ni makosa kuandika ''TUNAUZA MAFUTA YA TAA''...

Enzi zetu Ilikuwa tunatamka Mafuta Taa kama neno moja. Ila ukilisikilza hilo neno toka kwa mtu mwingine utasikia akitamka MAFUTA YA TAA. Nahisi ndio chanzo cha hiyo YA.

Hichi kizazi cha ''hakuna majotroo'' ndio kinatuharibia Lugha
 
Hayo mnaita makosa yaliyozoeleka...poleni
Sijayaita makosa na kwa hakika sio makosa isipokuwa wewe ndiye unayetaka tuamini kuwa ni makosa. Makosa kwa nani ikiwa wenye lugha ndivyo wanavyokubaliana na kuelewana? Halafu neno au maneno yanaweza kuwa na maana zaidi ya moja. Kwa hiyo neno (kiunganishi) "ya" linaweza kuwa na maana "kwa ajili ya..." au "yaliyotokana na..." nk.

Labda nikupe pole wewe unayetaka mzungumzaji wa kiswahili wa leo aseme "mafuta kupikia" badala ya "mafuta ya kupikia"! Vipi kuhusu 'taa ya mafuta' au 'taa ya umeme"...nayo ni makosa?

Labda kingine unachotakiwa kujua ni kuwa lugha inakua/inabadilika kwa kadri jamii inavyobadilika.
 
huko kukua kwako kwa kiswahili ndio mnaondoa maantiki na kuruhusu makosa yazoeleke.
Kweli uongo ukijirudiarudia huwa ukweli
 
huko kukua kwako kwa kiswahili ndio mnaondoa maantiki na kuruhusu makosa yazoeleke.
Kweli uongo ukijirudiarudia huwa ukweli
Mbona unakwepa kujibu maswali?

Ukitaka mantiki katika lugha unaweza kujikuta unalazimika kubadilisha maneno mengi kweli na kuishia kuwa kituko tu. Angalia majina ya kiswahili ya siku za wiki...'siku ya tano' tunaiita Jumatano na 'siku ya sita' tunaiita Alhamisi.....lakini neno 'alhamisi' tumeliohoa/tumelikopa kutoka kwenye kiarabu na hasa lilkiwa na maana ya "siku ya tano"....sasa kwa mantiki yako haya ni makosa na hiyo tunahitaji kuyasahihisha, au siyo?

Gang Chomba, labda ukubali tu katika hili la 'mafuta taa' huna hoja inayoweza kusimama yenyewe!
 
Haya ni makosa yaliyozoeleka kwa mfano wa2 wengi husema nimemkuta hayupo kama alikuwa anamtafuta m2 so imezoeleka hivyo na anaeleweka.
 
kiswahili kigumu kaka. Unatofautishaje 'mba' na 'mba'? Mboma tunasoma 'mbwa' badala ya 'm-bwa'? Neno 'ya' linatumika kwa namna nyingi. Inategemea na mazingira kama hayo hapo juu. Tukisema 'timu ya Yanga' unawaza nini? Yanga ni nini? Hata hiyo mafuta taa ni kosa pia. Kwani yanatumika kwenye taa tu?
 
yaani kama hivi:

Mafuta ya taa [mafuta taa?]
mafuta ya kupikia [mafuta kupikia?]
mafuta ya kula [mafuta kula?]
mafuta ya kujipaka [mafuta kujipaka?]
mafuta ya ndege [mafuta ndege?]

bado sijashawishika!. Lugha, hasa majina, sio lazima iwe na mantiki! Lugha ni mazoea (ya muda mrefu?) tu baina ya wanajamii katika kuwasiliana.

Hata jina la mafuta ambayo tumezoea kwa kiingereza kuyaita 'diesel' (dizeli kwa kiswahili), kimsingi linatoka na matumizi kama ilivyo 'mafuta ya taa'. Kilichoanza ni diesel engine (diesel likiwa jina la mvumbuzi wa aina hiyo ya injini ya gari)....hivyo mafuta ambayo yanatumika kwenye aina ya injini ya gari iliyovumbuliwa na diesel, wakaanza kuyaita diesel! ('dizeli' ukipenda 'mafuta ya dizeli'). Hata hivyo aina zote hizo za mafuta bado zina majina yake ya kitaalamu.

samaki wa kupaka-samaki paka
 
The matter is to understand what does it mean and not other wise
 
TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi mtoa mada alifail shule...

hapo kiunganishi ni ya Sasa yeye haweki kiunganishi hata mtoto mdogo ukiwa unamfundisha lugha hatokuelewa.

Mkuu nadhani ndio umeamka haya mambo yalishapitiwa zamani hizi yakajadiliwa hadi yakawekwa sawa mwishowe ikaonekana kuandika TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi..

hapo ulipolalia wenzio waliamkia.
Wacha kupotosha Lugha kama huelewi omba msaada ueleweshwe.
 
Haya ni makosa yaliyozoeleka kwa mfano wa2 wengi husema nimemkuta hayupo kama alikuwa anamtafuta m2 so imezoeleka hivyo na anaeleweka.
Unaweza sema Nimekuta hayupo..

Waingeleza Husema I Found Nothing....
 
TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi mtoa mada alifail shule...

hapo kiunganishi ni ya Sasa yeye haweki kiunganishi hata mtoto mdogo ukiwa unamfundisha lugha hatokuelewa.

Mkuu nadhani ndio umeamka haya mambo yalishapitiwa zamani hizi yakajadiliwa hadi yakawekwa sawa mwishowe ikaonekana kuandika TUNAUZA MAFUTA YA TAA ndio ipo sahihi..

hapo ulipolalia wenzio waliamkia.
Wacha kupotosha Lugha kama huelewi omba msaada ueleweshwe.

Huna unalojuwa, sanasana naona unakurupuka tu kama Hiza Tambwe.
Nenda kaulize kwenye Baraza la Kiswahili kisha watakupa jibu sahihi.

Sio unakaa na kuleta porojo zako hapa eti mlishajadili na kupata jibu kuwa ni MAFUTA YA TAA.

Toa uongo wako hapa
 
Mi nakumbuka wakati tuko wadogo tukitumwa na bi mkubwa dukani tunatamka ''MAFTATAA" maybe kama kuna innovation iliofanyika apo katikati ila so far nakubaliana kabisa na wanaosema mafuta taa.......
 
Mi nakumbuka wakati tuko wadogo tukitumwa na bi mkubwa dukani tunatamka ''MAFTATAA" maybe kama kuna innovation iliofanyika apo katikati ila so far nakubaliana kabisa na wanaosema mafuta taa.......

Una akili nyingi sana.
Wewe ni great thinker wa ukweli kabisa.
 
Kichefu chefu. Msitafsiri kiingereza directy kuwa kiswahili kama Wakenya walivyo tuchakachua! 'Nyama choma' akimaanisha nyama ya kuchoma. Etc.
 
unauza Kerosini (kerosene), kama vile tunauza petroli (petrol), dizeli (diesel), gesi (gas).

Au tunauza mazuti "mu taa" (kongo, rwanda, burundi).
 
Mi nakumbuka wakati tuko wadogo tukitumwa na bi mkubwa dukani tunatamka ''MAFTATAA" maybe kama kuna innovation iliofanyika apo katikati ila so far nakubaliana kabisa na wanaosema mafuta taa.......
Haswaa ndivyo ilivyokuwa......Tatizo vijana wa .com wamelinyambulisha siku hizi. Na kwa vile hawakuwepo enzi hizo sidhani kama hapa wanaweza kutuelewa!
 
Unaweza sema Nimekuta hayupo..

Waingeleza Husema I Found Nothing
....

Mkuu rejea vizuri tafsiri yako Nimekuta hayupo si sawa na I found Nothing! kwa uelewa wangu I found Nothing ina maana " Sikukuta Kitu"
 
By, INSTITUTE OF KISWAHILI RESEARCH, UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM,
kerosene n kerosini, mafuta ya taa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom