Ni lini uligundua kuwa vita dhidi ya ukoloni mambo leo imetushinda Waafrika

wazanaki

JF-Expert Member
Mar 20, 2020
1,092
804
Wakuu. Ningependa kujua kwa yoyote yule mwenye uelewa mpana wa ukoloni mambo leo unavofanya kazi. Atuambie ni lini alikuja kugundua kwamba vita hiyo ni kubwa sana na waafrika kwa ujumla tunazidi kushindwa. Facts za kihistoria zin ajieleza na hatujawahi kuchomoka kwenye mtego wa mzungu richa ya kuwa kila siku tunajaribu.

Mimi binafsi nilipogundua hatuwezi ku control mfumo wa hela wa dunia na wanao control wanaweza kuprint hela bila kuulizwa nikajua hatutakaa tuchomoke kwenye trap. No matter tunapiga kazi kiasi gani. Huo ndo mtazamo wangu kwa uelewa wangu. Just an opinion.

Wewe je unakuja na nini mezani? Tunajua ukoloni mambo leo upo. Lakini kwa nn hua tuna ignore kama vile ni conspiracy. Ukimwambia mtu kuna ukoloni mambo leo wazo la haraka linalokuja kichwani mwake anahisi unamrudisha shuleni kwenye notes alizokua anasoma kwa kukariri. Na wabongo tusivopenda kusoma anakuona kama unataka kumchallenge kielimu kumbe wewe lengo lako ni kufanya nae majadiliano ya kuweka awareness.
 
Mbinu ya ukoloni & ukoloni mamboleo ni ileile ya siku zote --- ^divide & rule^ Jesus rightly said a house divided against itself cannot stand. Ukiona Waafrika wenzenu wanaanza kuwapigia upatu Wazungu ilhali wakiwatusha Waafrika wenzao, just understand we are close to being doomed forever.
 
Wengi hawatilii maanani maana wanakuwa Kama hawaoni effect yake moja kwa moja tofauti na ilivyokuwa katika utumwa!.. watu wapo bize kujiimarisha kiuchumi wale nini,wavae nini,waishi wapi,wasome wapi n.k
Waonaji wa moja kwa moja ni viongozi ambao nao hunyamazishwa kwa miburungutu au Vito vya thamani sometimes kutishiwa kifo n.k

Wengine hutumia ule msemo if you can't fight them join them!
 
Pale tuliposhindwa kutengeneza hata sindano ya kushonea madabwada yetu, achilia mbali hata sheria tu tumeshindwa kuzitafsiri kwa lugha yetu licha ya kukopi na kupesti kutoka kwa Uingereza.
Mwaka wa 60 wa uhuru ni umri wa babu na bado tungsli maskini lusu licha ya kuwa na dhahabu,almasi,tanzanite nk.
 
Mm niligundua hili,pale wazungu walipoanza kukataa mifumo ya ujamaa na kujitegemea.

Hapa wazungu walilenga kwenye mambo makuu matatu.

1. hapa wazungu wameanza kutudhibiti kwenye uwezo wa akili na kujitambua. Wameanzia kwenye elimu za shule hadi vyuo watu wanakremishwa tu lakini sio uhalisia.

2 wamezibiti mifumi ya uzarishaji,hapa wazungu wameanza kudhibiti uwezo wa viwanda, wamehakikisha hamzalishi umeme wa kutosha wa kuanzisha na kuendesha viwanda vikubwa na vya kutosha ingawa maligafi mnazo.
Kupitia kitengo chao cha umoja wa mataifa I.A,E,A wameweka mipaka na vigezo vya kurutubusha uranium ambao ndio unaweza kutengeneza umeme wa uhakika.
Badala yake.wametuacha kuhangaika na umeme wa maji na gesi ambao kwa wao wenyewe umeme wa maji umeshapitwa na wakati.

Kwa huku kwetu Africa hakuna hata nchi moja iliyokidhi vigezo vya kutumia uranium.

Tuangalie hasa hapa kwenye nguvu ya umeme.

Ghana walijenga bwawa la umeme lenye kuzalisha mega watt 840 hivi,lakini kumbe lengo lao ni kutumia kwenye mladi wao wa kuvuna madini ya alluminium ,kalibu megawatt 600 bado wanatumia wao wenyewe kubeba malighafi za wagana.

Tumeona tena Ethiopia wamejenga bwawa la umeme mkubwa lakini hadi leo kumbe umeme ule wanatumia kutengenezea silaha zao.

Sasa tuwe waangalifu hata hapa kwetu leo tunajenga umeme wa mega 2200.
Je kuna lengo madhubuti kwa matumizi ya watanzania?
au kuna wanaokuja kuwekeza kwa faida zao!?
au kuna malighafi wanataka kubeba pia kama walivyofanya kwa wagana na ethiopia kwa kujisifu tuna umeme mwingi kumbe wanakazi zao wenyewe za kutuibia mali zetu.

3..ukidhibitiwa kwenye mifumo ya uzalishaji mali automatically umezibitiwa kwenye mifumo ya kifedha.
Hivyo kiongozu yeyote wa afrika atakae thubutu kwenda kinyume na matakwa yao hawezu kubak salama, kama alivyofanywa gadafi nawengine.

Wazungu wanajua,ukiweza kulutubusha uranium kwako utaweza kujenga setelite yako utakua na mawasiliano yako,hivyo utadhibiti mambo yako ya usalama nk,
Lakini pia utaweza kujenga viwanda vyako vikubwa na vidogo,ns kwakua una malighafi za kutosha hutokua na shida na wazung.
Sasa wazungu hawana malighafi yoyote hata pakulima mchicha tu shida.
Hivyo ni lazima wafanya hivyo ili waendelee kututawala kisasa.
 
Una vizuri mkuu
 
Huu

Ndio ukoloni mamboleo
 
Mkuu uko vizuri. Unauelewa mpana wa mifumo. Nafurahi nikiona my fellow tanzanian tena katika lugha ya kiswahili wakiwa na uelewa mkubwa kiasi hiki. Inanifurahisha kuona mambo yaliyo complicated yanaanza kua simple kueleweka
 
Mm niligundua hili,pale wazungu walipoanza kukataa mifumo ya ujamaa na kujitegemea.

Hapa wazungu walilenga kwenye mambo makuu matatu.

1. hapa wazungu wameanza kutudhibiti kwenye uwezo wa akili na kujitambua. Wameanzia kwenye elimu za shule hadi vyuo watu wanakremishwa tu lakini sio uhalisia.

2 wamezibiti mifumi ya uzarishaji,hapa wazungu wameanza kudhibiti uwezo wa viwanda, wamehakikisha hamzalishi umeme wa kutosha wa kuanzisha na kuendesha viwanda vikubwa na vya kutosha ingawa maligafi mnazo.
Kupitia kitengo chao cha umoja wa mataifa I.A,E,A wameweka mipaka na vigezo vya kurutubusha uranium ambao ndio unaweza kutengeneza umeme wa uhakika.
Badala yake.wametuacha kuhangaika na umeme wa maji na gesi ambao kwa wao wenyewe umeme wa maji umeshapitwa na wakati.

Kwa huku kwetu Africa hakuna hata nchi moja iliyokidhi vigezo vya kutumia uranium.

Tuangalie hasa hapa kwenye nguvu ya umeme.

Ghana walijenga bwawa la umeme lenye kuzalisha mega watt 840 hivi,lakini kumbe lengo lao ni kutumia kwenye mladi wao wa kuvuna madini ya alluminium ,kalibu megawatt 600 bado wanatumia wao wenyewe kubeba malighafi za wagana.

Tumeona tena Ethiopia wamejenga bwawa la umeme mkubwa lakini hadi leo kumbe umeme ule wanatumia kutengenezea silaha zao.

Sasa tuwe waangalifu hata hapa kwetu leo tunajenga umeme wa mega 2200.
Je kuna lengo madhubuti kwa matumizi ya watanzania?
au kuna wanaokuja kuwekeza kwa faida zao!?
au kuna malighafi wanataka kubeba pia kama walivyofanya kwa wagana na ethiopia kwa kujisifu tuna umeme mwingi kumbe wanakazi zao wenyewe za kutuibia mali zetu.

3..ukidhibitiwa kwenye mifumo ya uzalishaji mali automatically umezibitiwa kwenye mifumo ya kifedha.
Hivyo kiongozu yeyote wa afrika atakae thubutu kwenda kinyume na matakwa yao hawezu kubak salama, kama alivyofanywa gadafi nawengine.

Wazungu wanajua,ukiweza kulutubusha uranium kwako utaweza kujenga setelite yako utakua na mawasiliano yako,hivyo utadhibiti mambo yako ya usalama nk,
Lakini pia utaweza kujenga viwanda vyako vikubwa na vidogo,ns kwakua una malighafi za kutosha hutokua na shida na wazung.
Sasa wazungu hawana malighafi yoyote hata pakulima mchicha tu shida.
Hivyo ni lazima wafanya hivyo ili waendelee kututawala kisasa.
Nenda tena katafute ukweli kuhusu malighafi,utafute nchi zinazoongoza kwa malighafi duniani halafu utupe mrejesho.
 
NB:Usije ukaiingiza marekan kwenye hili,maana hata yeye alitawaliwa japo enzi zile.
Lakini pia marekani ni inamchanganyiko wa mataifa yote na haina mwenyewe.
 
Marekani yenyewe inaendeshwa hakuna aliye salama. Tofauti yake ni kwamba inaendashwa na kutumiwa kama nyenzo ya kuwakalia wengine
 
Nimeomba mrejesho wa nchi zinazoongoza kwa nature resources duniani ili tujue wazungu hawana?
 
Marekani yenyewe inaendeshwa hakuna aliye salama. Tofauti yake ni kwamba inaendashwa na kutumiwa kama nyenzo ya kuwakalia wengine
Marekani ni extension ya uingereza. "Whites". Wengine waliomo( blacks, wahindi, wachina na latino) ni watumwa. Wote wanamtumikia malkia
 
msingi wa elim yetu unatuandaa kufanya kazi za kitaaluma, na sio kuzalisha maarifa mapya kulingana na taaluma zetu.

hata leo tukibadili msingi wa elim yetu ukawa kwa ajili ya kuzalisha maarifa mapya itakua rahisi sana kuushinda ukoloni mambo leo.
 
Sisi sote ni product ya elimu ya mkoloni. Walio chomoka kwenye mtego ni wale wanaojishughulisha kusoma na kudadisi. tofauti na wale ambao wanasoma tu elimu ya mkoloni.
 
Mm niligundua hili,pale wazungu walipoanza kukataa mifumo ya ujamaa na kujitegemea.

Hapa wazungu walilenga kwenye mambo makuu matatu.

1. hapa wazungu wameanza kutudhibiti kwenye uwezo wa akili na kujitambua. Wameanzia kwenye elimu za shule hadi vyuo watu wanakremishwa tu lakini sio uhalisia.

2 wamezibiti mifumi ya uzarishaji,hapa wazungu wameanza kudhibiti uwezo wa viwanda, wamehakikisha hamzalishi umeme wa kutosha wa kuanzisha na kuendesha viwanda vikubwa na vya kutosha ingawa maligafi mnazo.
Kupitia kitengo chao cha umoja wa mataifa I.A,E,A wameweka mipaka na vigezo vya kurutubusha uranium ambao ndio unaweza kutengeneza umeme wa uhakika.
Badala yake.wametuacha kuhangaika na umeme wa maji na gesi ambao kwa wao wenyewe umeme wa maji umeshapitwa na wakati.

Kwa huku kwetu Africa hakuna hata nchi moja iliyokidhi vigezo vya kutumia uranium.

Tuangalie hasa hapa kwenye nguvu ya umeme.

Ghana walijenga bwawa la umeme lenye kuzalisha mega watt 840 hivi,lakini kumbe lengo lao ni kutumia kwenye mladi wao wa kuvuna madini ya alluminium ,kalibu megawatt 600 bado wanatumia wao wenyewe kubeba malighafi za wagana.

Tumeona tena Ethiopia wamejenga bwawa la umeme mkubwa lakini hadi leo kumbe umeme ule wanatumia kutengenezea silaha zao.

Sasa tuwe waangalifu hata hapa kwetu leo tunajenga umeme wa mega 2200.
Je kuna lengo madhubuti kwa matumizi ya watanzania?
au kuna wanaokuja kuwekeza kwa faida zao!?
au kuna malighafi wanataka kubeba pia kama walivyofanya kwa wagana na ethiopia kwa kujisifu tuna umeme mwingi kumbe wanakazi zao wenyewe za kutuibia mali zetu.

3..ukidhibitiwa kwenye mifumo ya uzalishaji mali automatically umezibitiwa kwenye mifumo ya kifedha.
Hivyo kiongozu yeyote wa afrika atakae thubutu kwenda kinyume na matakwa yao hawezu kubak salama, kama alivyofanywa gadafi nawengine.

Wazungu wanajua,ukiweza kulutubusha uranium kwako utaweza kujenga setelite yako utakua na mawasiliano yako,hivyo utadhibiti mambo yako ya usalama nk,
Lakini pia utaweza kujenga viwanda vyako vikubwa na vidogo,ns kwakua una malighafi za kutosha hutokua na shida na wazung.
Sasa wazungu hawana malighafi yoyote hata pakulima mchicha tu shida.
Hivyo ni lazima wafanya hivyo ili waendelee kututawala kisasa.
Huu ni Uongo na mbinu za kujitetea tu. Nchi ikitaka kuendelea itaendelea tu.

Mbona malaysia, brazil, India, China, South Africa, Nigeria wanaenda vizuri tu.

Ili nchi iendelee inahitaji mambo 4
1 Watu
2 Ardhi
3 Siasa Safi
4 Uongozi bora.

Kinachotushinda kutoka kwenye ukoloni mamboleo uliojaa umasikini Hasa kwa nchi yetu ninayoishi, Mosi ni SIASA CHAFU INAYOPELEKEA KUPATA UONGOZI DHAIFU.
MFN. Magufuli Alianza vizuri ila hakuwa na Siasa Safi ndy iliyopelekea akashindwa kubadili katiba iliyojaa udhaifu mkubwa. Nchi inataka sheria ngumu zinazopelekea Kila kiongozi kuwajibika ipasavyo.
Chukua mfano Chama cha siasa kinatakiwa kumsimamia Raisi,Mbunge na Diwani kuwajibikia ilani yao. Wakati huo Rais ni Mwenyekiti wa hicho chama na wajumbe ni hao wabunge ambao huzaliwa Mawaziri. Nguvu ya chama inakufa kimyaaaaa.

Ukoloni huo tumeupenda kwa uoga wetu wananchi.
 
Back
Top Bottom