samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Kamanda wa polisi mkoa wa kinondoni amesema walilazimika kuyatawanya maandamano ya wanachuo kwa kuwa uongozi wa chuo haukua na taarifa zozote na wala haukubariki maandamano hayo. Nijuavyo mimi jeshi la polisi ndilo lenye mamlaka ya kutoa kibali cha maandamano. Kumbukumbu zangu za hivi karibuni zinanionesha kuwa uongozi wa chuo kikuu siku zote umekua ukipinga migomo na maandamano ya wanafunzi na siku zote umekua mstari wa mbele kubandika matangazo ya kuwaonya wanafunzi na kutishia kuchukua hatua za kisheria. Nauliza ni lini uongozi wa chuo umepewa mamlaka ya kubarikia au kuruhusu maandamano ya wanafunzi.