Ni lini uligundua kuwa vita dhidi ya ukoloni mambo leo imetushinda Waafrika

Ukitaka kuushinda ukoloni mamboleo unatakiwa umiliki na kujitosheleza na kuwa na ziada katika haya:

1.Umiliki sayansi pamoja na technolojia.

2.Umiliki mifumo ya hela ikiwa ni pamoja na mifumo ya hela za kielektronic

3.Umiliki mifumo ya uchumi yenye ushindani.

4.Umiliki mifumo ya elimu ambayo elimu inayotolewa inaweza kubadilishwa kuwa products zenye ushindani.

Maana yake ukitaka kupigana na ukoloni mamboleo wekeza kwenye hayo niliyotaja hapo juu na siyo uwekeze kwenye kuwaita wazungu kuwa ni mabeberu.Sasa anatokea mwendawazimu mmoja mwenye PhD fake anataka kupigana na ukoloni mamboleo kwa mikono mitupu na kwa maneno matupu!
 
Siku tukijitambua tukaacha kuwalaumu wengine kwa matatizo na umaskini wwtu itakua mwanzo wa kupiga hatua kusogea mbele.
kaka unge bold hii post yako.
ndio utaratibu tuliojijengea. mpaka wanasiasa wamefanikiwa kutuaminisha kuwa kila baya ,hata kama ni kwa uzembe wetu. lawama kwa "BEBERU".
 
haha enlight me?
Yu are trapped in a very complicated system. Where yu work for your boss without even the presense of him. Its hard to recognize because in your economic system you are sorrounded by the people who looks like yu. Yu should look economic system in a bigger picture. Where there is a bigger economic system which benefit from small economic systems.
 
to be honestly everybody has a boss.
where i work my boss is high ranking goverment official. and his boss is is our current president.

but getting back to your statement. what is the solution?
 
to be honestly everybody has a boss.
where i work my boss is high ranking goverment official. and his boss is is our current president.

but getting back to your statement. what is the solution?
The solution is time( waiting for coincidence). At this point there is nothing yu can do. Its too late. Its that time when yu know somebody is exploiting yu and still nothing yu can do about it. Knowing is one thing, but acting upon is another thing
 
Watawala wote duniani wapo sawa kimipango.
Kila mwanasiasa anawaza maisha yake kwanza. Tofauti iliyopo ni kuwa wapo wanasiasa katili katika kuwatawala binadamu wenzao.
Ukatili katika kutawala ndio kulikoleta utumwa mbaya na usio na haki.
Utumwa ulikuwepo tangu karne za akina Nabii Ibrahimu lakini watumwa walikua na haki zao na ilikua ni dhambi kuizikiuka. Ukoloni ni zao la watawala katili. Kwa sasa hakuna kitu cha ukweli kinachoitwa Ukoloniambo leo toka Nje ya nchi. Ukoloni mambo leo unafanywa na Watawala wa ndani wenyewe ambao wengi wao ni katili na wabinafsi.
Hivi Nchi kama Falme za Kiarabu hakuna wazungu kule ? Iweje wapate maendeleo makubwa kabisa duniani? Bila shaka ni kwa sababu ya uongozi imara wenye kuwajali watu wao.

Afrika na waafrika ni watu wabinafsi. Watu wenye kutamani kila kitu kiwe chao bila hata kukihangaikia. Afrika ni bara ambalo Wasomi wanafanya kazi kwa muda mfupi sana kuliko wasio soma. Yaani mtu akishapata PhD basi anawaza sasa basi ,lengo linakua ni kupata kazi yanye mshahara mkubwa na vikao na safari nyingi na muda mwingi wa kukaa kwenye baa na kunywa pombe na wanawake. Hana muda wa kufikiria matatizo ya waafrika wenzake.
Maarifa yake yanaishia kwenye baa na wanawake. Awe ni profesa atawaza kuwasifia wanasiasa ili atoke jalalani. Akitoka jalalani anaona aibu kuulizwa maswali juu ya msaada wa Elimu yake kwa manufaa ya umma anajificha chini ya mwavuli wa Ukoloni mambo leo na ubeberu.

Hivi kweli nchi maskini kama Tanzania unaweza kuwaza kumjengea Rais Mstaafu mwenye Mtoto Rais nyumba yenye thamani ya kujenga Zahanati 20 halafu unasema kuna ukoloni mambo leo.?
Maana yake hasa ni nini ni kuwa wasomi wa Afrika wamebabe Ukoloni na ubeberu mbaya kuliko waliouleta.

Hivi mpaka leo tatizo tulilonalo kwenye mitaala ya Elimu ni historia ya nchi yetu jamani!! Yaani Profesa amefikia mwisho wa kufikiri nini changamoto za waafrika katika karne hii anawaza kutuletea masulizi nje ya sayansi.

Kwa nini tusianze kushughulika na mifumo ya Elimu inayotumiwa na wanasiasa ( wakoloni weusi ) kutunyonya kwa manufaa ya madaraka yao wenyewe?

Nchi yenye madini kila kona lakini hakuna mitaala ya kuwafundisba watoto kuyajua madini na matumizi yake tangu wakiwa wadogo ili waanze kuyachimba wenyewe na kuyauza kwa wazungu ili tuondoka na kuwaita kuja kuwekeza? Mbona Wanasiasa wamefundishwa siasa na utawala na sasa tunajitawala wenyewe kwa mbinu na mifumo ile ile ya waloloni?
Kwa nini madini tusiwafundishe watoto wetu mapema tangu shule ya msingi ili wajue utajiri mkubwa unaowazunguka. Yaani Elimu ya madini inapatikana vyuoni wakati Elimu za chini haikusomwa.
Kwa nini Mitaala ya Kilimo ,uvuvi,ufugaji isianzie shule ya msingi badala ya kuanzia vyuoni . Wakulima ni 85 % lakini watoto wao hawafundishwi kilimo tangu wakiwa wadogo ili waendeleze shughuli za kilimo ,uvuvi,ufugaji ,misitu,madini n.k? Watoto wanafumdishwa mambo ambayo yanawapa elimu ya kusubiri ajira kwa wahindi na serikali.
Ukiwauliza wanasiasa wanakuambia tatizo ni mabeberu wa ulaya . Hapa mabeberu wanatoka wapi wakati walishatuachia nchi zetu tupange mipango yetu wenyewe??

Bila kubadili mifumo ya Elimu na siasa hatutaweza kujenga mifumo imara ya kiuchumi.

Tujiulize hivi ni kwa nini shirika la nyumba halijengi nyumba kwa ajili ya kupangisha watu wa kawaida ,yani nyumba ni zile za mkoloni mpaka leo hakuna nyumba mahususi kwa ajili ya wananchi ili kuondoa ukali wa maisha.
Leo hii watanzania wengi wanafanya wizi ili watafute makazi na nyumba za ziada kwa ajili ya kupangishia wanyonge.
Serikali ingejenga nyumba za kutosha kwa watu wake kupangisha kwa bei na nafuu ingepunguza wizi mkubwa unaofanywa na maafisa waandamizi ambao kwa kiwango kikubwa wanahujumu nchi ili wajenge majumba ya kupangisha.

Kudhibiti hata mikataba hewa na ufisadi ni serikali kujenga nyumba kwenye miji kupitia shirika la nyumba ili wananchi wafanye kazi kwa uadilifu. Wafanya biashara wanahujumu na kukwepa kodi kwa ajiili ya kulipa kodi kubwa za pango wakato huo huo wanawaza kujenga majumba ili wawapangishie wanyonge.

Ukolomi mambo leo tumebaki nao waafrika wenyewe kwa ubinafsi wetu. Dunia ni kijiji yapo mambo mazuri ya kujifunza toka kwa wazungu na mabaya tukayaacha. Leo tunahangaika kujifunza mabaya na kuyaona kama fasheni.
 
Kama tunahitaji kutoka kwenye huu mtego wa ukoloni mamboleo tufanye tafuatayo:

1) Kubadili mifumo yetu ya Elimu, Elimu yetu bado imeendelea kuzalisha watu tegemezi, watu wasio na uzalendo, na wabinafsi.
Viongozi wetu tunaowalalamikia ni matunda ya mifumo iliyopo.
Elimu yetu ituwezeshe kujitambua na kujikubali sisi kama watanzania na waafrika na kuondoa dhana kua kila kitu kizuri kinatoka na kufanyika Ulaya,
Elimu yetu itukomboe kutoka kwenye vifungo vya utumwa (tuna Uhuru wa bendera ila bado ni watumwa)

2)Kujiondoa kwenye mzunguko wao wa uzalishaji, namaanisha bado sisi kama watanzania tupo kwenye mzunguko wa uzalishaji wa bara Ulaya sisi kama wazalishaji wa malighafi. Sisi bado ni kiungo kikubwa sana kwenye uzalishaji wao. Kujitoa huku ni kwa kukuza uchumi wa viwanda huku kwetu. Kuna malighafi ambazo zinapatikana kwetu tu na wala hawawezi kuzizalisha kwao, Tusitishe uuzaji wa malighafi tuuze bidhaa.

3) Kuwa makini na Mtego wa Misaada na Mikopo.
Katika sehemu ambayo inatufanya kubaki kwenye ukoloni mamboleo ni huu mtego wa Misaada na Mikopo ya mabeberu. Tufanye miradi tunayoipanga wenyewe. Kinachotokea ni kuwa hawa watu wanakuja na kutuambia ninakupa mkopo wa kujenga daraja la salender huku wakijua huo mkopo kwa kua sio sustainable hutaweza kuulipa..hapo ndipo utabakia kua mdeni wao milele. Hata Biblia inasema Mtu anapokudai unakua mtumwa wake.
 
Kwa kifupi unasema tusisinzia kukubali msaada wowote unaokuja kwa jina la hela

Kwa kifupi unamaanisha tuwe makini au tuepuke kabisa msaada wowote kinachokuja kwa jina la pesa. Kwa sababu pesa iko complicated na bado sisi kama waafrika hatujaelewa inavofanya kazi. Huwezi kufurahia kitu ambacho hujui kina fanyaje kazi
 
Kwa kifupi unasema tusisinzia kukubali msaada wowote unaokuja kwa jina la helaKwa kifupi unamaanisha tuwe makini au tuepuke kabisa msaada wowote kinachokuja kwa jina la pesa. Kwa sababu pesa iko complicated na bado sisi kama waafrika hatujaelewa inavofanya kazi. Huwezi kufurahia kitu ambacho hujui kina fanyaje kazi
Ni kweli hii Misaada na Mikopo inakuja na masharti ya ajabu yenye ukandamizaji na unyonyaji...mfano wale waliotusaidia kutujengea mlimani city kumbe wa walikua na mkataba wa miaka 100..ila ilikuja kwa sura ya msaada mpaka baadae ndo kushtuka tunaibiwa
 
Nimegundua kuwa kujinasua kwenye mtego huu wa ukoloni mambo leo ni ngumu, baada ya kuona namna uchaguzi unavyofuatiliwa kwa karibu na mataifa yanayojinasibu kwa majina kama Common wealth, UN, WB, na ofisi za balozi nchini. Hawa jamaa ni mercenaries ni hatari sana ukionyesha msimamo tofauti na sera zao.
 
Wakuu. Ningependa kujua kwa yoyote yule mwenye uelewa mpana wa ukoloni mambo leo unavofanya kazi. Atuambie ni lini alikuja kugundua kwamba vita hiyo ni kubwa sana na waafrika kwa ujumla tunazidi kushindwa. Facts za kihistoria zin ajieleza na hatujawahi kuchomoka kwenye mtego wa mzungu richa ya kuwa kila siku tunajaribu.

Mimi binafsi nilipogundua hatuwezi ku control mfumo wa hela wa dunia na wanao control wanaweza kuprint hela bila kuulizwa nikajua hatutakaa tuchomoke kwenye trap. No matter tunapiga kazi kiasi gani. Huo ndo mtazamo wangu kwa uelewa wangu. Just an opinion.

Wewe je unakuja na nini mezani? Tunajua ukoloni mambo leo upo. Lakini kwa nn hua tuna ignore kama vile ni conspiracy. Ukimwambia mtu kuna ukoloni mambo leo wazo la haraka linalokuja kichwani mwake anahisi unamrudisha shuleni kwenye notes alizokua anasoma kwa kukariri. Na wabongo tusivopenda kusoma anakuona kama unataka kumchallenge kielimu kumbe wewe lengo lako ni kufanya nae majadiliano ya kuweka awareness.
Ukoloni mamboleo ni bora kuliko ukoloni wa mwafrika kwa mwafrika mwenzie mfano:Uganda,Rwanda,Burundi,DRC,Congo na Tanzania awamu ya tano iliyozikwa jana.
 
The solution is time( waiting for coincidence). At this point there is nothing yu can do. Its too late. Its that time when yu know somebody is exploiting yu and still nothing yu can do about it. Knowing is one thing, but acting upon is another thing
in other words back to square 1.
 
Back
Top Bottom