Wewe kweli msahaulifu au unajifanya hivyo?Hakuna maandamano ya amani yenye lengo la Revolution. Nakataa. Polisi na JWTZ msipumbazike na hii hadaa ya wanyonya koni. Jiandaeni kisawasawa kutumia silaha zote
Hahahahahahaaaaaaa. Hapo mmeeleweka. Siku hiyo wanaume wa Kazi watakuwa na zana zote halali. subirini mkufilie mbali wakati huyo anayewahamasisha ananyonya koni huko majuu
Wewe nawe usijivike uwendawazimu. Jeshi halijaumdwa na watu wapumbavu wanaoweza kuvurumisha makombora ya mizinga kwa raia wake tena wasio na silaha. Nimehudumu jeshi, naijua miiko yake.Hapo si CCM tena. Hapo ni wazee wa kazi. JWTZ. Tena ni kitambo hawajatest mitambo yao
Thubutu kufanya mapinduzi uone cha mtema kuni. Jeshini ni Amri tu. Amir Jeshi Mkuu akiamuru waingie vitani wanaingia tu bila shaka. Nasema tena Thubutu kuandamanaWewe nawe usijivike uwendawazimu. Jeshi halijaumdwa na watu wapumbavu wanaoweza kuvurumisha makombora ya mizinga kwa raia wake tena wasio na silaha. Nimehudumu jeshi, naijua miiko yake.
Jeshi liwezacho kufanya ni ulinzi wa maeneo muhimu tu. Linaweza kujibu mashambulizi pale tu kutakapokuwepo watu wanaoshambulia kwa kutumia silaha, na silaha hizo zisiwe fimbo au mawe. Yaliyobakia ni kazi ya polisi, siyo jeshi.
Yale ya Mgabe yalikuwaje kwa mfano!!!Ni maandamano gani ya Aman ambayo yataleta Revolution? hapo wanataka kuletea Mapinduzi. sijajua mmejipangaje kupambana na majeshi katika maandamano yenu. Haya kila la kheri
Siioni sababu ya wananchi kuingia barabarani kuandamana. Bado hatujafikia level hiyoKama wananchi wataamua kuingia barabarani hakuna jeshi linaloweza kuwadhibiti, watanzania raia watu wazima wapo zaidi ya milioni ishirini wakati askari kwa majeshi yote hawafiki hata laki tano.
Sema uoga wetu ndo mtaji wa ccm, kwanza we unafikiri jeshi halina akili liuwe raia wake sasa litakuwa linalinda nini? Hakuna fomula ya kuuwa watu wengi kwa ajili ya mtu mmoja au watu wachache. Tuombe tu amani tuache vitisho na tutende haki. Yaani hutendei watu haki wakidai haki yao unawadhibiti kwa manyanyaso na vitisho, mwisho wake ni mmbaya siku zote.
Serikali dharimu hutolewaMwenyezi Mungu ameweka Serikali za wanadamu Duniani
Marekani walitia mkono..mbona mnatoa mifano ya madikteta?Hata Gadaffi alikuwa na jeshi tena imara kuliko hili.
Wadau, amani iwe kwenu.
Nimefuatilia baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Instagram na Telegram kuhusu haya makundi ya watu wanaotamani kuuangusha utawala wa Rais Magufuli. Kwa kiswahili wanasema kuwa hayo ni maandamano ya Amani. Ila kwa Kiingereza wanatamka Tanzania Revolution.
Kwa uelewa wangu, Maandamano tafsiri yake kwa Kiingereza ni Demonstration au Protests. Na Revolution maana yake kwa kiswahili ni Mapinduzi. Kwa uelewa wangu finyu, busara huweza kutumika katika kudeal na maandamano ikiwa ni pamoja na matumizi kiduchu ya nguvu. Ila Mapinduzi hapo lazima ujidhatiti kukabiliana nayo. Hapo silaha za moto na nzito hutumika na ni haki ya vyombo vya dola kutumia nguvu zote ili kulinda himaya dhidi ya maadui wa ndani na nje.
Kingine, Maandamano hudhibitiwa na Jeshi la Polisi. Ila Mapinduzi hapo wanaume wa kazi, JWTZ huingia mzigoni. Hapo silaha zinazotumika ni za moto tu. Hawajafundishwa kutumia TEAR GAS hao.
Kwa hiyo, ni vema wale wanaotamani kuona utawala wa Rais Magufuli unaangushwa wakatafakari upya ni nini hasa wanataka kufanya siku hiyo na nini madhara yake. Ni vema wakaweka wazi je wanataka kuandamana ama wanataka kufanya mapinduzi? Maandamano YES ila MAPINDUZI ni BIG NO. Watu wasije kufumuliwa vichwa wakifanya mapinduzi then wakaanza kulalamika kuwa jeshi la polisi na JWTZ wametumia nguvu ya ziada.