkaa -> unakata miti
  Makaa ->unachimba ardhini kwenye miamba ya mawe na hivyo kupata jina "MAKAA YA MAWE"

  Makaa si wingi wa neno mkaa, hizi ni bidhaa mbili zenye asili tofauti ingawa zote ni nishati.

  Hatuwezi kusema eti wingi wa petroli ni dizeli.
   
 6. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  oh hii imekaa vizuri. kwa hiyo wingi wa Mkaa ni Mikaa si ndio.. Thank you very much.
   
 7. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahsante sana.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mayasa, umewasoma wataalamu vema hapo juu? Hakuna mikaa, ni mkaa tu na makaa
   
 9. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Huo ndo uanasheria wa kuzaliwa...
   
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Usiwe na wasi wasi, lengo ni kuonyesha kwa vitendo kuwa anachotaka kueleza sicho.

  Mkuu, naelewa sana kuwa hizo ni bidhaa mbili tofaiti ila zenye kufanana kimatumizi, ila mleta mada ndio kajichanganya kidogo... Na atambue kuwa kuna vitu ambavyo havina wingi wala umoja.
   
 11. M

  Maamuma JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 856
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu iliyotolewa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Dar es Salaam, imeandikwa hivi:
  "Mkaa pia makaa nm vipande vya miti vilivyochomwa moto na kuzimwa kabla ya kuwa majivu."

  Kwa maana hiyo, maneno yote mawili (mkaa na makaa) ni sahihi. Wingi wa mkaa ni ama mkaa au makaa. Yote yanakubalika.
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tofautisha kati ya mkaa utokanao na miti na mkaa wa mawe. Mkaa wa miti umoja na wingi unabaki "mkaa". Mkaa utokanao na mawe, wingi na umoja wake ni "makaa ya mawe".
   
 13. Mayasa

  Mayasa JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 587
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ehh kumbe nilitaka kujipotosha.. asante kwa kunielewesha
   
 14. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  nina hakika mtoa mada ameishi kenya ama anaangalia sana tv za huko.
  Wakenya hawauzi mkaa, bali wanauza makaa.
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  wapendwa,

  vyote "mkaa" na "makaa" ni sahihi kutumika na ni maneno yasiyokuwa na wingi wala umnoja, yaani kiwe kipande kimoja ama vipande kadhaa, huitwa mkaa/makaa. ni sawa na neno "maji", huwezi kusema umoja wa maji ni "mji" au "uji" na wingi wake ndio eti; "maji"! "mji" na "uji" ni maneno tofauti kabisa na yana maana tofauti sana na hayana uhusiano na "maji"

  hivyo basi, yeye asemaye mkaa yuko sahihi na yule asemaye makaa pia yuko sahihi, iwe ni mkaa wa mawe ama makaa ya mawe, kauli zote ni sahihi

  @ X-Paster, kifungu nomino "makaa ya mawe" ni jina moja la bidhgaa inayoitwa "coal" kwa kiingereza, huwezi kusema kuwa kipande kimoja ni mkaa/makaa ya jiwe na vikiwa vipande kadhaa ndio makaa ya mawe kiwe kipande kimoja au tani kadhaa za bidhaa hiyo, huitwa makaa ya mawe!

  wakati mwingine huweza kutumika kifungu maneno "kaa la mawe" kumaanisha kipande kikubwa kuliko ukubwa wa kawaida wa mkaa/makaa ya mawe! halikadfhalika, siyo sahihi vilevile kusema "kaa la jiwe" ukimaanisha pande kubwa la mkaa/makaa ya mawe

  mbarikiwe sana

  Glory to God!
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Miss Judith,habari za siku!!
  Recently ninekuwa nikijiuliza huyu mpendwa yu wapi tena! Natumaini umekua vyema, na unazidi kubarikiwa.
  Nilikukosa sana, ukutane na muujiza wako jumapili ya leo na zaidi Mungu akutane na haja ya moyo wako
   
 17. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mpendwa King'asti,

  mimi sijambo sana na nimekuwa nikizifurahia baraka za Mungu kila siku. nimekuwa na kazi nyingi sana siku za karibuni na pia nililazimika kusafiri kwa dharura majuma kadhaa yaliyopita, lakini Mungu ni mwema na kila kitu kwa sasa kinakwenda vizuri.

  asante sana kwa kunim miss mpendwa na kwa dua. Mungu wetu wa rehema na neema asikuache siku hii njema ya leo na akifanye kila kiujazacho moyo wako kuwa kweli, amen.

  he, tusijekuwa tunachakachua thread ya watu,

  ubarikiwe sana mpendwa

  Glory to God!
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  aisee kumbe hakuna mkaa wa mawe wala makaa ya mti...!!
   
 19. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #19
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Ngoja tuanze kufafanua vizur haya maneno.
  Neno KAZI.
  Likitumika kwa mtu itakua MKAZI.
  Neno KAA hivyo mtu ataitwa MKAA.

  neno TU ikiwa ni mtu ataitwa MTU.

  Kwa kua kiwakilishi cha M huhusika kwa mtu.
  Hata wewe chunguza utafaham tu!.
   
Loading...