Ni maandamano au ni mapinduzi?

Kwani Yale Ya TAHRIR SQUARE Yaliyomtoa MUBARAK wa MISRI Yalikuwa Yanaitwaje? Ukipata Jibu Hapo Fanya Kubold Na Kisha Pigia Mstari
 
Sina hofu yoyote. Ila nawatahadhalisha maana wengine watakaoingia barabarani ni michepuko yetu. tusije kuwapoteza mapema
Mbona wanaokatwa mapanga hujawahi kuwatahadhirisha?Huu upendo kwa watanzania leo umeutoa wapi?
 
Sijamtisha mtu bali nimeeleza uhalisia. Fanyeni hayo mapinduzi dhen muone cha mtema kuni
Mbona Unawashwa washwa? tulieni niko huku natiki kalenda tu halafu nakukumbusha tu kuna wale vijana waliopita Kwa mujibu wako mtaani wa kutosha
 
Kwani Yale Ya TAHRIR SQUARE Yaliyomtoa MUBARAK wa MISRI Yalikuwa Yanaitwaje? Ukipata Jibu Hapo Fanya Kubold Na Kisha Pigia Mstari
Kumbe ndo hivyo! Basi subirini cha Mtema kuni.
 
Mbona Unawashwa washwa? tulieni niko huku natiki kalenda tu halafu nakukumbusha tu kuna wale vijana waliopita Kwa mujibu wako mtaani wa kutosha
Hahahahahahahahaaaaaa. Na sisi tunatest mizinga yetu
 

kwani umeambiwa lengo kuu la maandamano ni kumtoa JPM madarakani,akili yako haina akili,tunahitaji apate ujumbe kuwa watz tumechoka kuuliwa kama kuku,kuongozwa kama bata au nguruwe,tunahitaji asikilize ushauri wa watu,asiwe ye ndio alpha na omega,ajue kwamba mataifa ya nje yanamuangalia vibaya, ajue kuwa anatukosanisha na majirani pia mataifa ya nje,ajue kuwa demokrasia inatakiwa ihubiriwe na sio udikteta, ajue kuwa hali za maisha yetu ni ngumu na tunaishi kwa hofu,ajue kuwa uongozi ni bora kuliko utawala,ajue kuwa wapnzani nao ni watu ktk nchi yao,ajue kuwa kauli zake ni mmbaya na watu wanazihifadhi vibaya ktkt mioyo yao,ajue kuwa nchi hii si ya ccm peke yake,ajue kuwa hata kabla yake kulikuwa na maraisi na pia baada yake watakuwepo wengine,ajue kuwa asitaje bure jina la bwana MUNGU wakati anamfanyia dhihaka na unafiki,

MUNGU HADHIHAKIWI.AJUE KUWA WATZ WANALIA NA KILIO CHAO HATA SIKU MOJA HAKITAENDA BURE,TUNATAKA AJUE HVY,MAANA KATUZIBA MIDOMO AKASAHAU KUWA KUNA WATZ WANAISHI NJE KASAHAU KUWA KUNA MEDIA ZA KUFIKISHA UJUMBE, KASAHAU KUWA TZ ni mji mkubwa sana tofauti na Rwanda hvy huwezi kuongoza nchi km hii utadhan unaongoza chato au misungwi,kila kitu kina mwisho, hakuna kitu kibaya kama kumzuia mtu asitoe dukuduku lake kwani akizidiwa atalitoa kwa vitendo na hutoweza kumzuia,uvumilivu una mwisho.
 
Kwani Yale Ya TAHRIR SQUARE Yaliyomtoa MUBARAK wa MISRI Yalikuwa Yanaitwaje? Ukipata Jibu Hapo Fanya Kubold Na Kisha Pigia Mstari
Yale ni mapinduzi yaliyofanikiwa hahahaha lakini haya yenu hayatafanikiwa maana majeshi yako tayari kuyadhibiti
 
Kwa uwelewa wako mdogo nakuongezea kuwa mapinduzi hupangwa kwa siri hayatangazwi.ref yale mnayoyatukuza ya unguja. Kwa uelewa wako mdogo kinachotangazwa ni maandamano ya amani neno revolution pale linatumiwa kwa maana ya kutaka kubadili baadhi ya mambo mfano sheria za uchaguzi. Kwa huo uelewa wako mdogo akwilina alifumuliwa kichwa sio kuwa alikuwa anataka kupindua serikali lahasha.alikua abiria na lwa huo uelewa wako mdogo serikali ilipeleka viroba vya mchele huku ikijua imeua raiya asiye na hatia. Kwa uelewa wako mdogo adhabu ya kuandamana sio kuua.kwa uelewa huo mdogo ndo mana unashindwa kuhoji kwann kina mbowe waitwe polisi na wale 40 wapo jela huku hakuna polisi hata mmoja aliyefikishwa mahakamani hali ya kuwa mambo sasa ameshasema polisi walirusha risasi.
Ni hayo tu
 
Kwa mujibu wa hao walioratibu, Malengo ya Tanzania Revolution ni
  1. Kuwaondoa Rais Magufuli na Dr Shein Madarakani
  2. Katiba Mpya
  3. Tume huru za Uchaguzi Zanzibar na Bara
 
Utamu wa maandamano ni kuwa
CCM watapigwa
CHADEMA watapigwa
Wasio na Vyama watapigwa
Mali za Matajiri zitaharibiwa
Mali za maskini zitaharibiwa
Mali za Serikali zitaharibiwa
Mali za Raia zitaharibiwa
Wenye dini watapigwa
Wasio na dini watapigwa
Watiifu wa sheria watapigwa
Wavunja sheria watapigwa

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ikiisha waliobaki wataanza upya.
 
Kuliko kuendelea kutisha watu humu ni kheri ungeenda kuvitawaza vibabu vya kizungu upate hela
 
Moja ya kitu ulichosahau labda nikukumbushe MISRI ni moja ya nchi yenye jeshi imara kabisa Africa na vifaa vya kisasa kuanzia ndege za kivita za kutosha, mamia ya vifaru na gari za delaya, manowari vita na meli za kivita... lakini mwisho wa siku watu walijiselfie na vifaru barabarani..

Hiyo movie haiwezi fanikiwa sio kwa sababu ya jeshi imara la Tanzania lahasha bali kwa sababu ya uoga na ujinga wa watanzania, Hakuna jeshi lenye nguvu kuliko umma, nahuhakikishia hapo Dar es salaam waandamane watu 10000 tu JWTZ haitaweza kuwazuia kamwe, tuombe Mungu na tuache kauli za kejeli haya mambo ni hatari sana Lizaboni...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…